Tuna Tatizo la Uwezo wa Uendeshaji Uchumi Wetu?. TAZARA Asante Mchina, Vipi Mingine? Hatutafika Mahali Tukahitaji Kusaidiwa Hadi Ikulu Yetu?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Hii ni makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Gazeti la NIPASHE la leo
Screenshot_20240908-081339_Rifaly.jpg

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa ambazo huwa na maswali yakifuatiwa na hoja halafu jibu utatoa wewe mwenyewe.

Hoja ya leo ni je kuna uwezekano sisi Watanzania tuna tatizo la uwezo wa uendeshaji wa baadhi ya miradi mikubwa ya kiuchumi ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu?. Tumshukuru Mchina kutushika mkono kwenye hili la reli ya TAZARA vipi miradi mingine na taasisi nyingine tegemewa zinazo sua sua?. Tuna matatizo gani ya kushindwa kuendesha miradi yetu tegemewa kwa faida?. Je huko mbele tukifanya utafiti wa uendeshaji wa Ikulu yetu, serikali yetu, Bunge letu na Mahakama zetu, tukajikuta kote ni matatizo matupu, hakuna uwezekano tukafika mahali tukajikua tukahitaji kusaidiwa hadi kuendesha Ikulu Yetu?.

Najua hili la kusaidiwa kuendesha Ikulu yetu litawaogopesha maana Ikulu ya nchi ndio roho ya nchi, lakini kama kuna vitu sisi wenyewe tunashindwa, kuna ubaya gani kusaidiwa?. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Mfano mzuri wa Watanzania kusaidiwa kitu Ikulu yetu ni kwenye kuhamasisha utalii,
Nimebahatika kufika Africa Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda Mauritius, Seychelles, Misri, ukiangalia vivutio vyao vya utalii ukilinganisha na vyetu, hawatufikii hata nusu!, lakini ukiangalia idadi ya watalii wanatuzidi sana, sababu ni sisi tumeshindwa kuutangaza utalii wetu kikamilifu. Rais Samia alipoingia madarakani, akatokea mfadhili fulani akaifadhili ikulu yetu na Rais wetu kwa kuandaa filamu ya Royal Tour na kugharimia uzinduzi wake nchini Marekani, sasa utalii unashamiri, hivyo hakuna ajabu yoyote kusaidiwa popote hadi Ikulu!.

Wiki hii kumepatikana habari njema kwenye ziara ya Rais Samia nchini China, China imekubali kufanya ukarabati wa Reli ya TAZARA na kutusaidia kuiendesha kwa faida.

Taarifa hii ni habari njema kwa Watanzania, zinazothibitisha China sio tuu ni mshirika mzuri wa Tanzania katika ujenzi wa miundombinu, bali pia ni rafiki wa kweli, kwa kutusaidia misaada bila masharti magumu ya kuingilia uhuru wetu.

Ni China ndio aliijenga reli ya TAZARA, tena hadi vibarua wote ni kutoka China, na baada ya ujenzi, ukiondoa wale waliofia nchini na kuzikwa nchini, wengine wote waliondoka kurejea kwao.

Reli ya Kati ilijengwa na Ujerumani na kumaliziwa na Uingereza, vibarua walitoka India, na baada ya reli kukamilika vibarua hao walilowea Tanzania, na ndio hawa Wahindi waliopo ambao walijenga uhindini kwenye kila miji mikuu reli ilipopita.

Reli ya TAZARA ndio reli pekee ya Uhuru iliyojengwa baada ya Tanzania kupata uhuru, kazi ngumu kabisa katika ujenzi wa reli, sio kutandika mataruma, kazi kubwa ni kufanya upembuzi yakinifu na kuchoronga na kuchanja njia ya kutandika hayo mataruma, hata ujenzi wa SGR, upembuzi yakinifu na kuchanja au kuchoronga njia ulikuwa ni kwa mserereko tuu wa Reli ya Kati kwa kupita mule mule kama tuu kujaladia reli mpya kwenye njia ile ile ya Reli ya Kati.

Usafiri wa reli ndio usafiri wa gharama nafuu kabisa baada ya usafiri wa meli, na reli ndio usafiri wenye uwezo wa kusafirisha abiria wengi na mizigo mingi kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu.

Kati ya mipaka yote nchini Tanzania, mpaka wa Tunduma ndio mpaka unaongoza kwa kuwa bize, kutokana na malori ya mizigo inayokwenda Zambia kutokea bandari ya Dar es Salaam.

