Tumsaide huyu mtanzania mwenzetu

Tumsaide huyu mtanzania mwenzetu

Sema kila kitu usaidiwe unasitasita nini! Mbona wewe ni muoga nani atakukamata kama unasema ukweli na ushahidi upoo
Watanzania wengi ni waoga sana kutetea haki zao,hasa zile haki zinazo mwinywa na taasisi fulani!!
 
Atakua mwalimu huyo.

Uoga kama huo. Pesa yako unaendaje kuomba akaunt ifunguliwe.

Nenda na barua ya kuwapa ultimatum ama wafungue akaunti au wakupe maelezo. Ultimatum ikifika kutaneni mahakamani
 
Si afungue kesi ya madai apige mpunga mrefu!Hana mwanasheria?
Kama account yake imeshikiliwa na Bank, hizo pesa za kumlipa Mwanasheria atazipata wapi!? Na unajua kabisa bila mpunga mbele hakuna Mwanasheria atakae kuelewa, wataona kama unawapigia kelelee tu!!
 
Ni mtumishi wa umma. Mshahara umeingia kupitia ac ya bank flani naihifadhi. lakini ukawa na nyongeza ya shilings kiasi cha milioni plus. Kutokana na hicho kiasi kilichongoozeka akaunti yake imeshikiliwa. Hawezi hata kuangalia salio.

Kila alipokuwa anaenda kuwaomba waachie account yake ni danadana kuwa baada ya masaa 24 kila kitu litakuwa ok lakini hola.

Ijumaa iliyopita alienda tena kuomba waiachie acount yake. Walimlaghai kwa maneno matam tena mbele ya bank manager kuwa kufika jumatatu kila kitu kitakuwa sawa. Lakini mpaka leo mambo ni yale yale tu. Acount bado haisomi chochote

Kinachotia mashaka ni pale alipoomba bank statement alikuta pesa yake ya mshahara yote haipo ikiwa ni pamoja na kiasi kilichokuwa kimeongezeka. Alikuta pesa aliyoiacha kabla ya mshahara haujatoka. So bank statement zote anazo za baada tu ya mshahara na hii ya juzi aliyokuta mshahara haupo wote na kiasi walichokuwa wameongeza.

Ameongea na customer care makao makuu wanamdirect tawini kuwa case yake inatatuliwa hapo.

Amepambaana kwa gharama kila siku anatoka kijijini kwenda mjini kwa hilo jambo lakini hola

Wataalamu wa mambo haya hii kisheria imekaaje
This is a serious case, kama ana ushahidi usiotia shaka apeleke malalamiko yake kwa HR yaanzie hapo, haiwezekani HR kaniwekea mzigo wangu Bank alafu Bank eti wauuzie kisa hivyo vimashine vyao vibovu kusingizia,sasa mimi vinanihusu nini!!??
 
Kila kitu kiko wazi kabisa ni ww tu kama kweli upo tayari toa msaada. Sielewi inasaidia nini kutaka kujua jina la mhanga
Nadhani wewe ndo mpuuzi kuliko huyo jamaa yako mwenye tatizo na benki. Utawezaje kumsadia mtu hujui hata jina la benki na branch? Acha upumbavu
 
Sio kwamba naogopa mkuu ila naamini waliofanya makosa ni watumishi wachache tu wasiokuwa waadilifu kwa kazi zao. Sio vizuri kuichafua taasisi yote
Usingeandika humu ungewafuata hao wachache wasio waadilifu warekebishe hilo tatizo.
 
Back
Top Bottom