Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii.

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu!

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
my bro who told you that top oppostion figures never knew where magufuli is, was? mind you this is politics, i fully beleive they knew everything, and aslo magufuli is sick, thats a fact, follow what he has been saying as he moves around the country, and another major thing to remeber is this-------politics is a mind game, who knows if these opposition figures just pretened to buy the narrative, yet they all along knew the truth???????? this is politics bro, barikiwa sana lakini
 
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii.

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu!

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
Nilichogundua tu ni wanaCCM woote walikaa wakanywea wasijue la kufanya, mbwembwe zote zikawashuka.

Hahahaaaa
 
Tuwe wakwelii tu kuwa kudorora kwa afya ya Rais haukuwa uvumi ; ni kweli Afya iliyumba na ziara kukatishwa ; sio Jambo la Ajabu mwanadamu kuugua
Tatizo ni namna Taifa lilivyopokea katika hali inaonyesha umoja wa kitaifa umekufa

Kimsingi huwezi kusema 100%!kuwa Kigogo ni muongo
Rais ni Mgonjwa na hata leo hakua kwenye ubora wake
Ni bora azingatie muda wa kupumzika

Ndio mkaamua kumzuahia kufa? Tena kuwa kafia Ujerumani???? Mbona Kikwete aliwahi kuanguka tena sio mara moja. Kipi cha ajabu. Tabia ya kuzusha kifo kwa mtu ni mbaya sana.

Queen Esther
 
Mm nimejifunza kwamba wapinzani wa Tanzania ni wapumbavu tu...

Na kwa hatua hii hakuna mbadala wa CCM
Kama CCM ni wajanja Mbona wamezuia mikutano wa siasa kutwa kuwabambikia kesi wapinzani
 
Nenda YouTube leo wakati anaapisha viongozi uone live chart zaidi ya 10k walichangia positively ni record ya mwaka! Usihangaike na hawa wa tweeter na JF mawakala wa mafisadi.
Unajitia moyo tu, level chart za Youtube ni za watu waliotemgenezwa na account mbali.mbali na waandamizi wa MATAGA. Utaona comment zao ni zile zile, maneno yale yale muundo ile ule.utadhani ni mfumo flani hivi wa robotic responses.

hahahahhaaaa

Mjifunze mbona mlikuwa wapole, eti tumwombee, eti tuwe na utu. Hahahaaa mlipomlipua Tundu Lissi hamkujua kama kuna utu?
 
Huo umoja wa kitaifa kuyumba sababu ya tweets za akina Zitto mzee? Yaani kakikundi ambacho tunajua hadi fake IDs zao ndio unasema taifa? Unajua mliheshimika sana kiasi kwamba sasa significant number imeanza kujua motives zenu!
Kaangalie like na comments wakati wa uapishaji Ikulu ujue Rais Magufuli anapendwa.

Queen Esther
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
Hata mm sio mwana CCM nilinywea
Wanaccm kimyaaaa......kumbe ni wepesi kama karatasi, Wao kaumwa tu kidogo wanatetemeka sisi majembe yetu yametekwa yameteswa na mengine kuuawa na bado tunaendelea na mapambano, wapuuzi sana.
 
Uko sahihi,kwa upinzani wa style hii hatustahili kuwa na upinzani...

Yupo sahihi kivipi kwani wapinzani pekee ndiyo wameshangaa kujificha kwake? CCM wengi walikuwa busy kupotosha haya na yale kumbuka upinzani hawapo huru kufanya siasa na kama wangekuwa huru wangeitisha mkutano na kuelezea kila kitu
 
Awali ya yote napenda kuipongeza serikali jinsi inavyoweza sasa kudhibiti taarifa zake nyeti, na kuwafanya wale wazushi, waongo, na wazandiki kuumbuka kweupe

Hakika idara sasa ina watu weeledi, na wanafanya kazi. Watu wameingi chaka vibaya mno.

Hao mbumbumbu akina kigogo wameumbuka vibaya mno. Wapinzani ndani ya nchi hii wamekumbwa na ugonjwa wa ajabu kweli kweli.

