Tumeshinda kwenye Operation “Vaa Barakoa” sasa tuhamie kwenye Chanjo

Tumeshinda kwenye Operation “Vaa Barakoa” sasa tuhamie kwenye Chanjo

Endelea kutudhih
[emoji23][emoji23][emoji23]Mlishindwa kumpigania Lisu apate japo 20% sembuse huu ujinga wenu?

Corona itapita huku mkiendelea kuwa wajinga hivi hivi.
Endelea kutudhihaki na kufurahia kutudhumu uchaguzi. Ila na sisi tutakapofurahia RIP msilalamike. Mungu yupo, Ni wa kwetu sote na atatulipia khisasi Insha Allah.
 
Hiyo chanjo ianayokataliwa na wazungu ndio hawa maskini huku kwetu wataletewa na kulazimishwa kuchanjwa.
Kuna aina kama 10 zilizoidhinishwa na WHO ni ipi haifai kwa Tanzania au mnafuata mkumbo tu.
 
Hapo Mwanzo msimamo wa Rais na serikali nzima ulikuwa Tanzania HAKUNA KORONA kwa hiyo hakuna haja ya kuvaa barakoa. Baada ya wananchi, wanaharakati na baadhi ya viongozi wa dini kuonyesha msimamo wao wa kuvaa barakoa, serikali ikaanza kubadilika, tukaanza kusikia Tanzania ina korona chache sana mara hakuna aliyezuia kuvaa barakoa, mwisho wakakubali eti ukitaka kuvaa vaa za Tanzania, kwa wananchi huo ni ushindi.

Hatua inayofuata ni kuishinikiza serikali ikubali kuleta chanjo ya virusi vya korona.

Dalili ni nzuri, kwanza wameanza kusema chanjo ni ghari kitu ambacho hakina msingi wowote kwenye afya ya mtu, halafu wanasema eti hazijajaribiwa kwenye nchi za joto kama yetu sijui hizo taarifa wamezitoa wapi.

Najua mwanzo wataona aibu kukiri kama ilivyokuwa vigumu kukiri uwepo wa Covid 19, watakuja na maneno mengi wakijidai kuchagua aina ya chanjo inayofaa lkn mwisho watakuja kukubali kuileta kwa aibu kubwa.

Aluta continua.
 
Kuna aina kama 10 zilizoidhinishwa na WHO ni ipi haifai kwa Tanzania au mnafuata mkumbo tu.
Astrazeneca imeidhinishwa na WHO lakini ulaya wanaikataa, na South Africa waliitupa jalalani.
 
Duh wewe ni mwoga hakuna mfano. Unaonekana kuwa na nakisi kubwa ya elimu ya uraia. Hao viongozi wa dini hawadai haki kwa niaba ya waumini bali wanadai haki wakiwa sehemu ya raia; wakiwakilisha kundi kubwa la wananchi. Ujitokeze kuungana na wenzako kudai haki ya kupata chanjo bila kusubiri maaskofu. Aidha, chanjo haipaswi kutolewa kwa kila mtu kujigharimia mwenyewe. Serikali inawajibika kutumia rasilimali za wananchi kugharimia chanjo ya Covid 19 na kisha kuisambaza na kuhakikisha wananchi wanapata chanjo hiyo kwa ajili ya kulinda afya na usalama wa wananchi wote wa taifa hili. Jiongoze ndugu.
Utambue kwamba kwa uongozi tulio na nao, lazima upate pa kuanzia.
 
Endelea kutudhih

Endelea kutudhihaki na kufurahia kutudhumu uchaguzi. Ila na sisi tutakapofurahia RIP msilalamike. Mungu yupo, Ni wa kwetu sote na atatulipia khisasi Insha Allah.
RIP mbona hata huko chadema zinatokea sana?
 
Mjifunze basi kuomba kistaarabu,,kwani mkiomba kwa unyenyekevu kitaharibika kitu?,,sio lazima kutunishiana msuli,,nna hakika mkiomba kwa staha,hizo chanjo zitakuja tu...
Kwenye Uhai wa Watu hakuna Staha,maana hawa wenye mamlaka hawapo kwenye huo utamaduni wanataka tupelekeshane.
 
Mfano babako anatoka asubuhi kwenda ktk mihangaiko,,unampa condition aje na nyama akitoka job,ataleta?..
Huo ni mfano usio na uhusiano na mada,jukumu kuu la Serikali ni kuhakikisha usalama wa afya wa Raia wake.
 
Natamani chadema watengeneze barakoa na ccm navyama vyote ili tununue tuvae
 
Chanjo pia mimi nina wasiwasi nazo tangu nimeanza kuona michezo ya kuigiza ya Bil Gates na mpiga dili wake Faucci, hawa washenzi huenda wakatuuzia chanjo feki kupiga hela. Ningeishauri serikali kama inasita juu ya chanjo za mabeberu hwawezi kununua hata za Cuba? Cuba wapo mbali sana kwenye sekta ya tiba na wameshagundua chanjo kadhaa za Corona nyingine zimeshaanza kutumika nchini mwao. Waagize kutoka huko basi kama walivyoagiza chupa za Madagascar. Pia kuna China na India huko sidhani kama wanaroho mbaya kama wamagharibi na washirika wake.

Dunia imehspiga hatua nzuri juu ya chanjo, tukubali tukatae hapa hatutoki bila chanjo ingawa nakubali umakini unahitajika katika kuchagua aina ya chanjo.
 
Kwa hiyo mlivokuwa mnakataa njia za kitaalamu za kujikinga mlifikiri watakufa chadema tu?!!! Hatuna nguvu za kupigana na vyombo vya dola mnavyoviamrisha vitugandamize lakin Mungu atatupigania
Njia zipi dogo?

Una habari kama USA pamoja na kuvaa barakoa mbilimbili, lockdown, sanitizers, famigesheni, distance nk lkini kuna wafu laki 5 wameondoka mpaka muda huu? Na wana maambukizi milioni 28?
 
Hata Corona yenyewe mlidai huku haipo sababu eti huku Ni joto...ok endeleeni kudhihaki huu ugonjwa utawanyoosha tu.
99% watu wanaouguwa Corona wanaoona, na hiyo ni kule kwenye nchi wanaokufa kwa wingi.
 
Back
Top Bottom