PostGE2025 Tume ya Uchunguzi yenye lengo la kudogosha mauaji ya watanganyika

PostGE2025 Tume ya Uchunguzi yenye lengo la kudogosha mauaji ya watanganyika

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kwenye sayansi ya migogoro, hapa tunakoelekea ni CLIMAX/PEAK OF THE CONFLICT, na mambo yatarudi kawaida mpaka pale machafuko makubwa zaidi yatokee na pande zote mbili zipate madhara ndiyo kukaa mezani kutawezekana.
Mkuu naunga mkono hoja kuwa HADI PANDE ZOTE ZIPATE MADHARA ndio tutakaa mezani.

Otherwise, Only God knows. Time will tell
 
SITA, nchi za Magharibi zina ushahidi wa kutosha juu ya haya mauaji yanayoendelea nchini. Wanafahamu hadi MASS GRAVES zilipo, sema hawawezi kufanya chochote kwasababu wanakula na CCM. Hivyo huu ushahidi watautumia kama BLACK-MAIL CARD dhidi ya SAMIA na JAKAYA kwenye uporaji wa rasilimali za nchi. Mpaka sasa Watanganyika msijidanganye kwamba serikali hii inaweza kufanya lolote kwa maslahi yenu, ilhali iko BLACK-MAILED.
Mwisho nimejua sababu halisi ya kwa nini viongozi wengi Africa huwa wanafanya maamuzi ya kufedhesha.

Asante sana kwa uzi huu wenye elimu kamambe ya masuala ya kisheria
 
Wewe mpumbavu kama mtoa mada, kaanza kwa kuorodhesha watu wenye 'mamlaka' wanaopaswa kwenda ICC
Kikwete ana mamlaka gani,rais mstaafu atamuamuru nani?
..genocide ya Rwanda, Félicien Kabuga alikuwa na Mamlaka..?
 
Napingana na hoja yako.
Haki, usawa, na ustawi hutokana na taasisi imara, na sio dini. Na pia kumbuka kuna ukristo kama tamaduni na si dini.
..taasisi imara zipi, zinaanzia wapi? ukweli ni kwamba haki na usawa vinaanza kufundishwa nyumbani at a family level, dini inaelekeza familia kufundisha watoto juu ya haki na usawa kuanzia sala za familia, hizo taasisi zinajenga mafanikio kwenye msingi huo, wa mtu kukua ktk malezi yanayomfundisha haki na usawa toka akiwa mdogo..na kinyume chake ndio huko kufeli kwa taasisi hizo sababu huwezi mfundisha au kumlazimisha mtu mzima afahamu haki na usawa kwenye utu uzima..mafundisho ya dini ktk level ya familia ni nguzo ya jamii iliyostaraabika!
 
..genocide ya Rwanda, Félicien Kabuga alikuwa na Mamlaka..?
Kule Rwanda kuna mchungaji wa kanisa la Wasabato (SDA) anaitwa Elizaphan Ntakirutimana alikuwa ndiyo mchungaji wa kwanza kabisa kushitakiwa kwa makosa ya mauaji ya Watutsi kule ICTR. Yeye hakuwa kiongozi lakini alisaidia utekelezwaji wa ule ukatili, kisheria tunasema "Aiding and Abetting". Ndiyo maana nasema hizi Propaganda zinazoenezwa kipindi hiki na machawa, waandishi wa habari, majasusi na viongozi wa dini siku nchi ikiingia kwenye matatizo wasidhani kwamba wao watapona hata kidogo.

Kule ICTY kuna mwingine alikuwa anaitwa Dusko Tadic, hakuwa afisa wa jeshi wala kiongozi, lakini alikuwa ni raia wa kawaida anayechukia mno Waislamu. Wakati wa vita akaamua mwenyewe kuuwa watu kikatili sana na kubaka wanawake. Alishitakiwa vizuri tu.

