Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Kwa tuliokuwa tukijadili afya ya Rais basi mimi ni mmoja wao ninaamini na itakuwa hivyo kuwa Rais hakuwa katika afya yake iliyozoeleka. Na hata ukimuona leo ni bado hakuwa vizuri.

Nimeona video akisalimiana na katibu mkuu kiongozi ndugu Kijazi kwakweli inaonekana kabisa ndugu Kijazi kama ananena mambo fulani hivi. Kwanza inaonekana hawakuwa pamoja kwa muda fulani.

Any way tushukuriwe sisi ambao tuliweza kujiongeza na kuulizia kuhusu afya ya Rais. Tulikuwa na wajibu huo na tutaendelea hivyo kwa kila litakapotokea jambo lisilo la kawaida.
Rungu la Mbowe linakusubiri hapo Ufipa!
 
Mkuu;
Huwezi kusema CHADEMA wote ni wapumbavu!

Ninadhani ni baadhi ya wanaCHADEMA.

Sasa Hapo ndio mgawanyiko unapoanzia ukisema Chadema wajinga kushabikia matatizo ya kiafya ya Rais tambua kuwa pia wapo wana ccm walikua wanachekea Chooni tena hao ndio Wanga kabisa wanaomtakia mabaya Rais wetu na anakula nao
Tambua kuwa wanaoumia na hatua Kali za Rais ni wana ccm waliokuwa wanafaidika na ufisadi kuliko hao Chadema Kwa sababu wao hawajawahi kunusa utamu wa ufisadi SERIKALI

Chadema pia wana hoja kuwa ccm walishamgilia matatizo ya TUNDU LISU na hata kushangilia anyimwe matibabu

Kimsingi pande zote mbili zimekosea na ni muhimu kuzika tofauti na kukubaliana kuishi kwa msingi ya Utanzania na sio kuendeleza chuki
Wote tumeona tumefikia mahali pabaya Sana
 
Hatuna la kujifunza watanzania tumeshazoea haya mambo.kama lissu alipigwa risasi mpaka leo serikali haina majibu, viongozi tuliowachagua wenyewe kwa utashi wetu wanahamia ccm unataka tujifunze nini katika uzushi huu kama kwenye matukio haya ya uhalisia hatukujifunza kitu?
 
Vicky Emmanuel Nchimbi wrote this piece [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Taarifa zinazosambazwa kuwa JPM amefariki si za kweli. Ni uzushi Zipuuzeni. May be if he will die in future on God's will, but as for now he is alive. It's true alipata heart attack akiwa ziarani kusini na kukimbizwa Dar usiku kwa helcopter ya jeshi kisha akasafirishwa to SA then Germany. Mama Samia aliitisha cabinet jana to adress the situation and all security organs are alerted.

Taarifa rasmi haijatolewa kwa sababu ya kuhofia kuiweka nchi kwenye tention unnecessarily. Kwa hiyo ili kupunguza minong'ono iliyopo imebidi itolewe taarifa ya uteuzi aliofanya kabla hajaugua. Ni idea iliyotolewa na Mzee Lukuvi just to calm people down. Ndio maana watu wanahoji if he is okay kwanini asijitokeze hadharani hata kwenda kununua samaki kule ferry as he used to be? uteuzi haujafanywa leo, isipokuwa leo umetangazwa tu. And the one who announced is Gerson not JPM.

Kutumia uteuzi as derteminant that he is okay is wrong. He is not okay and he is not in the country. Ndio maana hata kwenye mkutano wa AALCO he will be represented by mama Samia. Lets pray for him for the quick recovery. I'm told leo kapata nafuu na kaweza kufungua macho usiku huu. These are good news lets keep push the prayers. Hata kina Bashe na Polepole wamepata ujasiri to speak it out baada ya mzee kufungua macho usiku huu. Lakini tangu juzi alipozidiwa they were quet as absent b'se they couldnt anticipate what nature could provide.

The most important thing let's keep praying for him, and send our gratitude to Germans kwa kupambania afya ya baba yetu. Tusimuombee mabaya just b'se of political dissimilarities. Our prayers, our unity, our nation, our President.
Tatizo mnajifanya kujua mno humu mitandaoni.. Mmewashika akili wapumbavu kuamini vijineno vyenu. Mnaumbuka taratibu, tumieni vidole vyenu wisely kutafuta comments na likes kwa njia hizo mtapotea
 
Tatizo matendo yao yanawahukumu, ndio maana wanakosa pa kuanzia, hivyo the only solution wanayoiona wao ni kukaa kimya wakiamini kuwa tatizo litajitafutia ufumbuzi lenyewe.
 
