Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora aisee maana sasa ivi wangekua apecha alolo kwenye usanii wao......Mmoja ni afisa TRA kanda ya kinondoni mwingine ni video director
Hiyo 50/ 50 bonge la ngoma waifanyie remix kwenye studio ya kisasa.. ongeza fid pale kati.na Lord eyez, .. itakuwa na fleva tofauti na itawarudisha kwenye gem.. hata ile mikwara ya GK ingefiti humo ila tatizo kile kigugumizi !
Asante mkuu Leo umependezesha sana siku yangu hii ngoma ya 50/50 ni zaidi ya hip-hop ila zamani kulikua na mawe![]()
Mapacha - 50/50 | Ngomanagwa
Mapacha - 50/50 by Ngomanagwa, Hip Hop music from Dar es Salaam, TZ on ReverbNationwww.reverbnation.com
Hii ngoma ya mapacha - 50 50 ni kati ya ngoma nilizokuwa napenda wayback hiyo miakaya 2006 hivi. Kilichokuwa kinamivutia hasa ni beat zao, hata ile tunabang ina beat kali.
Sema leo nimeisikiliza nikagundua production hasa kwenye mixing ilikuwa chini sana.
Imenibidi nisikilize ngoma nyingi zaidi nikagundua ni maproducer wachache kama Pfunk na Master Jay ndiyo walikuwa wanafanya mixing nzuri.
Wengi ilikuwa ni kutengeneza beat ukatupia vocals tu na mziki unaenda.
Teknolojia imeenda kasi, zamani kurekodi ilikuwa kazi ila ukisharekodi umetoka. Leo kurekodi rahisi ila kutoka ndiyo kazi.
Maproducer walikuwa Mungu watu, nimemsikiliza Nikki Mbishi anasema prod kameta aliwahi wamwagia bia kisa tu wamekaa nje ya studio wanasubiri walau wazungumze naye.
Nikakumbuka miaka hiyo niliwah wapeleka wanangu kwa Kidbway - tetemesha records akatukalisha nje kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja usiku mpaka Hussein Machozi alipoenda kumbembeleza walau atoke aongee nasi.
Ila kwa sasa teknolojia imebadili kila kitu studio nyingi, msanii anaweza rekodi sehemu yoyote na ngoma ikawa nzuri, shida ngoma ni nyingi na kupigwa redion ni majaliwa.