Tumeachana lakini huwa najisikia vibaya kuona anashida

Unatafuta kupigwa tukio mkuu ,mmeachana unageuza shingo ya Nini?.Mblock usiwasiliane nae tena.kitendo Cha kuwa na mawasiliano nae kosa, mwanamke anauwezo wa kushawishi mkubwa Sana.
 
Hiyo roho yako heri uwe mchungaji, huyo hata akiomba vocha mtumie sms ya tafadhali nipigie
 
Fanya yako acha ubwege. Unamsaidia vipi mtu aliyekudharau na wala hakuona umuhimu wa kukuomba samahani!?

 
Achana nae atakuongezea stress piga chini huyo jumla,, kupenda asiyekupenda ni risk taking achana nae kabisa mpe mkeo mpya ,, usiwe na huruma na kiumbe Kama hicho
 
Hivi watu hela za kuchezea hua mnazitolea wapi?
 
Ni sahihi bado una m-feel,lakini kama unakiri alikuacha kwa dharau jaribu kufikiri,
i.Vipi Kama mtu aliyenae atafahamu kuwa unamtumia pesa mwanamke wake ambae alikuwa ex wako?
ii.Inakuaje kama anakuchukulia,samahani(mtu fulani ivi boya)?
iii.Akitaka kurudi kwako uko tayari hata kama hujui atakuwa na lengo gani?
 
Amuombe bwana ake mpya
Sasa hivi hata kile ki infinix chake cha smart2 kimeharabika. Aliniomba mi nimwongezee akanunua kitecno cha batani. Kusema kweli hajui kusema nisamehe ila anashida. We msaidie tu mi huwa namsaidia kwa kuwa alishawahi kuwa rafiki wa aliyekuwa mpenzi wangu mwaka jana wa juzi

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Wacha kumsaidia dunia imfunze. Kwa nini kama ana maana asikutafute wakati wa raha ila anakutafuta wakati wa shida. Achana nae mzee unawalea watu ili watatue shida zao wakati wamekuacha kwa dharau na maumivu. Jinga kabisa
 
Mafala Ni wengi Sana duniani.

Haya bwana mtoa misaada

We endelea tu
 
Ulipewa LIMBWATWA sio bure!
 
Huna akili au unazo pesa za kuchezea.Mama etu ulimpa laki Mara ya mwisho lini ivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…