Watu wote wanaomzunguka Raisi watashitakiwa vizuri tu, mpaka pale itakapoonekana hawana hatia. Charles Taylor alishitakiwa kwa makosa ya Sierra Leone japo yeye alikuwa ni raisi wa Liberia. Nafasi yake ya ushawishi ilikuwa ni kubwa mno kwenye siasa za Sierra Leone. Sasa huyu JAKAYA anapojifanya yeye ni THE GREY CARDINAL, lazima yatamtokea puani. Amini nakwambia huyu Mzee siku siyo nyingi yatamtokea puani.
​
 
..taasisi imara zipi, zinaanzia wapi? ukweli ni kwamba haki na usawa vinaanza kufundishwa nyumbani at a family level, dini inaelekeza familia kufundisha watoto juu ya haki na usawa kuanzia sala za familia, hizo taasisi zinajenga mafanikio kwenye msingi huo, wa mtu kukua ktk malezi yanayomfundisha haki na usawa toka akiwa mdogo..na kinyume chake ndio huko kufeli kwa taasisi hizo sababu huwezi mfundisha au kumlazimisha mtu mzima afahamu haki na usawa kwenye utu uzima..mafundisho ya dini ktk level ya familia ni nguzo ya jamii iliyostaraabika!
Nazungumzia taasisi za kijamii na kiserikali, ambazo zinalinda haki na usawa wa jamii yote. Maana kuna utofauti ya kuwa na malezi bora nyumbani na kuwa na mfumo bora unaohakikisha haki na usawa kwa watu wote bila kujali familia walizotoka. Unaweza kuwa na familia yenye maadili, lakini bila sheria na taasisi imara, bado haki na usawa vitavunjwa tu. Unaweza kulelewa vizuri nyumbani, lakini bila sheria imara, haki zako bado zinaweza kuvunjwa, Mzee!. au familia inaweza kufundisha usawa, lakini taasisi ya hovyo kama tulizonazo zinaweza kuruhusu rushwa, upendeleo au ukandamizaji kwa jamii flani.

Na pia kumbuka tuna jamii nyingi tu zilizostarabika, na dini sio nguzo kuu.
 
Sasa jakaya anaingiaje hapo,au unaendeleza chuki alizokujaza askofu aliyesema 'mtu ukistaafu kaa mbali na

AFRIKA KUSINI YA MAKABURU.
Baada ya vita baridi (Cold War) kuisha 1991, Afrika Kusini kulikuwa na vuguvugu zito ambalo lingepelekea vita kubwa mno (Racial War) na umwagikaji mkubwa wa damu. Makaburu waliusoma mchezo mapema sana, na kina De Clarke wakaenda gerezani kumpigia magoti Mzee Nelson Mandela. Kama wangeendelea kukomaa basi machafuko makubwa yangetokea na mauaji yangekuwa ya kutisha mno. Ila walikubali kushindwa kimkakati na kufanikiwa kwa sehemu kubwa kuwahadaa wananachi kupitia The Truth Commission.

MOROCCO 2011 (ARAB SPRING)
Wakati machafuko yameanza Tunisia, Libya, Egypt na Syria, mfalme wa Morocco Idriss alitoka nje na kutoa hotuba kukubali mabadiliko. Mwaka huohuon walifanya mabadiliko ya katiba na uchaguzi wa wabunge. Morocco ikatulia tuli, na maandamano yakawa yameisha kihivyo yani. Serikali ya Morocco ina nguvu mno, tokea miaka na miaka. Majasusi wao na jeshi lao wanapewa mafunzo na mataifa kama Israel, Ufaransa na Marekani, hivyo siyo taifa la mzaha-mzaha. Mfalme Idriss alikuwa anaweza kuamua kuua tu maelfu ya watu wanaoandama kama ambavyo CCM+TISS+PT+TPDF walifanya, ila alitumia hekima ya hali ya juu mno.

Waliokomaa kama kina Mubarak, Ghaddafi na Assad kutumia silaha nzito yaliwakuta. Kiufupi hata uwe kiongozi mzuri vipi, ni lazima ujifunze kusoma alama za nyakati na kufahamu ni wakati upi unatakiwa kuondoka. Hata kama maandamano yanaratibiwa na watu wa nje, basi ni lazima kuna nyufa fulani ambazo adui amezikuta na akaamua kuzitumia. Ghaddafi tunampenda, lakini ukweli ni kwamba kuna mambo mengi utawala wake ulikosea sana kufanya nchini mle. Sasa hili somo JAKAYA ataenda kujifunza muda siyo mrefu..
​
Naam umeshiba nondo, maandiko yako hayachoshi mtu kusoma unarefer events with vivid examples.
 
