Ni ukweli usiopingika kuwa Jeshi letu la JWTZ lina ma-commando wazuri, na matokeo ya kujinoa kwao yameonekana hivi majuzi Comoro na hata DRC-Congo.
Lakini matukio ya hivi majuzi huko Garissa yamefanya nijiulize vizuri pointed questions.
Kenya kweli wana vifaa vizuri tu kama sisi.
Lakini response kwa shambulio la majahili ya AlShabab imewachukua muda mrefu sana kufika eneo la tukio na hata kuwa na tactical initiative ya situation yenyewe, yaaani kuiweka sehemu ya mapambano chini ya control hata kama majahili hawajauliwa/kutekwa.
Najua commando anafanya kazi yake vizuri eneo la vita, na yeye kazi yake kubwa ni kuteka/kuconfuse adui ili hatimae regular forces walidhibiti eneo.
Lanini hapa tuna eneo la mapambano NDANI ya eneo ambalo ni huru, yaani walengwa wa kutekwa au kuuliwa na maadui ndio hao tunaotakiwa kuwaokoa, ikiwa ni pamoja na kuua/kudhibiti majahili kama Al Shabab.
Na hilo ndo lengo la swali langu.
Marekani wana SWAT, India wana Anti -Terrorist Squad, New Zealand wana STG-Special Tactics Group, Pakistan wana RATS-Rangers AntiTerror Squad.
Hili si swala la Kova , ni kubwa zaidi.