Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Hahahaa!

Jomba naona hao ‘mabaharia’ wanakuboa sana.

Anywho, kwa kiasi kikubwa sana siku hizi humu hakuna mijadala ya maana.

Mingi iliyopo ni ya kijinga kijinga tu.

Ndo maana baadhi yetu tumepunguza hata uwepo na ushiriki wetu humu....
Hao 'mabaharia' ni wajuaji wasiojua kitu!
 
..kuna uvumi ulienezwa kuwa Raisi Magufuli kapata tuzo ya uongozi bora.

..Ikulu haikukanusha iliacha wananchi waamini uzushi huo.

..ila mitandao ya kijamii inasaidia sana kujua wananchi wanafikiria nini, na uelewa wao ni wa kiwango gani.
 
Nimejifunza kiongozi huyu hapendwi kabisa na wananchi wake! Walifurahia sana kuwa bora anaewanyanyasa na kujiona mungumtu kaondoka!
Hapendwi na Mafisadi kama wewe na Wenye Uchu wa Madaraka kama wawe. Kwa Dunia ya Sasa ni taabu kwelikweli kumpata Rais Mzalendo kama Dr.JPM. Mungu ni Mwema na Atashughulika na Wewe Mchawi.
 
Nimejifunza kiongozi huyu hapendwi kabisa na wananchi wake! Walifurahia sana kuwa bora anaewanyanyasa na kujiona mungumtu kaondoka!
Nimejifunza wanao mpenda huyu magufuli ni wengi kuliko unaweza ukadhani pamoja na mapungufu yake still ni kiongozi mwenye faida nyingi kuliko hasara kwa taifa
 
Point yangu ya pili haimaniishi CCM haina mapungufu, Yes CCM ina Mapungufu yake Je hawa ambao ni mbadala wa CCM vitendo vyao vinatuthibitishia kuwa wapo tayari kuwa mbadala wa CCM? Wanasema heri zimwi likujualo kuliko lisokujua huu msemo ndo huwa tunautumia tunapopiga kura tu
Aisee!!!
 
Fundisho kubwa ni kwanza kwa nini taarifa za kifo cha mhe mkubwa wa nchi kisubiliwe kwa bashasha hivyo kama ongezeko la mishahara... Kuna mpasuko mkubwa the way siasa zinavyoendeshwa kuna genge linadhani funga mikono na miguu wapinzani wenye mawazo mbadala then wanawatupa ulingongoni kupambana. Hatufiki....
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia kwenye kuvuja kwa siri za Ikulu.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 2.4 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii hata isiyoamini kwa haraka (skeptical).

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia ya kitendo iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini na kuushadadia wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza ni baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji, Godbless Lema na Lazaro Nyalandu wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu! Lazaro Nyalandu anatoa ujumbe wa kuliombea Taifa na mishumaa!

Haya ni maendeleo makubwa kwa taasisi/watu waliopewa dhamana ya kumlinda Rais na siri za Ikulu.

Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
 
Nimejifunza pia kuwa:
1. Uzushi/uongo huo hata wewe mwandishi ulikunasa.
2. Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii,siyo critical thinkers.
3. Tabaka tawala limepata ujumbe mujarabu kuhusu linavyotazamwa na wasaga nyasi.
4. Kunahaja ya kuwa na mijadala(national dialogues) ya kitaifa kuhusu jinsi gani taifa lienende.
 
Hata zile zisizokuwa changa au zilizopevuka,hazijapona. Propaganda za mitandaoni huziyumbisha mpaka zinaomba msaada wa mitandao husika iondoe baadhi ya tarifa/uzushi/fake news.
Mkuu;
Kumbuka nchi yetu bado ni changa kwenye masuala ya mitandao na kwa sababu hiyo wanachi wengi wanaamini kila wanachokisoma kwenye mitandao.
 
Kwa ujinga waliouonyesha kwenye mitandao kuhusu taarifa za uzushi za hali/afya Rais ni wazi kuwa Chadema hawastahili hata uenyekiti wa mtaa... Tuendelee kuchapa kazi...
Uzi Tayari

Jovic Jovic
Cdhani kama wote walioamini uzushi huo ni CHADEMA,labda kama una chuki binafisi na CHADEMA mkuu.
 
Sina neno LA kukwambia zaidi ya mpumbavu, wew hujui jambo lolote umekuja hapa na kuandika ujinga ujinga ukitegemea watu watakuamin Kama jamaa alikuwa haumwi twambie sasa ilikuwaje akakatiza ziala na kughairi baadhi ya vikao... Wewe ni mpumbavu yatosha kukupuuza
 
Aliyekibonyeza alitaka kupima imani za kishirikina walizonazo nzego,coz kuna walioamini kuwa moshi huo ni makombora ya kimakonde.

Moshi uliomzunguka kiongozi katika ziara Kusini mwa Tanzania siyo uchawi bali ni sehemu ya zana za kisasa za ulinzi zilizopo ktk magari ya VIP pengine kitufe kilibonyezwa kwa makosa sehemu isiyo stahiki
 
Wabaya wapo ndani ya utawala, Zito ni mjumbe wao tu, ambaye hastahili kuuawa, kwa namna yoyote ile. Wasakwe wanaompatia taarifa nyeti za kiusalama, waadabishwe kikamilifu. Siku zote kikulacho kinguoni mwako!
 
Nimejifunza kuwa mh. hapendwi na watu wengi sanaaaa, kwani kuna baadhi walianza kufurahia aumwe hadi afe.Ana maadui wengi sana huku mtaani, 1. Vyeti fake family, 2. Waliohitimu na kukosa ajira toka aingie madarakani, 3.Anaowatumbua na kuwadhalilisha mbele ya wananchi, 4. Watumishi ambao hajawapandisha mishahara toka aingie madarakani, 5.Wahanga wa bodi ya mkopo ambao wanakatwa 15℅ n.k. Arudi nyuma ajitahmin kwa nn watu wengi wamefurahia hiyo skendo ya ugonjwa wake?
 
Back
Top Bottom