Haya yanayotokea Tanganyika yametokea kote duniani. Tatizo ni kwamba tuliaminishwa kwamba sisi tuna kitu cha ziada kuliko majirani kama Rwanda, Kenya, Uganda, Kongo na Burundi. Sasa hiyo ngano (A Myth) imepasuka na ukweli umefahamika kwamba kumbe tuko sawa tu. Watanganyika na kuamini kwamba wao ni wa kipekee (Exceptionalism) ndiyo imetufikisha hapa. Watawala wanafanya chochote kile halafu wanajiliwaza kwa kusema hawa watu hawawezi kufanya lolote lile. Sasa wamefanya na wataendelea kufanya.
Kiuhalisia, serikali zote huwa zinazaliwa na kuanguka. CCM haina utofauti na serikali zilizowahi kuwepo hapa duniani kwa miaka zaidi ya 6000 tangu ustaarabu uanze. Mabadiliko huwa yanakuja tu (Change Is Constant), inategemea umejipangaje kuyakabili. Tanganyika haikujipanga kuyakabili mabadiliko na yamekuja kwa ghafla. Sisi tuko kama meli ya The Titanic ambayo iliaminiwa kwamba haiwezi kuzama, ila kiko wapi sasa. Serikali ya CCM na taasisi zake ndiyo viko ukingoni, sasa itategemea wataondoka kwa busara au lazima damu imwagike.
Kule Uingereza walinyonga mfalme wao, baadaye mtoto wake katawala akaanza ujinga uleule wa baba yake watu wakamfuata na ashukuru alikuwa na akili akakubali kuachia madaraka. Kule Urusi Ramanov walitawala kwa miaka zaidi ya 300 na hawakuamini kwamba kuna siku watatoka. Mwaka 1907 warusi waliandamana na kina Ramanov wakitumia shirika lao la kijasusi (THE OKHRANA) ambalo lilikuwa ni hatari waliaua, kuteka, kufunga na kutesa maelfu ya warusi. Wakajua yameisha.
Urusi imeingia kwenye WW1 raia wake wenye kisasi wakajiunga na Ujerumani kuhujumu nchi. Waliwasaidia wajerumani kuitwanga Urusi na kuitoa kwenye vita mwaka 1917, halafu wakaikamata familia iliyohusika na kuua maelfu ya ndugu zao miaka kumi nyuma. Walikamata familia nzima ya Ramanov na kuitandika risasi bila kumsazia hata mtoto. Vladmir Lenin ambaye alitoa hiyo amri alishuhudia kaka yake akinyongwa na serikali ya Ramanov, hivyo akalipiza kisasi.
KIUFUPI, kinachotokea barani Afrika hakina utofauti ni mapinduzi yaliyowahi kutokea Ulaya mnamo mwaka 1848 (1848 Revolutions) ambapo mataifa zaidi ya 50 yalighubikwa na vuguvugu za kutaka mabadiliko. Mapinduzi yalianzia Ufaransa mwaka 1848, ambapo walipindua kabisa mfalme wao na kuanzisha Jamhuri. Ila hasira zote hizi zilianza pale kabla ya maandamano, serikali ya Ufaransa kutumia nguvu kubwa kuanza kuua watu kikatili. Baada ya watu kuona Ufaransa imewezekana kikanuka Ulaya kote. Hivyo hawa Gen-Z wanapoona kwingine imewezekana basi fahamu fika lazima waige na hapa.
Kabla ya 1848, mataifa ya Ulaya yenye mifumo ya kifalme hayakutaka kubadilika, hivyo mwaka 1814 baada ya kumuangusha Napoleon yakapanga mkakati kule VIENNA (The Vienna Congress) wakishirikiana na Kanisa Katoliki kwamba wahakikishe wanaunda mtandao wa kupinga mabadiliko kutoka kwenye THEOCRATIC ABSOLUTE MONARCHIES to REPUBLICANISM. Kinara wa huo mchezo alikuwa ni Clemens Von Metternich ambaye aliunda mtandao wake wa kijasusi Ulaya nzima, kushughulikia wanaotaka mabadiliko. HAKUWEZA...
Ila mwaka 1848, Ujasusi wake na ule wa Kanisa vilifeli vibaya mno na watu walipindua kabisa falme na kuanzisha CONSTITUTIONAL MONARCHIES. Serikali iliyopona baada ya haya machafuko ni moja tu, PRUSSIA. Ukiuliza kwanini ilipona ni kwamba walifanya mabadiliko makubwa ya katiba na kuruhusu ULIBERALI ambapo watu waliruhusiwa kuishi maisha yao watayakayo. Mataifa yaliyokomaa kama AUSTRIA ambalo ndiyo lilikuwa na nguvu ulaya ilikula kwao. Baada ya hayo mabadiliko PRUSSIA ikajikuta inapata maendeleo kuliko taifa lolote Ulaya mwisho kuunganisha mataifa zaidi ya 30 na kutengeneza taifa la Ujerumani.
Hii CCM hii na TISS+PT+TPDF walioua maelfu ya Watanganyika hawataamini kitakachotokea hapa....