Reli ya TAZARA sio tuu ilisaidia sana kubeba mizigo ya Zambia na nchi jirani, za Kusini mwa Tanzania, bali ilisaidia kuokoa barabara zetu na kupunguza msongomano mpaka wa Tunduma.

Kitendo cha reli ya TAZARA kulega lega, kumepelekea mizigo ya Zambia na nchi za Kusini kusafirishwa kwa malori, hivyo kuharibu barabara, kuleta msongamano mpaka wa Tunduma, mizigo ya watu kuchelewa, na ngarama za usafirishaji kuwa juu, hali iliyopelekea jirani yetu Zambia kuamua kutumia bandari ya Msumbiji ambayo iko mbali zaidi, hivyo maboresho ya TAZARA ni habari njema sana kwa Tanzania.

Swali la kujiuliza, tulifikaje huko hadi TAZARA kushindwa kujiendesha kwa faida?. Na sio TAZARA tuu, hata TAZAMA, hata TIPPER, hata ATC, hata Reli ya Kati, NASACO, TCFB, UDA, KAMATA, DMT, Bandari, TANESCO, TTCL, hata POSTA ina chechemea!.

Hivi Tanzania kama taifa, tumewahi kukaa chini na kutafakari, tunakwama wapi?, nini kinachotukwamisha?.
Siku zote kisingizio kikubwa ni mtaji!, nimesema ni kisingizio tuu kwasababu kama ni mtaji, mbona tunakopa sana na serikali inatoa fedha nyingi kuyabeba mashirika yake na mfano mzuri ni Shirika la Ndege la Tanzania, ATCL, limepewa ndege mpya za kutosha tuu, limepewa mtaji mkubwa tuu wa kutosha lakini bado linaendeshwa kwa hasara!.

Hii reli ya SGR tunayoishangilia sana hii ruti ya DAR-Dodoma kupitia Morogoro, subirieni taarifa ya ukaguzi ya CAG mwakani!. Reli ya SGR haiwezi kujiendesha kwa faida kwa kubeba abiria, ubebaji abiria kwenye SGR ni huduma tuu, services, faida ya SGR ni kubeba mzigo wa kushiba!.

Wakati awamu wa JK wakipanga kujenga SGR pia walipanga ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kuipatia SGR yetu mzigo wa kushiba, mzigo unaipitia bandari ya Dar es Salaam, hauwezi kuishibisha SGR ikajiendesha kwa faida!. Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...

Hata uendeshaji wa reli ya kati, tuna matatizo!, faida kubwa ya bandari ya Dar es Salaam ni mizigo ya jirani zetu inayopita kwetu (transit goods), tukajenga bandari kavu ya Isaka ili mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC, ikifika tuu Dar Port, inapakiwa kwenye meli na kukimbizwa Isaka, malori ya Rwanda, Burundi na DRC, wataikusanyia pale. Mara ya mwisho nimepita pale Isaka, hakuna crane ya kushusha mizigo toka kwenye treni, hivyo hakuna mzigo unashushwa Isaka, yale maghala ya TRC, yamekodishwa kwa Bakhresa.

Kwenye kikao kazi cha Ofisi ya Msajili wa Hazina na watendaji wakuu wa mashiriki ya umma, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, aliyataja mashirika 40 ya umma ambayo ni mizigo, akapendekeza yafutwe!, huu ni uthibitisho sisi Watanzania tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya taasisi, lakini zikibinafshishwa, zinashamiri. Hili tumelishuhudia kwenye TBL na Sigara, TCC.

Wakati wa kelele za ubinafsishaji wa bandari, tulishauri, kitu cha kwanza kwa sisi Watanzania, ni kujitathmini tunakwama wapi?, tukijigundua tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya miradi, kwanza tukubali makosa, kisha tutafute ufumbuzi, na ikitokea ufumbuzi wa baadhi ya matatizo yetu yatahitaji kusaidiwa, hakuna ubaya kuomba msaada kusaidiwa, kuna nchi zinasaidiwa kuendesha baadhi ya miradi yake, na sasa kwa kadri dunia inavyobadilika kidigitali, utafika wakati tunaweza hata kujikuta tukaikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji kuiendesha kwa faida!. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?

Kwenye hili la kuikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji atuendeshee, mnaweza kudhani ninatania!, mwenzenu nimebahatika kufika ikulu mbalimbalimbali za wenzetu duniani ikiwemo ikulu ya Afrika Kusini, Ikulu ya White House, St. Peters Basilika pale Roma, Buckemham Palace Uingereza, ikulu, ni eneo la kivutio cha watalii, mfano mdogo ni angalia jingo la Beit Al Ajab Zanzibar.

Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa, tulikuwa tunapita kule nyuma ya Ikulu kwenda Feri, enzi za JK, kumefungwa eti ni kiusalama!, JPM alipoingia amepapendezesha Ikulu kwa kujaza wanyama na kuzalisha tausi, yote haya ni ya nini kama Ikulu inafungwa?.

Kwa vile sasa ikulu imehamia Dodoma, hakuna ubaya ikulu ya Dar es Salaam ikafunguliwa kwa utalii, sio tuu tutazalisha mapato mengi bali ikulu ndio kitakuwa kivutio number moja cha utalii wa ndani, kila atakayetembelea ikulu, atapitishwa Makumbusho ya Taifa, na kuishia kupumzika pale Botanic Garden, hata hili linasubiri mwekezaji ajitokeze aandike andiko?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
 
Mtu mweusi aliumbwa kuharibu kila kitu, kuanzia kukata miti hovyo, kuharibu miundombinu, wakati mtu mweupe aliumbwa kujenga , kutunza na kuendeleza kila kitu, ufanisi Kwa mtu mweusi ni tatizo la kiasili Kwa sababu ya akili ndogo, wakati wenzetu hufanya hata ukarabati wa nyumba zao mara Kwa mara, sisi ukijenga umemaliza milele, hivo nature ndio hutesa kuanzia viongozi hadi wananchi wa kawaida,
 
Sijasoma lakini nimeelewa kupitia kichwa cha habari.

Hauwezi kuendelea kwa kumonopolize utendaji kwa kundi fulani la watu na sio kushirikisha akili za watu wote katika Taifa.
Mpaka sasa Taifa linaendeshwa kisiasa na siasa ndio ajira pekee inayolipa matokeo yake muda na gharama kubwa hutumika kuhudumia wanasiasa na inner circle yao.

Siasa siasa siasa kila mahala na sio mifumo imara yenye malengo yakujenga Taifa na ustawi wa watu wake.
CCM wanaweza zaidi kutawala kuliko kuboresha uchumi wa Taifa na ustawi wa watu wake matokeo yake production force, skills na minds hazipo zaidi ya muda mwingi kufikiria ni namna gani Chama kitaendelea kutawala na kundi fulani la watu liweze kuishi maana lenyewe ndio lenye hati miliki ya nchi hii.

Ili Taifa hili mabadiriko yaje na watu wawe na akili yakujitegemea na kufanya kazi Kwa bidii Kwa maendeleo ya nchi hii basi CCM lazima itoke madarakani na Uhuru/mapinduzi/ukombozi vipatikane kupitia mkono ya raia wenyewe sio vyama vya siasa.
Elites/CCM oligarch wakitoka kwenye mifumo basi Taifa litakuwa huru na tutashuhudia akili mpya za kimapinduzi.
 
Mtu mweusi aliumbwa kuharibu kila kitu, kuanzia kukata miti hovyo, kuharibu miundombinu, wakati mtu mweupe aliumbwa kujenga , kutunza na kuendeleza kila kitu, ufanisi Kwa mtu mweusi ni tatizo la kiasili Kwa sababu ya akili ndogo, wakati wenzetu hufanya hata ukarabati wa nyumba zao mara Kwa mara, sisi ukijenga umemaliza milele, hivo nature ndio hutesa kuanzia viongozi hadi wananchi wa kawaida,

Muwe mnasoma historia. Uharibifu uliofanywa na unaofanywa na mizungu weusi hawafikii hata robo. Sasa mizungu inachafua space kuna debris in space, wamatumbi gani wamewahi kuchafua space?
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Gazeti la NIPASHE la leo
View attachment 3089972

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa ambazo huwa na maswali yakifuatiwa na hoja halafu jibu utatoa wewe mwenyewe.

Hoja ya leo ni je kuna uwezekano sisi Watanzania tuna tatizo la uwezo wa uendeshaji wa baadhi ya miradi mikubwa ya kiuchumi ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu?. Tumshukuru Mchina kutushika mkono kwenye hili la reli ya TAZARA vipi miradi mingine na taasisi nyingine tegemewa zinazo sua sua?. Tuna matatizo gani ya kushindwa kuendesha miradi yetu tegemewa kwa faida?. Je huko mbele tukifanya utafiti wa uendeshaji wa Ikulu yetu, serikali yetu, Bunge letu na Mahakama zetu, tukajikuta kote ni matatizo matupu, hakuna uwezekano tukafika mahali tukajikua tukahitaji kusaidiwa hadi kuendesha Ikulu Yetu?.