Nazungumzia taasisi za kijamii na kiserikali, ambazo zinalinda haki na usawa wa jamii yote. Maana kuna utofauti ya kuwa na malezi bora nyumbani na kuwa na mfumo bora unaohakikisha haki na usawa kwa watu wote bila kujali familia walizotoka. Unaweza kuwa na familia yenye maadili, lakini bila sheria na taasisi imara, bado haki na usawa vitavunjwa tu. Unaweza kulelewa vizuri nyumbani, lakini bila sheria imara, haki zako bado zinaweza kuvunjwa, Mzee!. au familia inaweza kufundisha usawa, lakini taasisi ya hovyo kama tulizonazo zinaweza kuruhusu rushwa, upendeleo au ukandamizaji kwa jamii flani.

Na pia kumbuka tuna jamii nyingi tu zilizostarabika, na dini sio nguzo kuu.
..ungezitaja hizo jamii km zipo, kuvunjwa kwa haki na usawa lazima kuwepo sabab binadamu tunatofautiana, hata hivyo kiwango cha uvunjifu kuwa mkubwa au mdogo unategemea sana jamii inajengwa katika misingi gani, kuweka sheria hakujawahi kuondoa tatizo..unaweza kupunguza au kuondoa tatizo pale tu unashughulika na chanzo cha tatizo..ni hatua ipi hasa unaweza kutengeneza jamii iliyostaarabika..? nadhani mafundisho ya dini kuanzia ngazi ya familia yana mchngo mkubwa zaidi kuliko kuweka taasisi nyingi kusimamia haki na usawa..hapo ni kukimbizana na matokeo baada ya kushindwa kushughulika na chanzo cha tatizo..
 
Haya yanayotokea Tanganyika yametokea kote duniani. Tatizo ni kwamba tuliaminishwa kwamba sisi tuna kitu cha ziada kuliko majirani kama Rwanda, Kenya, Uganda, Kongo na Burundi. Sasa hiyo ngano (A Myth) imepasuka na ukweli umefahamika kwamba kumbe tuko sawa tu. Watanganyika na kuamini kwamba wao ni wa kipekee (Exceptionalism) ndiyo imetufikisha hapa. Watawala wanafanya chochote kile halafu wanajiliwaza kwa kusema hawa watu hawawezi kufanya lolote lile. Sasa wamefanya na wataendelea kufanya.

Kiuhalisia, serikali zote huwa zinazaliwa na kuanguka. CCM haina utofauti na serikali zilizowahi kuwepo hapa duniani kwa miaka zaidi ya 6000 tangu ustaarabu uanze. Mabadiliko huwa yanakuja tu (Change Is Constant), inategemea umejipangaje kuyakabili. Tanganyika haikujipanga kuyakabili mabadiliko na yamekuja kwa ghafla. Sisi tuko kama meli ya The Titanic ambayo iliaminiwa kwamba haiwezi kuzama, ila kiko wapi sasa. Serikali ya CCM na taasisi zake ndiyo viko ukingoni, sasa itategemea wataondoka kwa busara au lazima damu imwagike.

Kule Uingereza walinyonga mfalme wao, baadaye mtoto wake katawala akaanza ujinga uleule wa baba yake watu wakamfuata na ashukuru alikuwa na akili akakubali kuachia madaraka. Kule Urusi Ramanov walitawala kwa miaka zaidi ya 300 na hawakuamini kwamba kuna siku watatoka. Mwaka 1907 warusi waliandamana na kina Ramanov wakitumia shirika lao la kijasusi (THE OKHRANA) ambalo lilikuwa ni hatari waliaua, kuteka, kufunga na kutesa maelfu ya warusi. Wakajua yameisha.

