Tumefikia huku? kwamba mzazi anapata taarifa ya kifo cha mtoto kwenye soshomedia?

Binafsi nimeisikiliza hiyo Interview ya Mzee Habash nimeumia...

Utandawazi imetufikisha sehemu taarifa za kifo cha mtoto wake mzazi anaziona kwenye mitandao ya kijamii[emoji24]
 
Mbona una mind vitu vidogo sana mkuu...
!!?🤷🤷
 
Inasikitisha sana. Ni kama kwa kibonde,kijana wake alipokea taarifa mtandaoni wakati huo alikua anaangalia mpira kibanda umiza,hajakaa sawa anaona taarifa ya mwili wa Baba yake kurudishwa dar akaona aende airport akahakikishe
 
Na wewe Mbona unatupa taarifa ya Baba yake Gadner kwenye sosho media??
 
Wengi wamekuwa malimbukeni wa mtandao, Kuna namna ya uwasilishaji wa taarifa kwa watu wa karibu na marehemu, Kama mzazi wake angekuwa na tatizo la pressure halafu unampa hizo habari unafikiri matokeo yangekuwaje
 
Tatizo ni kwamba Dunia imekuwa kama Kijiji, taarifa mbalimbali zinaenea kwa kasi sana, wale waliokuwa na mgonjwa baada ya kufariki ndiyo waliotakiwa kutoa taarifa kwa Baba yake labda kama kulikuwa hakuna Ndugu wakati anafariki.
 
Ulimwengu wa utandawazi hili halikwepeki na kwa mtu maarufu ndio taarifa zinaingia mitandaoni haraka sana. So hakuna cha ajabu hapo.
 
ajabu ni baba
Ulimwengu wa utandawazi hili halikwepeki na kwa mtu maarufu ndio taarifa zinaingia mitandaoni haraka sana. So hakuna cha ajabu hapo.
yako kupata taarifa za kifo chako kupitia mtandaoni.
 
Inaonekana ndugu zake wa karibu jasa wauguzaji hawajitambui, ni machoko wasio hata na ustaarabu wa kitamaduni, So sad.

Huo ni udharirishaji wa Marehem na watu wake wa maana kwenye Familia.
 
Umenikumbusha msiba wa Mzee komba! Kuna picha zilitumwa akiwa amelazwa kwenye meza Hosp muda mfupi baada ya kufariki huku uso ukionekana!...fikilia mwanafamilia anaona picha za hivyo...
 
Soshomidia?
Nahisi mjadala uanze kwenye hili neno
 
Ni tatizo.
nimetoka kumsikiliza mtoto wa marehemu CDF wa kenya,nayeye analalamika na blog vibungo,kwamba taarifa ya kwanza kuiona ni video ya helkopter ikiteketea kwa moto, na maelezo kwamba ilikuwa ni ya jeshi imebeba CDF.

Sheria ya matumizi ya mtandao inatakiwa kuboreshwa,watu wanatumia hata misibia kupta engagement,wala hawajali nini wanapost.
 
ajabu ni baba

yako kupata taarifa za kifo chako kupitia mtandaoni.
Inategemea imepita muda gani na baba yako ana tatizo gani. Watu hukubaliana wamwambie wakishakamilisha baadhi ya mambo na si kwa kukurupuka. Lakini penye wengi hapakosi wambea. Anatokea mmoja anamjulisha mtu wake wa karibu na baadae zinamfikia mhusika namba moja.

Kuna watu wamepata taarifa za vifo vya ndugu zao kupitia WhatsApp group au kupigiwa simu ya Pole. Sasa hivi mambo yanakwenda speed sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…