Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Akishawanyoosha then? Unajua visababishi vya heart attack,usiruhusu moyo wako ubebe chuki,visasi,hasira malipizi utauumiza moyo wako unaujaza mazito yapelekeao heart failure then kifo cha ghafla.MTU akikuchukia akikunyoosha anaeathirika zaidi ni yeye na sio wwe unayefanyiziwa.
Acha ramli wewe mchawi wa Luangwa , wasukuma hatuwangiwi kizembe hvyo
 
Nenda YouTube leo wakati anaapisha viongozi uone live chart zaidi ya 10k walichangia positively ni record ya mwaka! Usihangaike na hawa wa tweeter na JF mawakala wa mafisadi.
leo hakuwa live Tbc kumbe?
 
Katika hili la afya ya mkuu, kama taifa na serikali ya awamu ya tano imepata somo kubwa katika nyanja nyingi. Asante Kigogo na wengine mmefungua hisia na utashi wa tembo. Mwenye macho na aone.
 
Wapinzani wa Tanzania ni wadudu tu
Mkuu;
Hii sio lugha nzuri kuitumia kwa binadamu mwenzako.

Tupingane tu kwa nguvu za hoja na sio kuitana majina ya ajabu ajabu!

Ni ushauri tu, samahani kama nimekukwaza!
 
Huo umoja wa kitaifa kuyumba sababu ya tweets za akina Zitto mzee? Yaani kakikundi ambacho tunajua hadi fake IDs zao ndio unasema taifa? Unajua mliheshimika sana kiasi kwamba sasa significant number imeanza kujua motives zenu!
mimi siyo chadema wala ccm ila nilinunua beberu nisherehekea kufa kwa mtesi wa Lissu
 
Vicky Emmanuel Nchimbi wrote this piece [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Taarifa zinazosambazwa kuwa JPM amefariki si za kweli. Ni uzushi Zipuuzeni. May be if he will die in future on God's will, but as for now he is alive. It's true alipata heart attack akiwa ziarani kusini na kukimbizwa Dar usiku kwa helcopter ya jeshi kisha akasafirishwa to SA then Germany. Mama Samia aliitisha cabinet jana to adress the situation and all security organs are alerted.

Taarifa rasmi haijatolewa kwa sababu ya kuhofia kuiweka nchi kwenye tention unnecessarily. Kwa hiyo ili kupunguza minong'ono iliyopo imebidi itolewe taarifa ya uteuzi aliofanya kabla hajaugua. Ni idea iliyotolewa na Mzee Lukuvi just to calm people down. Ndio maana watu wanahoji if he is okay kwanini asijitokeze hadharani hata kwenda kununua samaki kule ferry as he used to be? uteuzi haujafanywa leo, isipokuwa leo umetangazwa tu. And the one who announced is Gerson not JPM.

Kutumia uteuzi as derteminant that he is okay is wrong. He is not okay and he is not in the country. Ndio maana hata kwenye mkutano wa AALCO he will be represented by mama Samia. Lets pray for him for the quick recovery. I'm told leo kapata nafuu na kaweza kufungua macho usiku huu. These are good news lets keep push the prayers. Hata kina Bashe na Polepole wamepata ujasiri to speak it out baada ya mzee kufungua macho usiku huu. Lakini tangu juzi alipozidiwa they were quet as absent b'se they couldnt anticipate what nature could provide.

The most important thing let's keep praying for him, and send our gratitude to Germans kwa kupambania afya ya baba yetu. Tusimuombee mabaya just b'se of political dissimilarities. Our prayers, our unity, our nation, our President.
Mkuu;
Hili andiko lako chanzo ni wapi? Facebook au Instagram?
 
Hawezi jifunza zaidi atawafanyia mbaya wale wote waliofurahia
 
Hivi msipende kuangalia juu juu mambo ya msingi.
Uvumi huu ulikuwa na baraka zote za Ikulu kwa maana hata baadhi ya viongozi wa juu ndani ya serikali hawakuwa na uhakika mzee yupo au hayupo? Mgonjwa sana au kidogo?
Na kama unataka kujiuliza zaidi nini kipo kwa viongozi wa juu ndani ya serikali na viongozi wa vyombo vya dola tazama tena kwa makini sana video ya shughuli ya kuapishwa Leo kwa hatua utagundua jambo moja LA hatari sana katika nyuso zao, WALITEGEMEA UVUMI HUU KUWA KWELI.
Sio rahisi kukubali lakini huo ndio ukweli, na ni ukweli wa kutisha sana. Kuna kukubalika mdomoni lakini sio moyoni na tusidanganyike tabia zibadilike.
100% naunga hoja hii niliwaza hivi hivi
 
Ombwe la wadudu wasiozidi 1000000. kumbuka tuko zaidi ya milioni 30 wenye akili nziri. Ukiondoa hao wadusu tuliobaki wote tuko vizuri.
Je uliangalia you tube mubashara comment za kushangilia zilivyokuwa zinaporomoka kwa maelfu??
Ndugu Rais, bila shaka umeusoma upepo ulivyo kwa sasa..
Ni vizuri, uachane sasa na roho mbaya, kiburi, majivuno, na visasi. Nadhani umejifunza ni namna gani Wananchi wako wengi wanavyokutakia mabaya (kifo), na wapo tayari kufanya sherehe muda wowote iwapo mauti yatakufikia. Iwapo utachagua kuendelea na ubabe, uonevu na kiburi shauri yako.
 
