Kuzushiwa kifo si jambo dogo kwa kiongozi wa nchi tena kwa muda wa siku mbili mfululizo wananchi kubaki katika sintofahamu.
Hilo ni moja zaidi yake ni reaction ya watu hasa katika mitandao ya kijamii ambayo ni representative ya wale wasio kuwa nayo mizani kuelekea upande wa wale waliofurahia sana habari hiyo.
Kama Rais akipata wasaa wa kuona mitizamo ya watu kuhusiana na kifo chake, basi tutegemee hasa kuona mabadiliko makubwa katika kauli zake na matendo yake. Kauli za kibabe, kebehi, sipangiwi na mtu, acha kiherehere, Mimi Rais wa wanyonge tutegemee kupungua kwa kiasi kikubwa.
Atakuwa ameona ana kikundi cha watu wachache sana wanaomshangilia na kumpigia makofi kinafiki huku kundi kubwa likiwa linavuja machozi ya damu na hawa ndiyo wanyonge. Kundi hili ndilo lilikuwa linasubiria breaking news ya msiba wa taifa.
Kwa sasa atakuwa anajitafakari sana idadi ya watu isiyomtakia mema hivyo kuangalia approach mpya katika uongozi wake. Huna namna utauona ufalme wa mbingu huku watu ulioukuwa ukiwaongoza wanasherehekea kifo chako.