Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Ndugu zangu, ili tufanikiwe kwenye jambo lolote kama taifa, ni lazima tuwe na ‘collective effort’ kuyaendea mafanikio hayo.
Hata tuwe na Rais mwema na muadilifu kama Malaika, hatuwezi kuwa na taifa lenye uadilifu na mafanikio ya maana ikiwa tutafikiri kuwa yeye pekee ndio mwenye jukumu la kutufikisha tuendako na sisi jukumu letu ni kumvunja moyo na kumchanganya. Ikumbukwe, binadamu hata awe muungwana vipi, ikiwa atapata 'external negative pressure kubwa' anaweza kubadilika, sio kwa kuwa anapenda bali kwa kuwa akili ya binadamu hufanya kazi katika mfumo huo.
Hatimaye baada ya kilia lia, hatimae tumefanikiwa tena kupata rais ambaye ni muadilifu ‘down to the earth’ ambaye anataka kujenga nchi iliyotamalaki uadilifu. Chaajabu, tuliokuwa tunaombea apatikane mtu kama huyu, baadhi yetu tumeamua kuchukua upande wa kumvunja moyo na kumchanganya huku tukitengeneza tatizo ambalo badae sisi sisi ndio tutakuja kulaumu.
Kwa mfano; Amewaasa viongozi wafanye mambo kwa kiasi, wafanye mambo kwa kuzingatia wigo wao kisheria (Sphere of influence) na kuchukua haki na stahili zao kwa mujibu wa sheria tu na si vinginevyo.
Hatimaye, tumekuwa tunapindua, maelekezo hayo ambayo ni sahihi kabisa katika angles zote, tumeshadidia eti ameelekeza watu wafanye ufisadi!Ni nini hiki?
Kwa kawaida duniani kote, mtu yoyote akipewa kazi yoyote, anapewa wajibu na haki/stahili (kwa mujibu wa sheria) so tulitaka Mhe. Rais aseme, “Naagiza, kila mtu aende kufanya atakavyo na kuchukua atakacho kwa namna atakavyo”? Au tulitaka aseme ‘Nawaagiza mkatekeleze majukumu yenu na hamtalipwa chochote, yaani mna wajibu bila haki”? Kwa nini tunakuwa na roho mbaya na wanafiki kiasi hiki?
Mnakumbuka wakati falsafa ikiwa 'hapa kazi tu' ilizuka rai kuwa, inapaswa kuwa 'Kazi na bata' kwa kuwa hapa kazi tu maana yake ni wajibu bila haki na kazi na bata ni wajibu na haki? au tushasahau mara hii?
Je!
Si kulikwa na kipindi haijulikani kati ya mkuu wa wilaya kwa mfano, mkuu wa mkoa na Waziri nani mkubwa? Je! Tunaitaka hali hiyo tena?
Si tulikuwa na wakati mkuu wa wilaya kwa mfano aliweza kupiga matukio yenye utata kokote nchini hadi sasa wengine wamehukumiwa kama majambazi? So tunachopinga tena sasa tunapoambiwa kila mtu afanye vitu kwa kiasi na kwa mujibu wa sheria ni nini? Mbona tunakuwa na roho mbaya na wanafiki namna hii?na tabia hii ni kwa maslahi ya nani hasa?
Matukio ni mengi hatuwezi kuyarudia yote.
Kwa ujumla Mhe.Rais ni mtu muadilifu anayetaka kujenga nchi ya kiadilifu na yenye haki ambapo kila mtu atafanya anachopaswa kufanya na kupata anachostahili kupata bila kudhulumiwa au kudhulumu wengine na hiyo ndio Tanzania tunayoitaka.
Hata hivyo, hawezi kulifanikisha hilo peke yake ikiwa hatutamsaidia na kumpa ushirikiano wa kutosha. Kitendo cha kumkatisha tamaa, kuchanganya, kupindisha anachosema na kuleta roho mbaya badala ya kumsaidia ili tufikie malengo ya pamoja, tunakuwa hatujitendei haki wenyewe wala hatutendei haki nchi hii.
Ni bora tukajisahihisha. Unafiki na roho mbaya ni tatizo ambalo madhara yake hayachagui wa kumuangukia.