Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Amani iwe kwenu wapendwa katika bwana.
Wakati tukiendelea kuomboleza msiba wa Jemedari wetu Dkt Magufuli, tuna kila sababu ya kutafakari sana kama taifa. Haiwezekani tupoteze watu maarufu na wakubwa hapa nchini kwa kipindi kimoja, sababu ya kupoteza hawa viongozi zinatajwa kuwa ni chronic illnesses. Je, tunasahu kua huyu Kovidi ndio anawaondoa wenye Chronic illnesses? Kuna hata mmoja tuliyeambiwa kafa kwa Covid-19? Tutajuaje wakati halisemwi hili ni siri?
Ni kweli Mungu hupanga vifo lakini kwanza vifo hutangulia na sababu ndipo Mungu atume malaika wake kuja kubeba roho zetu. Tulipewa maarifa tuyatumie kupambana na mazingira lakini sasa huenda mazingira ndio yanatuzidi maarifa tunabaki na vilio kila kukicha.
Hivi tungekuwa strict kujikinga na COVID-19 100% tukachukua tahadhari katika kila kipengele kwa mujibu wa maelekezo ya wataalam na WHO mnafikiri leo hii tungekua na hamaki kila mitaa tunakopita au taifa sasahivi lingekuwa na utulivu wa aina gani?
Kuchukua tahadhari siyo lazima Lockdown wala si chanjo ya Mabeberu. Tahadhari tuliyokuwa nayo mwaka jana ilitosha sana kupunguza maambukizi na wala leo tusingekua na hamaki mitaani.
Tumepuuzia hili, timekimbizana kwenye njia za kienyeji au asili ambazo ni njia za pata potea kuliko za kitaalam. Tumeshindwa kuyatumia maarifa ipasavyo hii hali itatutesa sana.
Mwisho nawatakieni mwisho mwema wa wiki, tuchukue tahadhari binafsi kwa kujali afya zetu na familia zetu. Apumzike kwa amani Jemedari wetu JPM.[emoji120][emoji120]