Urusi imeingia kwenye WW1 raia wake wenye kisasi wakajiunga na Ujerumani kuhujumu nchi. Waliwasaidia wajerumani kuitwanga Urusi na kuitoa kwenye vita mwaka 1917, halafu wakaikamata familia iliyohusika na kuua maelfu ya ndugu zao miaka kumi nyuma. Walikamata familia nzima ya Ramanov na kuitandika risasi bila kumsazia hata mtoto. Vladmir Lenin ambaye alitoa hiyo amri alishuhudia kaka yake akinyongwa na serikali ya Ramanov, hivyo akalipiza kisasi.

KIUFUPI, kinachotokea barani Afrika hakina utofauti ni mapinduzi yaliyowahi kutokea Ulaya mnamo mwaka 1848 (1848 Revolutions) ambapo mataifa zaidi ya 50 yalighubikwa na vuguvugu za kutaka mabadiliko. Mapinduzi yalianzia Ufaransa mwaka 1848, ambapo walipindua kabisa mfalme wao na kuanzisha Jamhuri. Ila hasira zote hizi zilianza pale kabla ya maandamano, serikali ya Ufaransa kutumia nguvu kubwa kuanza kuua watu kikatili. Baada ya watu kuona Ufaransa imewezekana kikanuka Ulaya kote. Hivyo hawa Gen-Z wanapoona kwingine imewezekana basi fahamu fika lazima waige na hapa.

Kabla ya 1848, mataifa ya Ulaya yenye mifumo ya kifalme hayakutaka kubadilika, hivyo mwaka 1814 baada ya kumuangusha Napoleon yakapanga mkakati kule VIENNA (The Vienna Congress) wakishirikiana na Kanisa Katoliki kwamba wahakikishe wanaunda mtandao wa kupinga mabadiliko kutoka kwenye THEOCRATIC ABSOLUTE MONARCHIES to REPUBLICANISM. Kinara wa huo mchezo alikuwa ni Clemens Von Metternich ambaye aliunda mtandao wake wa kijasusi Ulaya nzima, kushughulikia wanaotaka mabadiliko. HAKUWEZA...

Ila mwaka 1848, Ujasusi wake na ule wa Kanisa vilifeli vibaya mno na watu walipindua kabisa falme na kuanzisha CONSTITUTIONAL MONARCHIES. Serikali iliyopona baada ya haya machafuko ni moja tu, PRUSSIA. Ukiuliza kwanini ilipona ni kwamba walifanya mabadiliko makubwa ya katiba na kuruhusu ULIBERALI ambapo watu waliruhusiwa kuishi maisha yao watayakayo. Mataifa yaliyokomaa kama AUSTRIA ambalo ndiyo lilikuwa na nguvu ulaya ilikula kwao. Baada ya hayo mabadiliko PRUSSIA ikajikuta inapata maendeleo kuliko taifa lolote Ulaya mwisho kuunganisha mataifa zaidi ya 30 na kutengeneza taifa la Ujerumani.

Hii CCM hii na TISS+PT+TPDF walioua maelfu ya Watanganyika hawataamini kitakachotokea hapa....
​
Uchambuzi murua kabisa👏👏
 
Pia tume wachunguze na watuambie hizo asilimia 97 za ushindi wa rais samuya zimetoka wapi ? Pengine mzizi wa tatizo uko hapo maana serikali dhalimu hufanya mambo ya kidhalimu ndio maana mauaji yaliyofanywa kwao sio BIG DEAL wako bze kugawana madaraka tu
 
Wewe mpumbavu kama mtoa mada, kaanza kwa kuorodhesha watu wenye 'mamlaka' wanaopaswa kwenda ICC
Kikwete ana mamlaka gani,rais mstaafu atamuamuru nani?
Nikikuambia huna akili usiwe una kasirika ndo ukweli

Kesi za mauaji nani alikuambia wanakamatwa walioko kwenye mamlaka TU , nyuma ya Haya mauaji Kuna wasuka mipango washauri chain ni ndefu

Rudia kusoma hii Aya Ili uone kiwango chako Cha ujinga

Hivyo hapa watu kama JAKAYA MRISHO KIKWETE, ABDALLAH BULEMBO, RAJAB LUHWAVI, ABDUL AMEIR, ROSTAM AZIZ, ANGELLAH KIZIGHA na HAJI OMAR KEIR, hawawezi kujinasua hata kidogo, mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo. Kisheria kwenye JOINT CRIMINAL ENTERPRISE (JCE) tunachoangalia ni UFAHAMU WA TUKIO (The Mental Element), kwamba uko ndani ya taasisi ya kiusalama au kisiasa na ulikuwa unafahamu kwamba kuna mipango michafu inapangwa.
 
