Tuna ma-commando wazuri, lakini je tuna Rapid Response Force?

Tuna ma-commando wazuri, lakini je tuna Rapid Response Force?

Mkuu RRU si kwa ajili ya ugaidi tu ni kwa ajili ya maafa ya aina nyingi. Mara nyingi mazingira na matukio ndiyo huwalazimisha kujenga vitengo hivyo. Hebu tujifunze katika maafa yaliowahi kutokea nyuma kama mafuriko, ajali ya treni na kadhalika.Baada ya matukio ripoti zimeandikwa zikiwa na mapendekezo mbalimbali lakini zimefungiwa makabatini. Wenzetu pia baada ya kupata maafa mara kwa mara ndiyo wameweza kujenga vitengo hivyo na kuwa imara sana kwa sababu operesheni moja ndiyo inakupa uzoefu mzuri wa kufanya operesheni nyingine. Ndiyo maana kila linapotokea janga lolote wanajeshi ndiyo hupelekwa mbele bila kujali janga hilo linahusiana na nini na wala hawajui wanajeshi wamejifunza nini katika uokoaji. Hebu kwanza tujenge kikosi cha uokoaji na kupmbana na moto ndiyo tufike kwenye kupambana na ugaidi
Mkuu kulingana na mtoa mada, ikosi kinachoongelewa hapa ni cha mapambano na magaidi.
Nakubaliana kwamba hata kikosi cha maafa hapa Tnanzania hatuna zaidi ya kutumia wanajeshi kwa kazi ambayo hawakujifunza.

Hata hivyo hapa tujadili kikosi ambacho inaweza kujibu moto kwa moto na kuteketeza adui aina ya terrorist, a.k.a Al Shabab.
 
Kikosi kipo. Ondoeni hofu. Imaaa imaaaaa.. Tanzaniaaaaaaaaaaaaa
labda unaongelea askari wa kutuliza ghasia/maandamano(FFU).lakini kama unaongelea elite rapid reponse unit,tz hatuna.tusijitwishe sifa za kijinga.
 
Mkuu ufahamu wangu mdogo unaniambia kuna CRT ( Crisis Response Team) yenye wapiganaji toka FFU, formed in 2006, trained in the US unazungumzia kipi tena mkuu, ila kama ni komandos kama ulivyoweka katika hiyo picha hiyo itakua issue nyingine.

CRT wako vizuri sana
 
Mkuu ufahamu wangu mdogo unaniambia kuna CRT ( Crisis Response Team) yenye wapiganaji toka FFU, formed in 2006,

trained in the US unazungumzia kipi tena mkuu, ila kama ni komandos kama ulivyoweka katika hiyo picha hiyo itakua issue nyingine.

CRT ni criminal resistance team miongoni mwao ni hawa tigo
 
CRT ni criminal resistance team miongoni mwao ni hawa tigo

CRT-Crisis Response Team hii ni kikosi maalum chenye mchanganyiko wa wapiganaji either TPDF and TPF-FFU wana training ya kutosha hivyo wajinga na wapumbavu wote wa al- shabaab na washenzi wengine this is TANZANIA never do anything watakufa wao na sio watanzania
 
PRESIDENT’S OFFICE,

------STATE HOUSE,

--------------1 BARACK OBAMA ROAD,--

11400 DAR ES SALAAM.

Tanzania.

-

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Majeshi Maalum-(Special Forces)-ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35 vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa na ufanisi wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa vizuri.

Kwa--mujibu wa Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania na jeshi lake ni nchi pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake miongoni mwa majeshi bora duniani.

Chini ya kichwa cha habari-“35 Most Badass Elite Fighting Units from Around the World”-mwandishi, Micky Wren anaandika kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani, yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa, yana silaha za kisasa kabisa, yameandaliwa vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi na yenye uwezo kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia kumaliza uhuni wa utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo mkubwa.

Mwandishi anasema kuwa orodha hiyo haikupangwa kwa mtitiriko wa uwezo wa kijeshi--wa kila kikundi.-

Vikosi vilivyoko kwenye orodha hiyo ni kile cha Seal cha Jeshi la Maji la Marekani, SAS cha Jeshi la Uingereza, Huntsmen Corps cha Majeshi Maalum ya Denmark, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Kikosi cha MARSOC, Majeshi Maalum ya Taiwan ambayo yanatumia kinga za usoni zisizoweza kuingiliwa na risasi na Kikosi cha Irish Army Rangers cha Jamhuri ya Ireland.

Vingine ni Gendarmerie cha Serbia, Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Ugaidi cha JTF2 cha Canada, Majeshi Maalum ya Uholanzi, Kikosi cha SBS, Majeshi Maalum ya Jamhuri ya Korea, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Majeshi Maalum ya Ubelgiji, Kikosi cha MJK cha Norway, Canadian Joint Response Unit cha Canada, Majeshi Maalum ya Norway, Kikosi cha French Commando Marine, Majeshi Maalum ya New Zealand, Kikosi cha Norwegian Armed Forces Special Command na Kikosi cha Polish Grom cha Poland.

