Tumechezwa shere! Ruzuku ya bilioni 100 kwenye mafuta ni changa la macho

Leo mafuta yamepanda bei maradufu wananchi tunaendelea kuisoma namba kama kawaida! siyo mafta tu bali mchele, unga vifaa vya ujenzi n.k vimepanda, kwa kweli wenye nacho huongezewa hapa mawaziri na watendaji was erikali wanakula kuku kwa mlija per diem zikitafunwa kila siku hakuna anayewaza kodi za miamala wala bidhaa kupanda.

Wakiwa na wananchi nikucheka tu hata kama watu wanazungumzia mambo mengine utasikia wanasifu na kuabudu kuwa Mma Samia anaupiga mwingi amefanya mapinduzi makubwa katika nchi.

Kwa mimi navyoona chombo kinaelekea kuzama kwani hizi kauli ya vita vya Urusi na ukraine wananchi hawatakubali kuisikia.
 
Na kwenye kila tatizo wao kwao ni fursa ya kupiga ndefu[emoji35][emoji34]
 
Mkuu Mshana ukipata muda tudadavulie maana na manufaa ya kila kodi. Yaani hata RAIA hawaelewi kabisa sijui margin levy. ILA NISEME TU WATANZANIA NI WAOGA NA WANAFIKI SANA. HAWA JAMAA TUNAJUA WANATUPIGAJE, TUNAJUA NI AKINA NANI? TUNAJUA WANAPATIKANA WAPI LAKINI HUWA TUNAISHIA KULALAMIKA TU MITANDAONI KISHA TUNAZOEA. HATA WAO WANATUJUA TUTAONGEA KWA MUDA TU WAO AF TUNAZOEA.
 
Nilikunukuu mshana unamsifia mama anaupiga mwingi kulikoni Leo wiki Moja imepita nilikuwa Nairobi Kenya mafuta kule ukigawa na Hela yetu ni 2750 watu wa namanga wanavuka Kenya na gari zao kununua mafuta
 
Hazina faida yoyote huo utitiri wa hizo taasisi zote unaopata hizo ruzuku unaweza kuzivunja zote na kutengeneza taasisi chache zenye matokeo chanya kwa kila jukumu
 
Nilikunukuu mshana unamsifia mama anaupiga mwingi kulikoni Leo wiki Moja imepita nilikuwa Nairobi Kenya mafuta kule ukigawa na Hela yetu ni 2750 watu wa namanga wanavuka Kenya na gari zao kununua mafuta
Ni kweli kabisa siwezi kukataa kabisa nilifanya vile kwa nyakati husika.. Na hata sasa bado ana nafasi ya kuweza kufanya tofauti na haya yanayoendelea..Lakini kama akikubali kuwa msikivu
 
Kwani kuna la maana alilofanya? Shida yenu ni kuhamisha hoja na kuileta kwa namna ya kusafisha mchafu wenu.
Mie muda mwingine nakaa kimya. Hata sisi si ndo tulishangilia sana baada ya mwendazake kufariki na tuliompinga mama tulionekana NI sukuma gang sasa makelele ya nini????

Goja atunyooshe ili sote tuitwe sukuma gang!
 
Wharfage = 20.6 Tshs/Lita

3. Ushuru wa Maendeleo ya Reli (1.5% CIF) = 17.4 Tshs/Lita.

4. Ada ya Uchakataji wa Forodha = 4.8 Tshs/Lita

5. Ada ya Vipimo na Vipimo (WMA) = 1.0 Tshs/Lita

6. Tozo ya TBS = 1.2 Tshs/Lita

7. Ada ya TASAC = 3.5 Tshs/Lita

8. Ada ya EWURA = 6.1 Tshs/Lita

9. Alama ya Mafuta = 14.1 Tshs/Lita

10. Gharama za Demurrage = 5.5 Tshs/Lita

11. Gharama ya Wakadiriaji = 0.18 Tshs/Lita

12. Gharama ya Ufadhili = 11.6 Tshs/Lita

13. Hasara za Uvukizi = 5.8 Tshs/Lita

14. Ushuru wa Mafuta = 413. Tshs
 
15. Ushuru wa Bidhaa = 379 Tshs/Lita

16. Ada ya Petroli = 100 Tshs/Lita

17. Oil Marketing Companies Overheads & Margins = 123 Tshs/Lita

18. Tozo Zinazolipwa kwa Wakala wa Utendaji = 1.0 Tshs/Lita

19. Ushuru wa Huduma Unaolipwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (Ushuru wa Halmashauri~ Jumla) = 5.7 Tshs/Lita

Jumla ya Bei Kikomo = Tshs/Lita 2275.

Kisha 1. Upeo wa Wafanyabiashara = 108 Tshs/Lita

2. Tozo zinazolipwa kwa Wakala wa Utendaji = 5.44 Tshs/Lita

3. Gharama za Usafiri (Ndani) = 10 Tshs/Lita

4. Ushuru wa Huduma unaolipwa kwa mamlaka za Serikali za Mitaa

Mchanganuo wote huu unaingia kwenye lita moja ya mafuta na mlipaji ni mwananchi wa kawaida
 
Hazina faida yoyote huo utitiri wa hizo taasisi zote unaopata hizo ruzuku unaweza kuzivunja zote na kutengeneza taasisi chache zenye matokeo chanya k
Mkuu kwa upande wako unashauri nini kifanyike ili huu utitiri wa kodi upunguzwe kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wake? Iwe zaidi ya maneno matupu
 
Mkuu kwa upande wako unashauri nini kifanyike ili huu utitiri wa kodi upunguzwe kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wake? Iwe zaidi ya maneno matupu
Hebu soma tena nilichoshauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…