Tumpe Faraja Rais Samia kwa namna anavyofanya kazi bila kupumzika wala kukaa kwa ajili yetu Watanzania

Kabisa mkuu yaani mh Rais anafanya kazi kubwa Sana bila kupata muda wa kupumzika hata kidogo, Naomba ratiba ya mh Rais iangaliwe vyema ili Rais wetu awe anapata nafasi ya kupumzika kidogo ziarani,

Kupumzika nakozungimzia Ni kule Rais anakaa kidogo Ikulu, najuwa Rais wetu anatamani aonane na watanzania muda wote ili kuwatumikia kwa kuwasikiliza na kuwajibu maswali yao, kwa kutoa suluhisho penye utata
 
Tunaomba apate muda wa kupumzika bado tunampenda Raisi wetu
 
Si aliiomba kazi mwenyewe!! Faraja ya nini wakati unamlipa kwa kazi aliyoomba, hatumiki kwa hisani, ni wajibu wake, tunahitaji afanye zaidi ya hapo, mafaili yazunguke kitanda chake chote
 
Nyie chawa wa sasa bado sana kufikia level za chawa wa JPM.Hadi mje kufikia level za kina BIA YETU,KAWE ALUMNi huyo boss wenu atakua ameshaondoka madarakani.Wenzako walikua wanawekaga namba ya simu wewe vip au umesahau?.
 
Hamjulikani mnataka nini akitoka nje kelele akizungukia wananchi mikoani kelele kweli wewe ni 🚮🚮
 
Usawa huu wa vita ya Ukraine bado kuna watu mna mawazo namna hii? Matumizi mabaya ya rasilimali akili
 
Bei ya mafuta unayoiona kwa Sasa inatokana na kupanda katika soko la Dunia, lililochangiwa kwa kiasi kikubwa na Vit
Hatuhitaji Raisi wakupigiwa promo

Tunahitaji creative ,innovative, inventive
Person.

Akishakuwa na hizo sifa hapo juu wala haitaji Chawa kumpigia promo .


Aishi kama MKAPA leo Mkapa hayupo lkn Legacy yake inaishii.

Tunaona TRA,NSSF NA MASHIRIKA MENGI YA UMMA AMBAYO YAMEKUWA MSAADA KWA TAIFA HILI.

CHECK JPM vitu alivyofanya vinazungumzaa.


Wala huyu Mama hajajitahidi chochote.

Zaidi sasa ivi mnatumia nguvu ooo hadi 30
Wala hatuna habari hizo

Nina uhakika UCHAGUZI UKIWA HURU NA HAKI

HACHOMOKI YEYE NA YULE WA KULE SIJUI ZANZIBAR

NIMEMSISKIA JANA HUYO MPEMBA SHAKA ANASEMA HIVYO.




Usimuambie habari ya usalama wa raia na mali zao maana ni swala la kikatiba


Leo habari ya kazi kwa vijana wetuu tunapata kwasababu mtoto wa shangazi,sijui shemeji,sijui mtoto wa dada.








Bei ya mafuta unayoiona kwa Sasa inatokana na kupanda katika soko la Dunia, lililochangiwa kwa kiasi kikubwa na Vitaa
 
Pamoja na kuzunguka kwake na maisha yamezid kuwa magumu bora apumzike na mumewe tu.
 
Faraja peke atakayopata kutoka kwangu ni kimueleza ukweli kwamba ANADANGANYWA vibaya mnoo na wasaidizi wake aliowateua.

Ukweli ni huu. Kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo anavyozidi kufutika kwenye mioyo ya wapigakura wengi. Sababu ni hizi
1. Hajali hali mbaya ya kiuchumi ya wananchi
2. Nyongeza ya mishahara iliyojaa ghiliba nyingi
3. Kutoukubali ukweli kwamba vita vya Ukraine siyo sababu kuu ya inflations
4. Wateule wake wanatoa matamko na hakuna tija yeyote
5. Kuendelea kuuminya upinzani hususan kutoruhusumikutano yao
6. Kuendelea kupambana na marehemu bafala ya kuyarekebisha yale anayoyaona yalikosewa
7. Tozozisizowianana vipato vya wananchi na visivyozingatia mzunguko wa fedha

mwambie mama kuwa hali ni mbaya na aeneelee kushikilia hapo hapo ili CCM iendelee kuporomoka kwa kasi ya jiwe kwenye maji
 
Uchawa mwingine bwana! By the way umesahau kuweka namba kwa ajili ya uteuzi. Mwambie apunguze msafara wake maana ni mkubwa mno utakuja kukausha hazina yetu
 
toka mjue anafuatilia jf bas mnajipendekeza [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] afarijiwe kwa lipi mafuta kupanda tozo za miamala gharama za maisha toa ufakeni wako hapa
 
Hebu tutolee upuuzi sie,
Yeye ni Mtumishi wa Umma, yupo kazini, anapata mshahara na likizo pia anayo,

Angekua anajitolea huku hana anufaikacho kidoooooogo ungetushawishi.
 
Kama anataka kupumzika akae pembeni wapo watu wanaitaka hiyo kazi

Faraja atapewa na mumewe!
 
Watu wanakunywa chai kavu wanalala halafu unaleta maneno gani hayo mleta mada??
 
Maneno mazito sana haya mkuu.

Nimetokwa na machozi.
 
Mama haihitaji chawa maana kazi zake zinajieleza na Kuendelea kuwakongo nyoyo watanzania, msafara wa Rais umesheheni watendaji wote muhimu kwa ajiri ya kutoa ufafanuzi kwa Mambo mbalimbali yanayotekelezwa na serikali yetu
Uchawa mwingine bwana! By the way umesahau kuweka namba kwa ajili ya uteuzi. Mwambie apunguze msafara wake maana ni mkubwa mno utakuja kukausha hazina yetu
 
Nyie chawa wa sasa bado sana kufikia level za chawa wa JPM.Hadi mje kufikia level za kina BIA YETU,KAWE ALUMNi huyo boss wenu atakua ameshaondoka madarakani.Wenzako walikua wanawekaga namba ya simu wewe vip au umesahau?.
Sin haja ya kuweka namba ya simu maana Namuunga mkono mama yangu bila shuruti yoyote ile
 
toka mjue anafuatilia jf bas mnajipendekeza [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] afarijiwe kwa lipi mafuta kupanda tozo za miamala gharama za maisha toa ufakeni wako hapa
Mafuta hayajapandishwa na mh Rais wetu, Ndio maana unaona juhudi za mh Rais kupunguza Bei kwa kuweka Ruzuku ya billioni mia moja, ili kupunguza makali ya Bei, Hali ikitengemaa utaona Hali ikirudi Kama awali
 
Hafanyi kwa ajili yetu ndio maana unaona kila kitu kipo juu. Tuliokuwa tunaishi kwa kipato cha halali tumesimamisha ujenzi baada ya gharama za vifaaa vya ujenzi kuwa juu.

Kwa sasa kula ubwabwa imekuwa kitu cha anasa maana mchele haushikiki tena.

Yeye anafanya kwa ajili yake, familia yake na marafiki zake. Hapo anatafuta kujijenga kwa ajili ya 2025.
 
Nilivyoona heading nikajua umeandika kitu cha maana kumbe ni hizi pumba haya wale wakusifu na kuabudu kazi kwenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…