Nikikuambia huna akili usiwe una kasirika ndo ukweli

Kesi za mauaji nani alikuambia wanakamatwa walioko kwenye mamlaka TU , nyuma ya Haya mauaji Kuna wasuka mipango washauri chain ni ndefu

Rudia kusoma hii Aya Ili uone kiwango chako Cha ujinga

Hivyo hapa watu kama JAKAYA MRISHO KIKWETE, ABDALLAH BULEMBO, RAJAB LUHWAVI, ABDUL AMEIR, ROSTAM AZIZ, ANGELLAH KIZIGHA na HAJI OMAR KEIR, hawawezi kujinasua hata kidogo, mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo. Kisheria kwenye JOINT CRIMINAL ENTERPRISE (JCE) tunachoangalia ni UFAHAMU WA TUKIO (The Mental Element), kwamba uko ndani ya taasisi ya kiusalama au kisiasa na ulikuwa unafahamu kwamba kuna mipango michafu inapangwa.
🤣🤣🤣 Nikikujibu tena niite mbwa
 
Nime click report button nadhani wataona.
Nashukuru sana wamerekebisha.

Japo mimi kichwa changu cha habari kilitumia METAPHOR ya TUME KUTOKA KUZIMU (COMMISSION FROM HELL), ambao ni msemo wa kisheria unaotumika na nchi za COMMONWEALTH pale ambapo serikali inaunda TUME au KAMATI kwa ajili ya kupindisha ukweli, kudharirisha, kufilisi watu, au kukomeshana. Huu msemo unatumika sana mahakamani, hata zile kamati za SOKOINE za wahujumu uchumi ziliitwa COMMITTEES FROM HELL, haina tofauti na ule msemo wa LIST OF SHAME au PARADE OF HORRIBLES kwenye masuala ya kodi.

Sasa hawa MODERATORS wetu wanarekebisha kila kitu mwishowe wanatoka hadi kwenye mstari. Wasipokielewa kitu, basi tayari wanapita nacho wanaweka kile cha kwao.
​
 
...basi tayari wanapita nacho wanaweka kile cha kwao.
Nimekupata Mkuu.

Najaribu kuvaa viatu vya moderators. Labda kutokana na mchanganyiko wa watumiaji wa mtandao huu na utofauti wa uelewa wa masuala ya kisheria pia katika kupunguza kushtua baadhi ya hao hao watumiaji wameona waboreshe kama walivyofanya.

Neno kuzimu(hell) laweza kutafsiriwa tofauti ukizingatia Uzi huu haupo kwenye lile jukwaa la masuala ya kisheria.

Hata hivyo, kwa ufafanuzi uliotoa basi tulio wengi watumiaji wa mtandao huu na ambao tumefuatilia kwa Karibu uzi huu, tutakuwa tumeelimika juu ya matumizi ya "Commission from Hell" katika viunga vya kisheria.

Kwa mara nyingine asante sana.
 
Huyo Muuaji anajipa moyo anapo zungukwa na wakuu wa police, Usalama na JWTZ, hajui pale wana mchota akili tu. Usalama w Tz umekuwa ni kutrack watu na kuwaua, simple basic things they can do, wanafikiri kufanya hivyo ndo wataliponya Taifa au wata msaidia Muuaji wao that is totally wrong, njia sahihi ni kutoa haki sawa kwa watanzania na kuwaacha waamue wao wanachokitaka.

Kwa kuwa Muuaji upstairs kuna shida hashituki, I can tell u, Muuaji yuko 100% ya Kukamatwa na ICC, nampa pole kwa ujinga wake.
 
Back
Top Bottom