Ugonjwa wa kuzusha, kujitekenya na kucheka wenyewe, walianza kutuaminisha taarifa za ajabu kuhusu Rais tena wakishinikiza ikulu itoe taarifa kwa uongo wanaoeneza wenyewe.

Upinzani umekosa watu wa kujenga mawazo mbadala, watu wa kukosoa kwa hoja Leo wamegeuka waganga kutabiri vifo. Ona sasa taarifa wanazozusha zinawaumbua wenyewe, ni mwananchi gani atawaamini?

Mbona wanaweza kutumia mitandao kujenga hoja, kwanini wameingia kwenye uongo na uzushi?

Je, wamekata tamaa?

Kwa mtindo huu uchaguzi ujao unaweza kuwa kaburi la so called upinzani.

Muda utasema
 
Mshana Jr

unautaalamu mwingi ulio zaidi ya hili pengine unaweza kutupia JF, hiki kitu kwa ubobezi wa masuala nje ya teknolojia inaweza kuwa kazi za wazee wetu wa jadi. Chini ya anga hii huwa hakuna jibu la mwisho, chochote kinawezekana kuwa sahihi.
Kila wakati huwa nawaeleza kuwa Mshana Jr ni mpuuzi anayetafuta K za akina Demiss tu. Mnam overlate tu masikini.
 
Mkuu;
Kumbuka nchi yetu bado ni changa kwenye masuala ya mitandao na kwa sababu hiyo wanachi wengi wanaamini kila wanachokisoma kwenye mitandao.
CCM wenyewe kwa wenyewe hawakuwa na taarifa zaidi ya kuhaha kutengeneza propaganda mbalimbali
 
1.Watu wengi tena waliosoma bado wanaamini tatizo linaweza kutatuliwa kwa kumtakia mtu jambo baya, hatufahamu dhana ya kuwa sisi ndio nahodha wa maisha yetu na maisha tunayoyaishi ni uamuzi wa machaguo tuliyochagua na sio bahati nasibu wala mtu mwengine kusababisha tuwe tulivyo.

2.Upinzani bado hawajakua, bado hawajawa mbadala wa CCM, Wengi wanamchukia Magufuli kwasababu ya kuminywa mirija yao na sio wana uchungu na Watanzania.

3.Serikali imefanya jambo lililosahihi, kwa wakati sahihi katika namna sahihi kabisa.

4.Inawezekana kukawa na mageuzi makubwa ya vyombo vyetu vya usalama na ile mianya ya kuvuja kwa siri ambazo wengine hatupaswi kujua imeanza kuminywa kimya kimya, watu wenye kazi zao wapo kazini.

5.Watanzania tunapenda sana umbeya na Majungu, zamani tulikaa katika vijiwe vijiwe sasa hivi Teknolojia imeturahisishia kuendeleza tabia zetu za umbeya na Majungu.
Nakubaliana na wewe kwenye suala la umbeya na majungu. Siku hizi wanaita ubuyu.

Kibaya zaidi, watu wanaamini ubuyu zaidi ya ukweli!
 
Tuwe wakwelii tu kuwa kudorora kwa afya ya Rais haukuwa uvumi ; ni kweli Afya iliyumba na ziara kukatishwa ; sio Jambo la Ajabu mwanadamu kuugua
Tatizo ni namna Taifa lilivyopokea katika hali inaonyesha umoja wa kitaifa umekufa

Kimsingi huwezi kusema 100%!kuwa Kigogo ni muongo
Rais ni Mgonjwa na hata leo hakua kwenye ubora wake
Ni bora azingatie muda wa kupumzika
Kigogo alisema Rais kasafirishwa Ujerumani huku wakichagiza kuwa "kafa"
 
Ndio mkaamua kumzuahia kufa? Tena kuwa kafia Ujerumani???? Mbona Kikwete aliwahi kuanguka tena sio mara moja. Kipi cha ajabu. Tabia ya kuzusha kifo kwa mtu ni mbaya sana.

Queen Esther
Afadhali ya kuzushia kifo kuliko ya kupanga
na kushiriki njama ili kuwaua watu flani kisa, wana Sera bora mbadala kuliko za kwake
 
Back
Top Bottom