Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Wanasema Yesu alizawaliwa paspo kukutana baba na Mama, yaan kutoka kwa bikira Maria, Je na mtume alizaliwaje?
Kwa nini unafunganisha hapa una lengo gani? maana hawa ni watu wa wili tofauti
 
Nimejaribu kuelewa andiko lako kwa kulisoma kwa umakini sijaelewa. Nichukulie mfano ambao umeutoa wa Yesu na Gautama (buddha). Nitatumia mfano rahisi wa Yesu mnazareti.

Biblia imeandika maisha, matendo, kifo na kufufuka kwake. Haya ni matendo yaliyotokea katika historia na kwa hiyo yanapaswa kupimwa usahihi wake kwa vyanzo vya karne ya kwanza na si vinginevyo. Tuna vitabu kwenye Biblia vimeandikwa ndani ya miaka 30. Na kitabu cha mwisho kimeandikwa mwishoni mwa karne ya kwanza.

Lakini tuna rekodi za wanahistoria wengine kama Tacitus, Pliny the younger, et al ambao wanaandika juu ya mtu huyu na kutupa taarifa za ziada juu yake.

Huyu ni mtu ambaye hakuwahi pigana vita walq kujenga himaya. Na ilikuwa ni karne ya 1. Kama hizi taarifa zipo basi karne ya 7 natarajia ziwepo zaidi.

Hata hivyo mambo yote kuhusu Muhammad rasul Allah tunayapata toka katika Quran, hadith na Sira. Ambazo compilation yake imekuja baadaye sana. Karne ya tisa na kuendelea.

Kwa standard ya kihistoria tunapaswa kurudi karne ya 7 na kupata majibu. So far nimejaribu kusoma na kusikiliza sijaona chanzo kinachoelezea Muhammad rasul Allah alikiwa ni nani na aliyoyafanya ni yapi na alisema nini. Ukiondoa Sira Hadith na Quran unabaki huna chochote juu yake.

Hivi vyote ulivyoandika ukiungqnisha hupati Muhammad wa kwenye Koran Sira na Hadith. Kama siko sawa unaweza nirekebisha.

Ninachojaribu kufanya ni kuona kama naweza kumpata rasul Allah nje ya Sira hadith na Quran, toka vyanzo vya karne ya 7. Ndio swali langu la mwanzo na ndio ninachotafiti binafsi
 
iv mbona sikuizi na nyie mmeanza kuvaa zile mikufu za wakatoliki ( tasibih ) au mmeiga rozari?? Na piah na nyinyi siku iz mna maji ya upako sijui mnayaita maji ya nn wenyew vile vile mnapiga mauno ( kaswida ) tofauti na mlivokuwa zaman??
 
iv mbona sikuizi na nyie mmeanza kuvaa zile mikufu za wakatoliki ( tasibih ) au mmeiga rozari?? Na piah na nyinyi siku iz mna maji ya upako sijui manayota maji ya nn wenyew vile vile mnapiga mauno ( kaswida ) tofauti na mlivokuwa zaman??
 
Swali lako limebadilika mwanzo ulisema unataka kujua ikiwa Muhammad (S.A.W) Ali exist au ni mtu kwenye vitabuni nimejibu kwa kukuletea baadhi mabaki na athaari zake alizo ziacha ndani yake nimekupa mabaki ya maandishi yaliyo mzungumzia ambayo hayapo kwenye sira au Hadith na hawakua waislamu.

Saiz unatakakuja alikuwa anafanya Nini na alikuwa mtu gani maana yake unataka kujua kama alikuwa mtume au lahh
 
Kwann mnatenda uovu kwa kisingizio cha dini.? Mnabaka, mnaua, mnateka.
Ahsante ndugu, khulka ya kutenda uwovu siyo khulka ya dini bali ni khulka ya mwanaadamu. Ametekwa Mo dewji, ametaka kuuliwa Tundu lisu, wanawake wengi wanabakwa nk. Havina mahusiano na dini bali khulka ya mwanaadamu.
 
Ahsante ndugu, khulka ya kutenda uwovu siyo khulka ya dini bali ni khulka ya mwanaadamu. Ametekwa Mo dewji, ametaka kuuliwa Tundu lisu, wanawake wengi wanabakwa nk. Havina mahusiano na dini bali khulka ya mwanaadamu.
Lakini wanaofanya hvy wanasema wanafanya hvy kwasababu hawataki elimu dunia wanataka Quran, hapo unasemaje.?
Mfano boko haram Nigeria.
 
