Meridah Tough
Senior Member
- Nov 27, 2017
- 136
- 365
Kwa kweli dunia ina mambo ya ajabu sana. Exboyfriend wangu ni Mchaga wa milimani. Tumedumu naye katika mahusiano kwa miaka zaidi ya mitano. Lakini katika muda huo kumekuwa na ups and down nyingi sana ambapo tukikaa tunarekebisha maisha yanaendelea.
Kwao natambulika ingawa si rasmi. Na swali la kwanza waliloniuliza kwao mimi ni kabila gani.
Wakaonyesha kunipokea na kunijali ingawa haikuwa utambulisho rasmi.
Baada ya miaka yote, nimegundua mwenzangu ameanzisha mahusiano na binti wa kichaga, yupo chuo mkoani.
Nikajaribu kuongea na mwenzangu ambaye aliniambia hayupo serious naye na ndio maana muda wote yupo na mimi na hawezi kuniacha hata itokee nini.
Baada ya siku chache tena mwenzangu akawa anaendeleza mahusiano hadi kupigiana simu zao mbele yangu.
Nilichokifanya ni kumlazimisha jamaa kuchagua jambo moja, mimi au Mchaga mwenzake wa huko chuo.
Mwenzangu alionyesha ugumu sana sana sana kuniacha ila pia kule kwa Mchaga mwenzake pia hataki kuacha.
Anachonieleza ni kuwa amenizoea, namjali, mimi ni part ya maisha yake, hivyo hataki niondoke ila wazazi wake wanataka apeleke mtu Mchaga na si kabila lingine.
Nimeamua kuondoka katika maisha yake ingawa mpaka sasa mwenzangu analeta ugumu sana katika kuchukua vitu vyangu nilivyoacha kwake. Ananidanganya na kunizungusha sana lakini kiukweli maisha anayotaka niyaishi, si maisha ninayoyataka.
Nimehuzunika tu kwa kuwa tumefika mwisho kwa sababu mimi si MCHAGA. Ubaguzi ambao Wachaga wengi wanao.
Nashukuru Mungu kwa kunipa pumzi hii hata nimeweza kulitoa dukuduku hili kwa ndugu zangu wana JF.
Pamoja na comment za kibabe ila kiukweli huwa ninafarijika sana ninaposhare na kukosolewa au kuonyeshwa njia sahihi.