Vingine ni Kikosi cha US Army Special Forces Sniper with Remington Modular Sniper Rifle, Majeshi Maalum ya Marekani, Majeshi Maalum ya Indonesia, Majeshi Maalum ya Romania, Kikosi cha SASR cha Australia, Kikosi cha KSK cha Ujerumani, Majeshi Maalum ya Ujerumani, Majeshi Maalum ya Israel – Shayetet 13, Majeshi Maalum ya Urusi – Spetsnaz, Majeshi Maalum ya Austria – Jagdkommando, Majeshi Maalum ya Iraq, Majeshi Maalum ya Ujerumani ya SEK-M na Majeshi Maalum ya Peru.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU

DAR ES SALAAM

3 Julai, 2014

Habari Maelezo-at-Wednesday, July 02, 2014
 
mkuu
imara is a general term.be specific,wako imara ku-respond na kukabiliana na matukio ya kigaidi na ya ghafla kama ya le ya westgate/garissa university?.tusidanganyane hapa,jwtz ijipange.

Wewe unaweza sema ni general term... Lakini sisi tunajua tuko vipi
 
hamna kitu.

Sawa mkuu.. Uoga wa matukio ya ugaidi ndo unakufanya useme hivi, lakini kuna mambo yanahitaji ufafanuzi toka kwa msemaji wa Jw... Sisi tutapambana kwaajili ya waTz wote, hofu ya nini mkuu!?
 
Sawa mkuu.. Uoga wa matukio ya ugaidi ndo unakufanya useme hivi, lakini kuna mambo yanahitaji ufafanuzi toka kwa msemaji wa Jw... Sisi tutapambana kwaajili ya waTz wote, hofu ya nini mkuu!?
Mkuu mi sina wasi wasi kama kikosi kama hicho kipo na ni sehemu ya Jei Waa.
Lakini kama mmoja alivosema hapo juu ni hawa Tigo tunao wafahamu, basi imani yangu ina yoyoma.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Jeshi letu la JWTZ lina ma-commando wazuri, na matokeo ya kujinoa kwao yameonekana hivi majuzi Comoro na hata DRC-Congo..............

naomba usidanganyike kabisa kwamba eti una makomandoo wazuri. Wako wapi? Ni ile ile hadithi ya polisi wetu na hata hao wa huko Kenya. Wanahangaika kutisha raia kwa kuwa wana mikanda ya chuma na bunduki, lakini subiri wakutane na Al Shabaab, weeee! Hapo ndo utajua kwamba ni wadhaifu. Hawana lolote.

utakuwaje komando wa maana wakati unakula ugali na nyama kila siku na kuongeza maharage. Bahati mbaya utotoni makuzi ndo hayo, unaishia kukomaa miguu na fuvu la kichwa tu! Brain hoi!
 
Wewe hukuona walivyopasua matofali kwa kichwa? Hata John Rambo hawezi ile
 
Hivi wewe umekulia na kuishi bongo au ndo umekuja juzi baada ya baba yako kustaafu toka thuko nje?
naomba usidanganyike kabisa kwamba eti una makomandoo wazuri. Wako wapi? Ni ile ile hadithi ya polisi wetu na hata hao wa huko Kenya. Wanahangaika kutisha raia kwa kuwa wana mikanda ya chuma na bunduki, lakini subiri wakutane na Al Shabaab, weeee! Hapo ndo utajua kwamba ni wadhaifu. Hawana lolotte.

utakuwaje komando wa maana wakati unakula ugali na nyama kila siku na kuongeza maharage. Bahati mbaya utotoni makuzi ndo hayo, unaishia kukomaa miguu na fuvu la kichwa tu! Brain hoi!
 
Wewe hukuona walivyopasua matofali kwa kichwa? Hata John Rambo hawezi ile

si umeona askari wa iraqi wakipiga za Rambo lakini ISIS walipoingia jamaa wanatimua kama wezi wa njiwa?
 
Hivi wewe umekulia na kuishi bongo au ndo umekuja juzi baada ya baba yako kustaafu toka thuko nje?

Kwani bongo kuna nini kitakachonifanya nisifu watu ninaowafahamu udhaifu wao? Au ile patriotism? Huwezi kushinda kwa kushangiliwa tu. Tuwe na fact maana mifano yenu eti ni comoro na drc.

Ziko nchi zina komando wa kueleweka bhana. Uliza Angola ndo utawajua komando wanafanya nini.
 
Ha ha
Sikuwa nimekosea, pengine asiyeujua muziki wa JW ni watu kama ninyi, wabongo wa kusingiziwa!!
Kwa umri wako kama huujui, basi huna haja ya kuhadithiwa, maana utaendelea kutoelewa.

Ila mkirudi toka majuu na visuruali kata-K, jitahidini basi ingalao mgambo kuitoa kutu za huko majuu.
 
Kwani bongo kuna nini kitakachonifanya nisifu watu ninaowafahamu udhaifu wao? Au ile patriotism? Huwezi kushinda kwa kushangiliwa tu. Tuwe na fact maana mifano yenu eti ni comoro na drc.

Ziko nchi zina komando wa kueleweka bhana. Uliza Angola ndo utawajua komando wanafanya nini.

Hebu weka mifano ya Angola mkuu MchunguZI
 
Last edited by a moderator:
Hahaa..hawa kwa ajili ya kupambana na wamachinga wanaouza bangili, hata short guns hazijafanyiwa calibration...
Naomba kuishia hapo nisije nikahukumiwa through cyber crime act ya mwaka 2015...

Short guns gani tena??!!. . . . . . .
We calibration unaona kitu kikubwa sana??!!!

Unaulizia special forces halafu unataka habari ziwepo tu . . . . . .
 
Back
Top Bottom