Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
TUMEPOTEZA JABARI NA MWAMBA WA UCHUMI KATIKA SIASA ZA AFRIKA
NA ELIUS NDABILA
0768239284
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemaliza kazi yake aliyoandaliwa kufanya hapa duniani. Kifo si hiari, ni lazima kwa kuwa vitabu vya dini vinatuasda kuwa kila mtu aliyezaliwa na mwanamke siku zake si nyingi duniani. Hatuna sababu za kulia kwa sababu ya kipenzi chetu Magufuli kufariki, bali tunaowajibu wa kuendelea kumuombea kwa kuwa Mungu amechuma ua lake.
Wakati tunafikiria msiba wa Rais wetu, Biblia inatufundisha kuwa Mungu ndiye chanzo cha uhai wetu. Vitu vyote vyenye uhai vilitoka kwa Mungu. 1 Kor 8:6. Mwanadamu pia aliumbwa na Mungu. "Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake." Zab 1
Mwanadamu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu, Mwa 1:26."Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai." Mwa 2:7. Tunaona hapo vitu vinavyounda uhai, cha kwanza ni mavumbi ya ardhi, cha pili ni pumzi ya uhai.
Muunganiko wa viwili hivyo huleta nafsi hai yaani mavumbi ya aridhi na pumzi ya uhai.Katika mlinganyo huo, ukiondoa kitu kimoja tayari hakuna uhai. Mavumbi ya ardhi pekee sio hai, hali kadhalika pumzi ya uhai pekee sio kitu hai. Hivyo twaweza kusema kifo hutokea wakati pumzi ya uhai inapotengana na mwili. "Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa." Mhu 12:7.
Ni rahisi tu, mwili ulitoka kwenye mavumbi ya ardhi na hivyo pindi mtu anapokufa mwili huo utarudi katika mavumbi na huko utaoza na kuwa sehemu ya udongo. Pumzi ya uhai ilitoka kwa Mungu na hivyo humrudia Mungu, pumzi hii ya uhai ndiyo roho.
Hayati Magufuli amefanya kazi kubwa katika uongozi wake ambao kwa akili za kibinadamu tunaamini amekamilisha kazi yake ya haspa duniani. Magufuli ametuachia miradi mingi ambayo ataendelea kukumbukwa vizazi na vizazi. Historia ya Tanzania, Afrika na Dunia itaendelea kumkumbuka kama Rais ambaye alisimama kidete katika kuwasimamia Watanzania hasa wanyonge ambao miaka mingi walikuwa hawafurahii keki ya Taifa.
Hayati Magufuli alishajua kuwa duniani hapa si makao ya milele bali alijua kuna siku atafariki. Katika uongozi wake kila alipopata nafasi ya kuhotubia alitukumbusha mambo kadhaa, kubwa alisema amejitoa sadaka kwa ajili ya Watanzania, Pili alisistiza kumuombea kwani ametoa sadaka Maisha yake na pia alisistiza Watanzania kuwa wamoja kwa masilahi ya Taifa. Magufuli aliwasistiza Watanzania kufanya kazi kwa bidi na maarifa huku akisema Tanzania ni Tajiri na ninatamani siku moja iwe iwe nchi inayotoa mikopo.
Idadi kubwa inayojitokeza kumuaga Hayaji Dkt Magufuli ni inshara tosha kuwa alikuwa kiongozi wa wat una ambaye kwa kiasi kikubwa watu walimuelewa. Lakini pia inatuma ujumbe kwa Watanzania wachache na dunia kwa ujumla kuwa si kweli kuwa Magufuli hakuwa chaguo la watu bali alikuwa tumaini la watanzania wengi ukiondoa Wala rushwa, Wezi, Wanyonyaji na watu wengine waliokuwa wamezoea kuishi kwa jasho la wengine.
Katika Makala hii nimewahoji Watanzania kadha kwa kuwauliza je wao watamkumbuka kwa jambo gani Hayati Dkt John Joseph Magufuli? Na haya yalikuwa ni maoni yao,Mary Steward Mwenisongole wa Dodoma, Nitamkumbuka Hayati Dkt Magufuli kwa kutujali wanyonge wa hali ya chini, miradi mikubwa ya maendeleo, nidhamu kwa watumishi kubwa zaidi kumtanguliza Mungu kwa kila jambo alilo kuwa anafanya.
Hagai Sanga wa Kiwira-Rungwe, Nitamkumbuka Hayati Mhe Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa misimamo yake thabiti katika kulinda raisilimali za nchi na kurejesha nidhamu katika ofisi za umma. Alijitoa sadaka kwa ajili ya Tanzania.
