Tumeachana lakini huwa najisikia vibaya kuona anashida

Tumeachana lakini huwa najisikia vibaya kuona anashida

demisexual

Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
7
Reaction score
28
Ni mwanamke ambaye nimeishi nae zaidi ya miaka miwili lakini tulikuja kuachana kwa fujo sana kutokana na tabia alizo zianzisha na kusababisha kushuka sana kwa utendaji wangu wa kazi sababu nilikuwa bado namuhitaji lakini ndo ugomvi sana. Nikaamua kukubaliana na hali maana alikuwa kashapata mshikaji mwingine ambaye alisabibisha mimi na yeye tuachane japo ilinichukua mda kidogo sababu nilipata depression.

Niliamua kumtafuta na kumuambia kwamba tuongee kila mtu amsamehe mwenzake na kila mtu aendelee na maisha yake maana niliona chuki inaniumiza mwenyewe maana kila nikimuona nilikuwa natetemeka kwa hasira nikaamua kwenda mbali lakini stress zinazidi.

Baada ya kumtafuta kila mtu akaendelea na maisha yake japo hakuniomba msamaha wala nini ni mtu ambaye hawezi kusema nisamehe hata siku moja. Kuna siku akanipigia ananiomba nimu azime hela atanirejeshea nikaamua kumtumia kama nimetoa sadaka lakini nikaona tabia inazoe akanitafuta tena siku nyingine kaniambia anashida na hela kama laki nikagoma kumpa maana nikaona analeta mazoea akati anamtu wake japo najua anashida.

Mara nyingi huwa najisikia vibaya kuona anashida yoyote ata nikisikia kwamba nashida fulani huwa natamani nimsaidie au hata nimtafute nimjulie hali japo ni mwanamke aliniacha kwa zarau sana je anafaa kusaidiwa?.
 
Ni mwanamke ambaye nimeishi nae zaidi ya miaka miwili lakini tulikuja kuacha kwa fuja sana kutokana na tabia alizo zianzisha zake na kusababisha kushuka sana kwa utendaji wangu wa kazi sababu nilikuwa bado namuhitaji lakini ndo ugomvi sana. Nikaamua kukubaliana na hali maana alikuwa
Huna ndugu wa kuwasaidia? Vipi watoto yatima na watoto wenye ulemavu na magonjwa huoni wanapata shida zaidi ya huyo mwanamke?
 
Ni mwanamke ambaye nimeishi nae zaidi ya miaka miwili lakini tulikuja kuacha kwa fuja sana kutokana na tabia alizo zianzisha zake na kusababisha kushuka sana kwa utendaji wangu wa kazi sababu nilikuwa bado namuhitaji lakini ndo ugomvi sana. Nikaamua kukubaliana na hali maana alikuwa kashapata mshikaji mwingine ambaye alisabibisha mimi na yeye tuachane japo ilinichukua mda kidogo sababu nilipata depression,
Hafai piga moyo konde huyo anakuona bwege
 
Unaanzaje kumpa moyo wako mtoto wa mwenzio? Kwenye mapenzi wekeza kucha na nywele hata ukivikata vitaota Tena, lakini sio kuwekeza moyo my dear. Mijitu yenyewe hi haieleweki kabisa.

Pole kwa maumuvu, usiache kunsaidia huyo mlimbwende kwa kadiri uwezavyo.
 
Endelea kumsaidia,hata wanaume wengne hufanya hvyo pia
 
Kama huna mtoto nae unahangaika nae wa nini wakati alikuacha kwa dharau acha dunia imnyooshe vizuri usimpe hata mia yako
 
Hana wazazi, ndugu zake wanaowwza kumsaidia?

Au wewe ndio baba mlezi?
 
Back
Top Bottom