Tumetoka mbali - kuna ngoma za zamani ni kama vile vocal imerekodiwa kwa simu ikadondosjwa juu ya beat

Tumetoka mbali - kuna ngoma za zamani ni kama vile vocal imerekodiwa kwa simu ikadondosjwa juu ya beat

Hiyo 50/ 50 bonge la ngoma waifanyie remix kwenye studio ya kisasa.. ongeza fid pale kati.na Lord eyez, .. itakuwa na fleva tofauti na itawarudisha kwenye gem.. hata ile mikwara ya GK ingefiti humo ila tatizo kile kigugumizi !

Warudi kwenye game kufanya nini, kwani wanahitajika?
 
Mapacha, hawa jamaa walikuwa wanapendelewa sana mabeat
Kuanzia

Fifty fifty

Tuna bang

Nipe jibu ft nurueli & mangwair
 

Hii ngoma ya mapacha - 50 50 ni kati ya ngoma nilizokuwa napenda wayback hiyo miakaya 2006 hivi. Kilichokuwa kinamivutia hasa ni beat zao, hata ile tunabang ina beat kali.

Sema leo nimeisikiliza nikagundua production hasa kwenye mixing ilikuwa chini sana.

Imenibidi nisikilize ngoma nyingi zaidi nikagundua ni maproducer wachache kama Pfunk na Master Jay ndiyo walikuwa wanafanya mixing nzuri.

Wengi ilikuwa ni kutengeneza beat ukatupia vocals tu na mziki unaenda.

Teknolojia imeenda kasi, zamani kurekodi ilikuwa kazi ila ukisharekodi umetoka. Leo kurekodi rahisi ila kutoka ndiyo kazi.

Maproducer walikuwa Mungu watu, nimemsikiliza Nikki Mbishi anasema prod kameta aliwahi wamwagia bia kisa tu wamekaa nje ya studio wanasubiri walau wazungumze naye.

Nikakumbuka miaka hiyo niliwah wapeleka wanangu kwa Kidbway - tetemesha records akatukalisha nje kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja usiku mpaka Hussein Machozi alipoenda kumbembeleza walau atoke aongee nasi.

Ila kwa sasa teknolojia imebadili kila kitu studio nyingi, msanii anaweza rekodi sehemu yoyote na ngoma ikawa nzuri, shida ngoma ni nyingi na kupigwa redion ni majaliwa.
Asante mkuu Leo umependezesha sana siku yangu hii ngoma ya 50/50 ni zaidi ya hip-hop ila zamani kulikua na mawe
 
Back
Top Bottom