Shaibath T. Kapingu wa Songwe, Nitamkumbuka Dr John Magufuli kwa usimamizi mzuri wa fedha za umma na miradi mikubwa ambayo ama hakika itakuwa na tija. Lakini sitamsahu kwa elimu bure na kuboresha sekta ya Afya na kipekee zaidi ni namna alivyokuwa anatatua kero za Wananchi wanyonge kwa wakati na kulinda maslahi yao.Katika Uongozi nikiwa kiongozi kijana nitamkumbuka kwani Uongozi wake umetupa fursa Vijana kufanya siasa na kushiriki shughuli za kiuchumi na zaidi aliamini katika kutoa fursa kwa Vijana.Tumepoteza jabari na mwamba wa uchumi katika siasa za Afrika.
Bariki Ndondole wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Nitamkumbuka Rais Magufuli kwa kuleta nidham kwa Watendaji wa Umma. Kwa Sasa wananchi wanapata hudumu bila ubaguzi wa vyeo au vipato.Ni mengi alifanya kama Elimu bure ,kupinga rushwa, usalama wa nchi,hamasa ya kuchapa kazi na kufufua viwanda na mengine mengi sana. Mungu amuweke mahali pema.
Edna Lamerck wa Ilemela Mwanza, Nitamkumbuka Rais Magufuli kwa kuwa alisimamia vizuri maslahi ya watumishi Serikalini na kulipa mishahara kwa wakati kuliko kipindi kingine chochote.
Godfrey Mulima Matesi wa Serengeti, Nitamkumbuka Rais Magufuli kwa kuwa alisimamia Misingi ya Utawala Bora akiwa mzalendo nambari moja na kielelezo kwetu.
Pili, alituheshimu na kutunyenyekea akianza kwa Mungu kisha kwa matabaka yote ya Watanzania.
Tatu, hakuamini katika kushindwa, kwa kumtegemea Mungu Mhe. Magufuli alifanya makubwa yanayoonekana hata sasa.
Nne, ni Rais wa pekee Aliyetusihi tumtazame Mungu kwanza katika changamoto yoyote ile. Tumpate wapi Mtu kama Yeye atuelekezaye kwa Mungu kama tumaini letu! Mapenzi ya Mungu yatuku.
Mwalimu Majaliwa sikabenga wa Kinondoni nitamkumbuka Hayati Dr. John Pombe Magufuli kwanza kwa namna alivyokuwa ni kiongozi anayeamini katika malengo, mikakati, utekelezaji ili kuleta matokeo makubwa. Lakini pia aliamini katika kasi na weledi katika utekelezaji ili kutimiza malengo na kuleta matokeo yaliyokusudiwa. Tabia hii ya kiongozi huyo shupavu kuwahi kutokea ndiyo iliyosukuma maendeleo makubwa kwa mda mfupi. Pumzika kwa amani hayati Dr john pombe Magufuli.
Kumuelezea Hayati Magufuli kunahitaji muda mrefu kwani ni Dhahiri ameacha alama ambayo haitafutika katika ulimwengu huu. Tangu aingie madarakani alikuwa mfano kwa bara la Afrika nan chi zingine zikitamani kumuazima ijapo kwa wiki moja tu.
Hatua zake zilizoangazia utendakazi na matokeo zilipigiwa mfano kote barani Afrika, wengi wakisema kipindi hicho kuwa - dozi yake ilihitajika kwa mataifa kushughulikia masuala yao mengi ya utawala.Katika siku yake ya kwanza ofisini kama rais alituma ujumbe mkali kwamba asingevumilia tatizo sugu la utoro kazini kwa wafanyakazi wa umma na kuzuru wizara ya fedha na kuuliza walipokuwa maafisa mbalimbali katika wizara hiyo.
Pia alikabiliana na kufuta maelfu ya wafanyakazi hewa kutoka katika mfumo wa malipo ya serikali na 'kuwatumbua' hadharani maafisa waliotuhumiwa kwa ufisadi ama kutofikia viwango vya ufanisi vilivyotakiwa. Wakati mwingine yote hayo yalifanywa katika runinga, mubashara.
Alianza pia kwa kukabiliana vikali na alichokiona kama uharibifu wa pesa za umma huku akifuta sherehe ya kuadhimisha siku ya uhuru kwa mara ya kwanza katika miaka 54. Badala yake aliagiza pafanyike kampeni ya usafi nchi nzima na yeye mwenyewe akiwa mstari wa mbele katika shughuli hiyo, akizoa taka nje ya Ikulu.
Rais Magufuli pia atakumbukwa kwa misimamo yake ya kutetea haki za wanyonge na jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo alikuwa na usemi maarufu wa ''Hapa Kazi Tu''Rais Magufuli pia alikuwa mfano kwa viongozi kadhaa wa Afrika ambapo baadhi hata waliiga namna ya utendaji kazi wake, ambaoo atakumbukwa kwa kuzuia safari za nje kwa viongozi wa uma.Magufuli anaondoka akiwa ameiacha Tanzania katika uchumi wa kati ambayo ndiyo ilikuwa ndoto yake tangu alipoingia madarakani.