Hakuna mwislamu anaye valia rozali shingoni, na kama yupo basi huyo sio miongoni mwetu hata kama atajinasibisha na uwislamu, Tasbih inaweza kushikwa mkononi na akivaliwa shingoni kwa nia ya kuibeba hakuna shida lakini ikiwa kwa nia ya mapambo bado ni mafundisho tofauti na dini, hayo ni matakwa ya watu binafsi nasio dini. Ni kama vile wapo wakristo akivalia kanzu na kofia
 
Lakini wanaofanya hvy wanasema wanafanya hvy kwasababu hawataki elimu dunia wanataka Quran, hapo unasemaje.?
Mfano boko haram Nigeria.
Ahsante ndugu, Boko haram ni kingudi cha kigaidi nasio cha kiisilamu, ni kikundi cha kigaidi chenye lengo la kuuchafua uwislamu.
 
Halijabadilika. Hebu niasidie katika hizi data ulizoleta, assuming ni 100% correct, zinaoneshaje kuwa Muhammad wa kwenye hadith na Sira na Quran aliwahi kuwepo? Mfano ukikuta maandiko yanasema "Mimi Ali Muhammad" hii inamaanisha ali yupi? Maana Ali Muhammad ni common name Arabia, anaweza kuwa mtu yeyote. Lazima taarifa iwe qualified kumfanya mtu awe specific. Hadith na Sira ziko so specific kiasi kwamba unaelewa wazi zinaongelea Muhamqqd yupi.

Data ulizoleta, bila kujali authenticity yake, haziko specific kujibu Swali Je Muhammad rasul Allah, na sio some vague Muhammad aliishi karne ya saba, alifanya aliyoyafanya, ikiwemo kueneza Uislam, kujenga Millitary empire ya Umah wa waislam na kuwa aliyashinda na kutawala maeneo tajwa na kuwa aliishi kwenye miji ya Mecca na Medina. Kuwa matukio kama Hijra et al yalitokea.

Hili ni swali langu toka mwanzo na halijabadilika, na sijapata mwanga ama majibu.
 
Ahsante ndugu
Kuna kitabu nimekupatia kimeandikwa na swahaba wa mtume jina lake anaitwa Ibn Abbas (619– 687), tofauti na hapo utakuwa umeshaufunga ubongo kwa kupokea vitu vipya kwasababu tayari unamajibu yako unayo yaamini kichwani.

Kwasababu kama alivyosema ndugu @Zacht huwezi kuthibitisha uwepo wa mtu wa karne zilizopita kutokana na kwamba hakuna mtu hata mmoja kwasasa ambaye aliishi nyakati hizo. Tofauti na hapo ni kutumia njia za kisayansi kama alivyoelezea. Katika karne yetu hii hakuna mtu hata mmoja alimuona Yesu vipi watu wanatoa na muvi show kwa kuonyesha sura yake kabisa na inawekwa kwenye rozali na watu wanaamini..? Nani aliwahi kumuona mama Maria? hadi anatengezewa sura yake na watu wanavaa shingoni? karne hiyo kulikuwa na kumbukumbu ya kuchukua picha? Unakuta ni vitu haviingii akilini kabisa.

Na kama mnavyodai kwamba Dini hii ilitengenezwa kwa story za kusikika na kuungaunga basi hao waliotunga wangeweza kuweka na picha za wahusika ili kunogesha kabisa, lakini leo huwezi pata picha ya mtume Muhammad (s.a.w) wala Swahaba wake yeyote wala watu waliokuja karne baadae. Lakini cha ajabu picha ya Mtume Muhammad (s.a.w) hakuna ila tunapicha ya Yesu.

Hakikisha kama unataka kuelewa usijipe majibu ya moja kwa moja kunako fikra zako, vyema kufungua akili na ukubali vitu vipya kisha ufanyie utafiti wako, kuliko kujifunga kabisa kwamba jambo hilo halipo. Tutakesha
 
siku ya kuzaliwa yesu sio realistic maana haijaandikwa popote ni kundi flani liliamua kuitenga tar 25/12 ,wangeweza kuitenga siku yoyote ile ila ya muhamad ni real
Kwa nini ya Muhamad iwe real ya Yesu iwe uongo chief? Unaweza kutupa maelezo kidogo ya hapo ili tuelewe u real na uongo uko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…