Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Andika maneno ambayo meko aliyasema juu ya tundu lissu kisha rudi umetete.

Kubali kwamba meko amewagawa watanzania na kuwaambukiza roho mbaya.

Watumishi wa umma kwa kiwango kikubwa hawampendi mtukufu magufuli
 
Hapana hauko sahihi...wasiompenda ni wale walimuamin mpambavu yule...hakuna siku nimeona live chat nyingi sana za kumfurahia raisi kama leo pale youtube. Kwani raisi si binadam kama binadam wengine?? Kwani akiugua ni shida? Mungu aendelee kumlinda na kumpa afya njema!!
 
Hukujifunza lolote mbali na umbea
Mimi nimeng'amua uyu jiwe amechukiza watu kiasi kwamba wanamtamani afe hii sio dalili nzuri kwa Taifa.
Mfano Kikwete alipougua dushe akapelekwa Marekani wengi tulimwombea apone sasa uyu kwanini wengi wanataka afe?
Kumbuka uyu anayejiita jiwe sio jiwe ni binadamu kama mimi na wewe anaweza kuugua nakufa pia.

 
Nadhani mleta uzi ndiye ana matatizo, watz wanakuaje wajinga kujali afya ya mkuu wa nchi wao, hebu atuambie pia kuhusu ile clip ya Ruangwa na ukomo wa ziara kwann wananchi wasiwe na hofu. Sio kila jambo kimya ni suluhisho. Watanzania wengi tunaomjali Rais tuliishi kwa hofu kinyume na wewe usiyejali au uliyedokezwa kutoka Ikulu kuwa hakuna shida.
Kama hapakuwa na haja ya press release nadhani asubuhi hata Mh Rais leo angetokea kanisa, siku nzima ya speculation ni muda mrefu sana.
Kuna siku wananchi watapuuzia na kutojali matukio ya kweli. Kuna haja ya kujali wananchi ambao mioyo yao ina nia njema kinyume na wabezaji.
 
Nimejifunza kuwa kuna kundi la wapigaji ambalo lamwombea JPM mabaya ili turudi zama za kupiga
 
Mkuu mbona una conclude kwamba Rais ni mgonjwa, umejuaje? Kigogo kadanganya watu hadi kufikia kutaja chumba ambacho ati Mh Rais alilazwa huko Ujeremani! Bado unasema Kigogo siyo muongo kwa 100%!! Ajabu
Kigogo anaishi na kufanya kazi ikulu ya magogoni, na wewe upo Magomeni, sasa wapi na wapi?
 
No. 2 kwa hiyo tuamini kwamba kina Seth Rugema na hao wengineo walikuwa wakifisidi nchi kwa baraka za upinzani na si chama twawala?
 
Wanaomuombea mabaya rais ni wapinga dili, vyeti feki, waliotumbuliwa pamoja na rafiki zao ambao walikiwa wanapata za bure
 
No. 2 kwa hiyo tuamini kwamba kina Seth Rugema na hao wengineo walikuwa wakifisidi nchi kwa baraka za upinzani na si chama twawala?
Point yangu ya pili haimaniishi CCM haina mapungufu, Yes CCM ina Mapungufu yake Je hawa ambao ni mbadala wa CCM vitendo vyao vinatuthibitishia kuwa wapo tayari kuwa mbadala wa CCM? Wanasema heri zimwi likujualo kuliko lisokujua huu msemo ndo huwa tunautumia tunapopiga kura tu
 
Nenda YouTube leo wakati anaapisha viongozi uone live chart zaidi ya 10k walichangia positively ni record ya mwaka! Usihangaike na hawa wa tweeter na JF mawakala wa mafisadi.
Binafsi nimefurahi kumuona leo, nimeona kuna ujumbe Ikulu nzima ilikua inautuma kwa wananchi haswa wale wambeya, mfano kitendo cha uwepo wa viongozi wa dini, chakula cha pamoja vyote vilikua na meseji fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…