Tumefikia huku? kwamba mzazi anapata taarifa ya kifo cha mtoto kwenye soshomedia?

Tumefikia huku? kwamba mzazi anapata taarifa ya kifo cha mtoto kwenye soshomedia?

hufikirii kuwa hata hao ndugu walipata taarifa huko pia? kiini kipo kwa aliezitoa taarifa pale hosp alizipeleka wai
Mbona unalaumu kwa kufikirika tu?
We una uhakika hospitali hawakuwapa taarifa ndugu? Je, ndugu walimwambia baba?
 
Mmeamshwaje wakuu poleni na mvua zinazoendelea kutufikirisha.

Jana niliangalia interview ya Milad na baba wa Gadna nachelea kusema baba yule yupo kwenye mtikisiko na msikitiko mkubwa sana.

Kilichonifikirisha na kuniuma ni yeye kusema siku hiyo alimtafuta mwana akamkosa akaenda jumuiya akiwa hana raha kwa kumkosa mwana mbaye alitaka kumsomea neno kutoka kitabu kitakatifu. akapigiwa simu mbili ile ya pili ilikuwa ni pole direct kwamba "nimeona Gadna amefariki huko kwenye mitandao" can you imagine habari nzito inafika kwa mtu muhimu kwa njia nyepesi kabisa?!!.

Kwanini tumekuwa washamba na malimbukeni kiasi hiki maana ingekuwa ajali utasema mashuhuda walipost, ingekuaje kama baada ya kifo kutokea akatafutwa mtu wa familia akapewa muda kupeleka kwenye ngazi ya familia hii taarifa then ndo ipelekwe kazini?.

Ni nani alivujisha taarifa mitandaoni kabla ya watu muhimu ambae mmoja wapo kwa ukubwa ni mzazi? natamani kuwepo na mtu wa kuwajibishwa katika hili ili iwe mfano.

Tuliona mzee Zoro nae alipatia taarifa kutoka kwenye mitandao binti yake amefariki well angalau ilikua ajali mashuhuda walipostpost lakini bado sio sawa. Usiseme kuwa huo ni umaarufu na maisha yake hapana; Mfu anahitaji stara.
Swali la kwanza ambalo ulipaswa ujiulize lilikuwa ni;
Je,kipindi Gadna alipopelekwa hospital baba yake hakuwa na taarifa kuwa mwanae ni mgonjwa?

Km alijua,je alipozidiwa aliyekuwa akimuuguza alitoa taarifa kwa baba?

Je,kuugua na kulazwa kwa Gadna ilikuwa siri kiasi cha baba yake kutogahamu?

Kwani Gadna alifariki ghafla?
Kama aliugua,iweje baba yake asiwepo karibu?
 
Back
Top Bottom