Tumeshinda kwenye Operation “Vaa Barakoa” sasa tuhamie kwenye Chanjo

Tumeshinda kwenye Operation “Vaa Barakoa” sasa tuhamie kwenye Chanjo

Hii nayo tutashinda Mkuu kule Twitter mwigulu wamemchapa za uso na wanaendelea kumchapa za uso tena kwa facts. I love Twitter’s Republic zamani uhuru wa kule ulikuwepo hapa ila siku hizi utaishia kula ban.
wengine tumegeuka wagonga like tu.. jf ya sasa ni utoporo mwingine
 
Muacheni huyo mchato asije akaagiza kuswitch internet off mwaka mzima,maana kama kigogo amefanya watanzania wavunje sheria kwa kutumia akiwemo VPN
 
Basi tuanze na mashinikizo ya kuitoa ccm kabisa madarakani na kuweka katiba mpya maana inaonesha kumbe tuna nguvu ya kushinikiza.
 
Ni kweli kabisa wakubali chanjo watu wapewe wao wanatumia mitungi ya oksijeni , mmoja wao katuambia leo katumia wiki mbili, je mwananchi wa kawaida analindwaje, wanaharakati na Viongozi wa dini watusaidie kwa hili.
Upo sahihi. Tuzidi kuwasihi viongozi wa dini, wazidi kuihimiza Serikali kuutimiza wajibu wake.

Kwa kuwa hoja ya msingi ya Serikali ni ughali wa chanjo (ule utopolo wa Mwigulu kuwa eti Dar kuna joto Ni upuuzi), tupiganie hospitali binafsi na taasisi binafsi zinazojihusisha na masuala ya afya kupewa uhuru wa kuagiza na kutoa chanjo.

Kauli ya viongozi wa dini imeonekana kuwa na nguvu kwa serikali kuweza kubaeili fikra zile zisizo sahihi dhidi ya corona, basi hawa hawa watuongoze katika kulipigania hili la chanjo. Lakini chanjo iambatane na upimaji
 
Mjifunze basi kuomba kistaarabu,,kwani mkiomba kwa unyenyekevu kitaharibika kitu?,,sio lazima kutunishiana msuli,,nna hakika mkiomba kwa staha,hizo chanjo zitakuja tu...
Ujue mtoto anarithi tabia toka kwa mzazi/mlezi.
 
Uongo una tabia ya kuwahi kufika lakin haudumu, ukweli una tabia ya kuchelewa kufika lakin ukishafika unadumu
 
Mkuu Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo haziko kwenye orodha ya nchi zitazopewa chanjo,kwa kuwahakuna takwimu ya wagonjwa Wa corona.

Na nchi kama nchi ilitangaza kuwa corona ilimalizwa na maombi ya siku tatu.

Na ninavyomjua Baba,hakubali kushindwa,hasa na mabeberu.
 
Mjifunze basi kuomba kistaarabu,,kwani mkiomba kwa unyenyekevu kitaharibika kitu?,,sio lazima kutunishiana msuli,,nna hakika mkiomba kwa staha,hizo chanjo zitakuja tu...
Tumnyenyekee Kwan anaiagiza chanjo kwa pesa yake? Si Ni Kodi zetu wananchi?!!!
Kupata chanjo na matibabu Ni haki ya wananchi siyo mtu mmoja anaamua peke yake. Nyie Kama mnamwabudu binadamu kiasi Cha kuhatarisha hata Maisha yenu mwabuduni huko huko kivyenu; Sisi tunamwabudu Mungu muumba wa mbingu na nchi si binadamu..vyeo Ni kitu cha kupita tu.
 
Wakati waliozitengeneza chanjo wananchi wao wanazikimbia, Waafrika wanalilia. Huku mnachomwa na jua mwaka mzima na kupata vitamin D ya kutosha, mnakula vyakula vulivojaa vitamin C, bado mnalilia chanjo.

Iko ambayo imeonyesha mafanikio makubwa,nimesahau ila inaanza na herufi p ngoja nimalizie k vant niicheki jina lake.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Mlishindwa kumpigania Lisu apate japo 20% sembuse huu ujinga wenu?

Corona itapita huku mkiendelea kuwa wajinga hivi hivi.
Korona Inapita na wakubwa wote sasa.

Ulitaka tumpiganieje Lisu?.
 
Wakati waliozitengeneza chanjo wananchi wao wanazikimbia, Waafrika wanalilia. Huku mnachomwa na jua mwaka mzima na kupata vitamin D ya kutosha, mnakula vyakula vulivojaa vitamin C, bado mnalilia chanjo.

Hata Corona yenyewe mlidai huku haipo sababu eti huku Ni joto...ok endeleeni kudhihaki huu ugonjwa utawanyoosha tu.
 
Back
Top Bottom