Tumelala giza tumeamka bado hakuna umeme !.

Tumelala giza tumeamka bado hakuna umeme !.

Jana Arusha kutwa nzima hakuna umeme,usiku umeme ulirejea saa 7 asubuhi saa 1:43 wamekata.

Tumeshindwa kupasi nguo,vyakula kwenye fridge vimeharibika,tumelipia Dstv full package hatuna tunaweza kutazama.

Kipindi kuelekea Christmas [emoji319] majumbani ukiwa mtupu.

Tunajuwa Makamba alihujumu TANESCO hukumchukulia hatua stahiki.

Umempachika Dotto Unaibu Waziri Mkuu na Nishati lakini hakuna cha maana zaidi ya misafara na mbwembwe ambazo hazitusaidii Watanganyika.

Ila Arusha miaka nenda rudi Umeme ni Tatizo, Sijajua changamoto ni nini.
 
mlimnanga sana yule jamaa sasa kinawapata kiberiti alichowasha kimezima!.. mkamuita dictator mlifikiri nchi hii inatakiwa iongozwe soft soft!.
hata hivyo shangazi alishagasema vinampwaya viatu vyakaka!.
nchi inaongozwa na wenye pesa zao amabao wanataka mambo yao yapite ili biashara zao zifanyike!.

alipowagusa hao watu wakubwa mkaanza kusema "haki za binadamu haki za binadamu!"
mmesahau kuna watu walikimbia nchi..?
kama walikuwa ni wenye haki kwanini walikimbilia mafichoni..?
hamtafumbuka macho msipokubali kufumbuliwa!
mmkikaa kimdebwedo hata visivyoliwa vitaliwa.
Nchi za Kiafrika hizi zinahitaji viongozi aina ya Magufuli na Kagame. Tuwape miaka 30 wanyooshe nchi halafu watuachie. Nakwambia bara zima hili litavuvumka na kupiga hatua sana.

Mimi naamini hii demokrasia ya Kimagharibi hii ni mtego tu wa kuendelea kuididimiza Afrika. Ulaya na kwingineko wao waliendelea wakati wa udikteta wa kifalme; na vinginevyo. Siamini kama wangeweza kufika hapo walipo na upuuzi huu wa demokrasia bandia hii ya mgongo wa chupa tuliyonayo Afrika.

Afrika inahitaji akina Kagame zaidi kuliko akina Samia - potelea mbali hata kama kutakuwa na maumivu kidogo maana hakuna maendeleo ya maana bila maumivu...
 
kwa wenye akili huu ndio wakati wakuvuna utajiri wakutosha kabla hawajaja hao akina magu..
nchi inavunwa na inaliwa,urafi na uroho bila kuwa na rungu lakudhibiti hakuna kituko tutaacha kuona sahivi nishaanza kuionea huruma thamani ya pesa yetu!
 
Watanzania wanapata shida sana, gharama za maisha zimepanda kila mtu analalamika. Nauli wamepandishiwa bila huruma, wakitaka kufanya biashara waweze japo kula, umeme wanaoutegemea wanakatiwa.

Viongozi wao wanakimbia na kuwapita kwenye foleni utadhani kuna kitu cha maana wanawahi ili kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom