KERO Tumelipia viwanja Vikonje 'BM' – Dodoma, kampuni iliyotuuzia imeingia mitini, tunaomba msaada Serikalini hatusaidiwi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni kuna kampuni inauza viwanja inaitwa Landmatrix Ltd walikuja ofisini kwetu na kutueleza kuwa wanauza viwanja vilivyopimwa maeneo mbalimbali mnamo mwaka 2024 kwa wakati huo walikuwa na mradi eneo la Vikonje 'BM', Dodoma.

Malipo yalikuwa ni kwa awamu ndani ya miezi 24 na makubaliano yalikuwa ukifikia asilimia 80 unakabidhiwa hati. Sasa tumelipa zaidi ya asilimia 80 na tukajazishwa fomu za hati, ila changamoto imekuwa ni kwamba hatupati mrejesho wowote kutoka kwao na bahati mbaya simu zao hazipatikani pia ofisi imefungwa hapo tumepata wakati mgumu.

Tumefanya jitihada za kuomba msaada serikalini ikiwa ni kuandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa jiji kuomba msaada wake ila hadi muda huu hatujapata mrejesho wowote.

Wasiwasi ni kwamba tunahisi jamaa wametutapeli maana tunasikia wengi wakilalamika bila kupata msaada, tunaomba serikali iingilie kati suala hilo ili tupate haki zetu
 
Uje utupe taarifa iliyo kamilika...
 
Wasiwasi ni kwamba tunahisi jamaa wametutapeli maana tunasikia wengi wakilalamika bila kupata msaada, tunaomba serikali iingilie kati suala hilo ili tupate haki zetu
Mkuu unaleta tuhuma za utapeli kwa HISIA?, weka facts mezani na ushahidi wa kutosha kuwa umetapeliwa.

Je maeneo mliyonunua yana mgogoro? Je kuna kesi yoyote kwenye eneo ulilouziwa? Umefanya uendelezaji wowote hapo ukapata kikwazo? Umejaribu kufuatilia hati na upimaji wewe binafsi na ukapata kikwazo chochote?

Kama hayo yote hayajatokea, unasemaje UMETAPELIWA? Kwa facts zipi?.

HATI siku zote ni lazima uifuatilie mwenyewe, hizo Kampuni huwa hazifanyi hio shughuli, wakikuuzia kiwanja hati kapambane mwenyewe, Mtu akuuzie kiwanja bei mbuzi, umlipe miezi 24, halafu akupe na HATI. HAIWEZEKANI.

Be a Man, Focus na kutatua changamoto na sio kulaumu.
 
Kuna kampuni inaitwa Land Consult Limited nayo ilikuja na gia ya aina hiyo na kujipa majukumu ya kupima kila kipande cha ardhi katika kata ya Chanika, Dar es salaam kwa ahadi za Lukuvi kuwa kila kiwanja kitakachopimwa kitapatiwa hati.

Mbinu hiyo inayotumiwa na makampuni kujitokeza huko wizarani na kutambulika na kupewa tenda za namna aliyoelezea mtoa mada nadhani ina viashiria vya ufisadi ambao viongozi wakuu huko wizarani lazima watakuwa wanapata mgao wa utapeli huu.

Haiwezekani Kampuni kama Land Consult Limited ifungue ofisi katani Chanika, Ikusanye pesa kwa wananchi shilling kuanzia 150000 hadi 250000 kwa kila kaya, wapime viwanja na kuwekea watu mawe halafu wafunge ofisi na kupotea hivi hivi tu hata kata kwenye hiyo Halmashauri na Wizara wakwambie tu kwamba Kampuni ilifilisika na mmiliki wa kampuni alifariki. Huu ni ulaghai kwenye ngazi ya juu kabisa ya taasisi.
 
Kero yangu ni kuna kampuni inauza viwanja inaitwa Landmatrix Ltd walikuja ofisini kwetu na kutueleza kuwa wanauza viwanja vilivyopimwa maeneo mbalimbali mnamo mwaka 2024 kwa wakati huo walikuwa na mradi eneo la Vikonje 'BM', Dodoma.

Malipo yalikuwa ni kwa awamu ndani ya miezi 24 na makubaliano yalikuwa ukifikia asilimia 80 unakabidhiwa hati. Sasa tumelipa zaidi ya asilimia 80 na tukajazishwa fomu za hati, ila changamoto imekuwa ni kwamba hatupati mrejesho wowote kutoka kwao na bahati mbaya simu zao hazipatikani pia ofisi imefungwa hapo tumepata wakati mgumu.

Tumefanya jitihada za kuomba msaada serikalini ikiwa ni kuandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa jiji kuomba msaada wake ila hadi muda huu hatujapata mrejesho wowote.

Wasiwasi ni kwamba tunahisi jamaa wametutapeli maana tunasikia wengi wakilalamika bila kupata msaada, tunaomba serikali iingilie kati suala hilo ili tupate haki zetu
Nasikia vikonje yote,watu wanatakiwa watoke Maana IPO karibu na TBC na fence ya Ikulu,ni kweli?
 
Back
Top Bottom