Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Tanganyika ilikuwa eneo la kilimo katika utawala wa Uingereza. Walitangaza uwekezaji katika kilimo na waliopenda kuwekeza iliwapasa kuonyonyesha uwezo wao wa kuiendeleza ardhi kabla ya kupatiwa eneo. Baada ya kuonyesha hati ulipewa miaka mitano uwonyeshe uwekezaji wa kudumu uluoufanya kabla ya kupewa hati.
Wagiriki wengi walikuja kuwekeza katika kilimo. Waliajiri watu, wao wenyewe na waliowaajiri wote walilipa kodi katika serikali ya Mwingereza. Walikuwa na uwezo wa kununua vifaa vya kisasa vya kilimo na walijenga maghala imara ya kihifadhia mazao yao.
Kutokana na ukubwa wa eneo la utawala la Jumuia ya Madola, mkulima alikuwa huru kupeleka nyanya zake Kenya, Zambia hata Malawi. Hii ilifanya wigo wa soko kuwa mpana.
Enzi hizo kijana akimaliza masomo ana uhakika wa ajira kwa Mgiriki iwe udereva wa trekta, lorry, au hata upishi na alikuwa na uhakika wa kusomesha watoto wake na kujenga nyumba bora.
Wagiriki wale hawakukaa mijini, walikwenda Iringa, Ruvuma, Lushoto na kuanza kuvunja mapori. Wakitusaidis kukuza miji pia.