Pole,umeumia sana.Nimejifunza kwamba utamaduni wa Watanzania kumstahi rais na kumuheshimu sana, siyo tu unaisha, bali unaelekea kwenye utamaduni wa ajabu wa kumtakia mtu, tena rais, kifo.
Hii ni tabia mbaya kwa upande wa wananchi wenye mawazo hayo.
Lakini tabia mbaya hii imepaliliwa na kutiliwa mbolea na ubabe wa rais Magufuli.
Watu waliwakejeli Kikwete na Mwinyi kwa udhaifu wao, lakini haikufikia watu wengi hivi kusheherekea uvumi wa kifo cha rais.
Siasa za chuki hazina mshindi ni hatari hata kwake apandacho MTU ndicho atakachovuna soma historiaWe jinga sana yaani wa kuunganishwa ni hawa wapuuzi chadema?? Namuomba awakanyage kwelikweli
Umejuaje kwamba ni CHADEMA tu na si Watanzania wengine?Usiseme watanzania, bali sema chadema na magenge mengine toka upinzani kama kina Zitto
Akishawanyoosha then? Unajua visababishi vya heart attack,usiruhusu moyo wako ubebe chuki,visasi,hasira malipizi utauumiza moyo wako unaujaza mazito yapelekeao heart failure then kifo cha ghafla.MTU akikuchukia akikunyoosha anaeathirika zaidi ni yeye na sio wwe unayefanyiziwa.Namuombea Maghufuli akaze zaidi , huyo jamaa namwelewa Sana japo somtyme anakera, Kwa sasa anaenda kuwanyoosha wote, mwamba huwa hakopeshi yule ....
Mitandaoni humu kuna wahuni wachache tuu hao ni kama chura hawawezi kumzuia tembo kunywa maji, twende na JPM mpak 2025 non stop
I am beyond good and evil ina Nietzschean way.Pole,umeumia sana.
Acheni propaganda za linings hapa, kama wananchi hawampendi si tutaona kwenye uchaguzi,Ndugu Rais, bila shaka umeusoma upepo ulivyo kwa sasa..
Ni vizuri, uachane sasa na roho mbaya, kiburi, majivuno, na visasi. Nadhani umejifunza ni namna gani Wananchi wako wengi wanavyokutakia mabaya (kifo), na wapo tayari kufanya sherehe muda wowote iwapo mauti yatakufikia. Iwapo utachagua kuendelea na ubabe, uonevu na kiburi shauri yako.
I am very sorry for youZitto, Lema na Fatuma karume
ukijifanya wewe ni first class citizen lazima uwe diktetaMimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!
Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.
Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.
Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii.
Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.
Kitu kingine nilichojifunza baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu!
Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.
Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.
Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
Mkuu;Kwahiyo wale professional doctors aliokuwa nao hawana akili ila wewe ndio unataka kuwa mshauri wa madaktari wake...