Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Kama Samia atakuwa ni mtu wa kukaa chini na kufikiri kwa makini basi atagundua kuwa yeye kuwa hapo siyo accident, Bali Mwenyezi Mungu amemuweka hapo kwa sababu maalum.
Machozi na vilio ambavyo watanzania walipitia katika utawla wa Magufuli, Mwenyezi Mungu aliamua kuwafanyia wepesi kwa kumuondoa mtu ambaye kila mtu alishaona kuwa hashikiki tena, hawezekaniki tena, anachokitaka yeye anaweza kukifanya na asiwepo mtu wa kusema fyoko, na yeyote aliyethubutu basi alikiona cha mtema kuni.
Magufuli hakuanza hivihivi kuanza kubambika watu kesi, kufanya kazi na vikundi vya watu wasiojulikana, kupora korosho za watu, kuvunja nyumba za wananchi kikatili, kuonea wafanyabiashara, kuonea wapinzani, kufukuza watu kazi kwenye hadhara kinyume cha taratibu za utumishi wa umma, kuvumilia viongozi wahuni kama akina sabaya Ila alianza kwanza kwa kuvunja kiapo chake cha kuheshimu katiba na sheria za nchi.
Kinachonisikitisha kwa Samia ni kwamba hakuwa mwanafunzi mzuri kwa Magufuli kuweza kujifunza mwenzie alianzia wapi kwenye mserereko wake wa kuanguka. Magufuli alianza kuserereka kuelekea kwenye kufanya udhalimu nchini baada ya kuanza kuvunja sheria na katiba hasa zile zinazowapa wapinzani wake haki fulanifulani ambazo yeye alikuwa hazipendi!
Sasa hebu tazama kiapo cha raisi Samia huku ameshika Qur'an tukufu, anaapa kulinda katiba inayotoa haki kwa Wapinzani kufanya siasa nchi nzima halafu kwenye kiapo hicho anamalizia kwa maneno eeh Mwenyezi Mungu nisaidie, Kisha siku 100 baada ya kiapo hicho anasema vyama vya siasa hakuna kufanya mikutano ya wazi ila vikao vya ndani tu, hivi sheria ndivyo inavyosema?
Samia ameamua kufuata Umagufuli, Umagufuli huu hautomuacha salama, kwa sababu ni njia feki, si njia za haki hata kidogo. ni njia amabzo zimeshakuwa tested na zikafeli sana, na mwishowe aliyezijaribu akaishia kuwa muongo zaidi, muonevu zaidi, mnunua watu wamuunge mkono, mnyamazisha vyombo vya habari ili visikemee udhalimu wake.Kama si udhalimu wake kukema kupitia kifo chake yule mzee alikuwa anatupeleka shimoni.
Samia alikuwa na nafasi adhimu sana ya kufanya reforms za msingi katika nchi hii lkaini ameamua kuwa "caretaker" president kwa kuendeleza umagufuli, bila shaka amejikosesha nafasi adhimu ya kulifanyia mabadiliko ya msingi taifa hili ambayo yangempa heshima kubwa mbele ya umma.
Anasema eti anataka kujenga uchumi kwanza, kiukweli kabisa kutawala kwa mujibu wa sheria hakumzuii mtawala kujenga uchumi, bali ni kutafuta uchochoro wa kutowajibika mbele ya wananchi. Hatuhitaji kwenda mbali kupata mifano, tunaweza kuangalia hapahapa nchini. Hakuna utawala uliovutia Uwekezaji nchini kama utawala wa Kikwete, lakini Kikwete hakuminya uhuru wa kisiasa wa wananchi.
Ni wakati wa Kikwete tulishuhudi uchumi ukikua kwa asilimia 7 lakini yote haya yalifanyika bila kuminya uhuru wa kisiasa wa wananchi!. Sasa Samia inakuwaje atwambie eti shughuli za Kisiasa zifanyike kupitia vikao vya ndani tu, hiyo sasa ni siasa gani? Utawapataje wananchama wapya kwa vikao vya ndani?
Samia amewahi kuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba na mwaka 2015 alizunguuka nchi nzima kuinadi ilani ya CCM yenye kutaka tuwe na katiba mpya. Kama CCM imewahi kuataka tuwe na katiba mpya kabla ya kuwa na uchumi wa kati, Samia asitwambie eti tusubiri akuze kwanza uchumi ndo tuwe na katiba mpya wakati sasa hivi tayari tupo kwenye uchumi wa kati. Au anataka kwanza tuwe Donnor country ndo tuwe na katiba mpya?
Lugha aliyotumia ya kuwa ngoja kwanza akuze uchumi kimsingi anamaanisha kuwa Hataki katiba mpya. Ni sawa na mtu anayeaandika bango nje ya duka lake kuwa mkopo kesho, kesho yake ikifika bango bado linasoma vile vile kuwa mkopo kesho!, Sasa kukuza uchumi ni kazi isiyoisha, hakuna siku uchumi utatosha maana kuujenga ni kazi isiyoisha!
Kiukweli kabisa suala la Katiba mpya kamwe halikwepeki, ni kujitia upofu tu kukwepa suala hili. Kuna mahitaji ya utekelezaji wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012, Kuna mgongano wa katiba ya Muungano na ya Zanzibar kwenye amsuala ya muundo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, katiba ya sasa bado inatambua muundo wa zamani wa serikali ya SMZ, Kuna ukweli kuwa nchi sasa ikpo katika mfumo wa vyama vingi lakini katiba ya sasa ni ya mfumo wa chama kimoja. Kwa hiyo Katiba mpya haikwepeki.
Tangu zamani palipokuwa pakitokea tukio kubwa nchini, liliambatana na mabadiliko ya katiba
Sasa mwaka 2010 kulitokea mabadiliko ya muundo wa serikali ya Zanzibar, Kwa nini Katiba ya nchi haibadilishwi ili kuaccomodate jambo hili?
Samia aache kutafuta wepesiwepesi, asimame sasa kama mkuu wa nchi arekebisha discrepancy hii.
UCHUMI TUTAUJENGA TUTAENDELEA KUUJENGA, YEYE SIYO WA KWANZA AU WA MWISHO KUJENGA UCHUMI, SASA HIVI ANATKIWA AFANYE VYOTE YAANI REFORMS ZA MSINGI ZA NAMNA YA KUENDESHA NCHI HII PAMOJA NA UCHUMI

- Tulipopata uhuru, muda mchache baadae tulikuwa na katiba ya Jamhuri
- Tulipoungana na Zanzibar tuliingiza mambo ya muungano kwenye katiba
- Mwaka 77 baada ya Muungano wa ASP na CCM kulizaliwa hii katiba ya sasa ya Chama kimoja
- Miaka iliyofuata mabadiliko yalifanyika kuingiza muundo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ndani ya katiba