Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, afya njema na ulinzi wake wa daima

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Kila niamkapo asubuhi naihoji nafsi yangu nilikua wapi? Nakosa jibu.

Ninapoaanza kunyanyua mwili wangu nasikilizia utimamu wa afya yangu ninajiuliza, ni kipi kinachonistahilisha afya hii njema, ili hali nimekua nikila junk food regularly na kulala na balimi kumi kichwani kila siku na kufika nyumbani salama. Nakosa jibu.

Ninapofungua mlango wa nyumba yangu, na kutazama mali zangu zilivyo salama ili hali niko katikati ya wanyang'anyi na mbwa mwitu. Nakosa jibu.

Ninapowasha simu yangu na kupokea habari za misiba na michango ya misiba kwenye ma-group mbali mbali nakosa jibu.

Ninapoenda Muhimbili au Ocean Road nakuona watoto wadogo wakiwa kwenye dialysis au kwenye chemotherapy au radiotherapy, nakosa jibu.

Ninapoenda MOI nakuona wagonjwa waliovunjika nyonga na miguu kwa ajali mbali mbali za barabarani au kwa kukatwa katwa mapanga na wezi au majambazi, nakosa jibu.

Ninapopita barabarani nakuona mtu akiwa hana pesa ya kula na mimi nimefuga afutatu kwenye wallet au bank, naishiwa jibu.

Naam, Nimrudishie BWANA nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? (Zaburi ya 116: 12-14).

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. (Zaburi ya 103: 1-2).

 
Kukosa kwako jibu ndiyo unatumia hilo gape la knowledge kufulfill delusion uliyonayo.

Huyo Mungu unayemsema wewe ni chaka lako kujificha unapoishiwa maarifa tu.
Kwasababu in reality huyo Mungu hayupo
 
Haleluyah.!

God is so good.
 
Wakati wewe umeamka na kumshukuru Mungu wako, huyu huyo Mungu ameruhusu mwenzako awe pale Mloganzila akipambania oxygen. Yaani huyo huyo Mungu anayeruhusu nitambe mtaani kwa afya ya kutosha, huyo huyo ameruhusu mtu apate ajali agongwe na gari afe hapo hapo.

The mystery of LIFE is unexplainable!!
 
inafikirisha sana....

nakumbuka kipindi niko o-level kuna mwanafunzi mmoja alikua nyuma yangu darasa moja, alikua na umri wa miaka 15.... aliugua ghafla akawa hahudhurii masomo, mpaka ikafikia hatua ya kulazwa....
Aligundulika na cancer ya ubongo, walitaka kumpeleka nje kumfanyia upasuaji lakini hakuchukua mda alifariki hapahapa tz.....
Alikua ndo mtoto wa pekee kwa wazazi wake....

Hili tukio hadi leo hii nikilikumbuka linanifanya nifikirie mambo mazito sana....
 
Kazi ya Mungu haina makosa
 
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiewe (Ayubu 1: 21-22)
 
amina
 
Yeyote mwenye akili timamu hakosi cha kumshukuru Mungu.

Hongera! Una akili nzuri!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…