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii.

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu!

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
Katika sakata lote hili la siku mbili tatu, nimegundua mambo mawili matatu.

La Kwanza: RAISI wetu alikuwa anaumwa kweli na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kama sijakosea imetuficha for which reason i don't know but it was stupid idea. Kwanini nikasema stupid Idea kwasababu imezalisha taharuki na maombezi mabaya Nchini mwetu. Na sio hivyo tu kisheria wananchi ni haki yetu kuambiwa kweli.
La Pili: Tanzania imeingiliwa na chuki mbaya sana. Na hili limeanza tangu wakati wa Tundu Lisu kabla na baada kupigwa risasi. wakati Tundu Lisu wafuasi wengi wa CCM walikuwa wakimuombea mabaya na hata kufa baada ya kupigwa risasi, na yote ni chuki. Na sasa tumeaona kwa vijana waliokuwa wamechukizwa na alivyofanyiwa Tundu Lisu na kuanza kuiga tabia mbovu na kumzulia kufa kwa RAISI wetu.
La Tatu: Always don't show your weakness, Ikulu leo wametuonesha weakness yao. Walikuwa wameuachie apumzike RAISI wetu. huyo aliemshauri ajitokeze leo hafai kuwa mshauri wake. Kuumwa sio jambo baya.
Pumzika na ugua pole RAISI wetu
 
Ndugu Rais, bila shaka umeusoma upepo ulivyo kwa sasa..
Ni vizuri, uachane sasa na roho mbaya, kiburi, majivuno, na visasi. Nadhani umejifunza ni namna gani Wananchi wako wengi wanavyokutakia mabaya (kifo), na wapo tayari kufanya sherehe muda wowote iwapo mauti yatakufikia. Iwapo utachagua kuendelea na ubabe, uonevu na kiburi shauri yako.
Huyu jamaa ubabe wake na utemi ni too much......

Hivi sasa hapa TZ, huwezi kujua ile kitu inayoitwa "separation of power" miongoni ya mihimili mitatu mikuu, ambayo ni Bunge, mahakama na serikali, ambapo inatakiwa ifanye kazi zake ikiwa huru kabisa, katika kile kinachoitwa "check and balance"​
Badala yake katika nchi hii kila atakachokisema Rais kwenye majukwaa ya kisiasa, yanachukuliwa kama sheria!​
 
Magufuli kuna mambo anafanya vizuri ila kuna mambo mengi pia anavuruga kwa kutokubali ushauri .

Abadilike aache kuongoza nchi kwa matakwa yake binafsi Urais ni taasisi.
 
Katika sakata lote hili la siku mbili tatu, nimegundua mambo mawili matatu.

La Kwanza: RAISI wetu alikuwa anaumwa kweli na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kama sijakosea imetuficha for which reason i don't know but it was stupid idea. Kwanini nikasema stupid Idea kwasababu imezalisha taharuki na maombezi mabaya Nchini mwetu. Na sio hivyo tu kisheria wananchi ni haki yetu kuambiwa kweli.
La Pili: Tanzania imeingiliwa na chuki mbaya sana. Na hili limeanza tangu wakati wa Tundu Lisu kabla na baada kupigwa risasi. wakati Tundu Lisu wafuasi wengi wa CCM walikuwa wakimuombea mabaya na hata kufa baada ya kupigwa risasi, na yote ni chuki. Na sasa tumeaona kwa vijana waliokuwa wamechukizwa na alivyofanyiwa Tundu Lisu na kuanza kuiga tabia mbovu na kumzulia kufa kwa RAISI wetu.
La Tatu: Always don't show your weakness, Ikulu leo wametuonesha weakness yao. Walikuwa wameuachie apumzike RAISI wetu. huyo aliemshauri ajitokeze leo hafai kuwa mshauri wake. Kuumwa sio jambo baya.
Pumzika na ugua pole RAISI wetu
Aliyewaita nyumb hakukosea kabisa!
 
Ila somo amelipata, time will tell kwan ataishi milele? Anawatesa sana watu. Mseminari mwenzangu, tumesali Rozari, Novena na Antifona ila mimi zimenisaidia sana kuwa na huruma kuliko huyu anayejifanya Mkuu wa malaika.
 
Umejuaje kwamba ni CHADEMA tu na si Watanzania wengine?

Na, CHADEMA si Watanzania?
Chadema ni wajinga flani sijui ni kutoka nchi gani..

Sasa mtu unakuwa mfuasi mfano wa Zitto au Lema au Fatuma Karume ambao na usomi wao wanashikiwa akili na kigogo unategemea utakuwa mtu mwenye akili kweli..
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom