MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Kila niamkapo asubuhi naihoji nafsi yangu nilikua wapi? Nakosa jibu.
Ninapoaanza kunyanyua mwili wangu nasikilizia utimamu wa afya yangu ninajiuliza, ni kipi kinachonistahilisha afya hii njema, ili hali nimekua nikila junk food regularly na kulala na balimi kumi kichwani kila siku na kufika nyumbani salama. Nakosa jibu.
Ninapofungua mlango wa nyumba yangu, na kutazama mali zangu zilivyo salama ili hali niko katikati ya wanyang'anyi na mbwa mwitu. Nakosa jibu.
Ninapowasha simu yangu na kupokea habari za misiba na michango ya misiba kwenye ma-group mbali mbali nakosa jibu.
Ninapoenda Muhimbili au Ocean Road nakuona watoto wadogo wakiwa kwenye dialysis au kwenye chemotherapy au radiotherapy, nakosa jibu.
Ninapoenda MOI nakuona wagonjwa waliovunjika nyonga na miguu kwa ajali mbali mbali za barabarani au kwa kukatwa katwa mapanga na wezi au majambazi, nakosa jibu.
Ninapopita barabarani nakuona mtu akiwa hana pesa ya kula na mimi nimefuga afutatu kwenye wallet au bank, naishiwa jibu.
Naam, Nimrudishie BWANA nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? (Zaburi ya 116: 12-14).
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. (Zaburi ya 103: 1-2).