Nimejifunza kuwa Rais huyu ni kipenzi cha watanzania maana wakati wa kuapisha viongozi hao watatu viewers walikuwa 1M na comments zote zilikuwa positive na walionyesha mapenzi makubwa kwa kiongozi wao mkuu wa nchi
 
Huo umoja wa kitaifa kuyumba sababu ya tweets za akina Zitto mzee? Yaani kakikundi ambacho tunajua hadi fake IDs zao ndio unasema taifa? Unajua mliheshimika sana kiasi kwamba sasa significant number imeanza kujua motives zenu!
Wamejishushia heshima sana, tena katika wakati mbaya sana. wasubiri majibu ya kazi yao 2020
 
Magafuli anatakiwa kujifunza kuwa humble na binadamu wenzake. Ukiona binadamu wenzako wanakuombea kifo ujue kuna mahali unawakwaza.

Kuwa humble na binadamu wenzako haimaanishi kwamba usitekeleza majukumu yako kama Raisi.

Mi nadhani aisikilize ile hotuba ya Kikwete vizur kuna kitu atajifunza.
 
Mkuu mbona una conclude kwamba Rais ni mgonjwa, umejuaje? Kigogo kadanganya watu hadi kufikia kutaja chumba ambacho ati Mh Rais alilazwa huko Ujeremani! Bado unasema Kigogo siyo muongo kwa 100%!! Ajabu

Sija conclude moja kwa moja ila nimelenga kusema KUUGUA ITS NOT A BIG DEAL YEYE NI MWANADAMU haikutakiwa kuuwa jambo la kushangilia
Mimi mambo ya kigogo sitaki kusikia ila tuangalie tu impact ya kuporomoka kwa utaifa
 
Me i fully eleive that magufulis health is not RIGHT NEITHER IS IT OKAY, infact if you follow very carefully what he has been saying when going around the country you will discover that his MENTAL STATE IS UNSTABLE. have you heard what he has been talking at those places, times sacking people simply coz they are not in his convoy (like takukuru boss of mtwara, without first finding out if this boss is either sick or) telling a certain water engineer do you want this people to drink your urine? telling a certain woman who asked for water that she should go and request water from her husband, the list is endless, truth be told, MAGUFULI IS SICK BOTH MENTALLY AND HEALTH WISE PERIOD, i support those who share my views,
 
Huo umoja wa kitaifa kuyumba sababu ya tweets za akina Zitto mzee? Yaani kakikundi ambacho tunajua hadi fake IDs zao ndio unasema taifa? Unajua mliheshimika sana kiasi kwamba sasa significant number imeanza kujua motives zenu!

Do you include me in that ; am not a politician and I will never be one
Simply all sides ccm na Chadema have their part of blame
 
1.Watu wengi tena waliosoma bado wanaamini tatizo linaweza kutatuliwa kwa kumtakia mtu jambo baya, dhana ya kuwa sisi ndio nahodha wa maisha yetu na maisha tunayoyaishi ni uamuzi wa machaguo tuliyochaguo na sio bahati nasibu wala mtu mwengine kusababisha tuwe tulivyo.

2.Upinzani bado hawajakua, bado hawajawa mbadala wa CCM, Wengi wanamchukia Magufuli kwasababu ya kuminywa mirija yao na sio wana uchungu na Watanzania.

3.Serikali imefanya jambo lililosahihi, kwa wakati sahihi katika namna sahihi kabisa.

4.Inawezekana kukawa na mageuzi makubwa ya vyombo vyetu vya usalama na ile mianya ya kuvuja kwa siri ambazo wengine hatupaswi kujua imeanza kuminywa kimya kimya, watu wenye kazi zao wapo kazini.

5.Watanzania tunapenda sana umbeya na Majungu, zamani tulikaa katika vijiwe vijiwe sasa hivi Teknolojia imeturahisishia kuendeleza tabia zetu za umbeya na Majungu.
mkuu pls ongea ukweli, zote tunajua hali ya tz, taifa liko katika janga kubwa, kisiasa, kiuchumi na hata kielimu, magufuli is EVIL
 
Afu wameaibika sana !
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii.

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake!

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
 
Back
Top Bottom