Tumia pesa yako ndogo watu wakufanyie kazi

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Inawezekana una kaela kadogo; labda umepata kama mshahara, au kuuza kitu n.k, na ungependa pesa yako ikuzalishie na isipotee.

Unaweza ukawekeza kwenye haya makundi:-
  • Wauza mishikaki
  • Wauza matunda
  • Mama ntilie
Utaanzaje anzaje:-
  • Tembelea hayo makundi hapo juu
  • Tathmini mauzo yao kwa siku
  • Kwa wale wenye mauzo mazuri, ingia nao makubaliano ya kuongeza 'stock' huku mkigawana faida 50/50
  • Usiwape fedha, we wapelekee mzigo
  • Kama utawapata wengi, na faida pia itakuwa kubwa.
  • Kwa namna moja ama nyingine, unakuwa umemuajiri bila yeye kujua.
 
Uaminifu ni zero siku hizi, Ukifanya hivyo unajitafutia tu Stress, Bora pesa yako weka Bank tu aise
Unaweza kuanza na wachache kwanza, kwa kuweka hela kidogo ili kupima uaminifu
 
🀣utakuwa unashinda na kulala nao
 
Kwa 50/50 utakua uonevu. Naushia hpo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…