Najua hili la kusaidiwa kuendesha Ikulu yetu litawaogopesha maana Ikulu ya nchi ndio roho ya nchi, lakini kama kuna vitu sisi wenyewe tunashindwa, kuna ubaya gani kusaidiwa?. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Mfano mzuri wa Watanzania kusaidiwa kitu Ikulu yetu ni kwenye kuhamasisha utalii,
Nimebahatika kufika Africa Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda Mauritius, Seychelles, Misri, ukiangalia vivutio vyao vya utalii ukilinganisha na vyetu, hawatufikii hata nusu!, lakini ukiangalia idadi ya watalii wanatuzidi sana, sababu ni sisi tumeshindwa kuutangaza utalii wetu kikamilifu. Rais Samia alipoingia madarakani, akatokea mfadhili fulani akaifadhili ikulu yetu na Rais wetu kwa kuandaa filamu ya Royal Tour na kugharimia uzinduzi wake nchini Marekani, sasa utalii unashamiri, hivyo hakuna ajabu yoyote kusaidiwa popote hadi Ikulu!.

Wiki hii kumepatikana habari njema kwenye ziara ya Rais Samia nchini China, China imekubali kufanya ukarabati wa Reli ya TAZARA na kutusaidia kuiendesha kwa faida.

Taarifa hii ni habari njema kwa Watanzania, zinazothibitisha China sio tuu ni mshirika mzuri wa Tanzania katika ujenzi wa miundombinu, bali pia ni rafiki wa kweli, kwa kutusaidia misaada bila masharti magumu ya kuingilia uhuru wetu.

Ni China ndio aliijenga reli ya TAZARA, tena hadi vibarua wote ni kutoka China, na baada ya ujenzi, ukiondoa wale waliofia nchini na kuzikwa nchini, wengine wote waliondoka kurejea kwao.

Reli ya Kati ilijengwa na Ujerumani na kumaliziwa na Uingereza, vibarua walitoka India, na baada ya reli kukamilika vibarua hao walilowea Tanzania, na ndio hawa Wahindi waliopo ambao walijenga uhindini kwenye kila miji mikuu reli ilipopita.

Reli ya TAZARA ndio reli pekee ya Uhuru iliyojengwa baada ya Tanzania kupata uhuru, kazi ngumu kabisa katika ujenzi wa reli, sio kutandika mataruma, kazi kubwa ni kufanya upembuzi yakinifu na kuchoronga na kuchanja njia ya kutandika hayo mataruma, hata ujenzi wa SGR, upembuzi yakinifu na kuchanja au kuchoronga njia ulikuwa ni kwa mserereko tuu wa Reli ya Kati kwa kupita mule mule kama tuu kujaladia reli mpya kwenye njia ile ile ya Reli ya Kati.

Usafiri wa reli ndio usafiri wa gharama nafuu kabisa baada ya usafiri wa meli, na reli ndio usafiri wenye uwezo wa kusafirisha abiria wengi na mizigo mingi kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu.

Kati ya mipaka yote nchini Tanzania, mpaka wa Tunduma ndio mpaka unaongoza kwa kuwa bize, kutokana na malori ya mizigo inayokwenda Zambia kutokea bandari ya Dar es Salaam.

Reli ya TAZARA sio tuu ilisaidia sana kubeba mizigo ya Zambia na nchi jirani, za Kusini mwa Tanzania, bali ilisaidia kuokoa barabara zetu na kupunguza msongomano mpaka wa Tunduma.

Kitendo cha reli ya TAZARA kulega lega, kumepelekea mizigo ya Zambia na nchi za Kusini kusafirishwa kwa malori, hivyo kuharibu barabara, kuleta msongamano mpaka wa Tunduma, mizigo ya watu kuchelewa, na ngarama za usafirishaji kuwa juu, hali iliyopelekea jirani yetu Zambia kuamua kutumia bandari ya Msumbiji ambayo iko mbali zaidi, hivyo maboresho ya TAZARA ni habari njema sana kwa Tanzania.

Swali la kujiuliza, tulifikaje huko hadi TAZARA kushindwa kujiendesha kwa faida?. Na sio TAZARA tuu, hata TAZAMA, hata TIPPER, hata ATC, hata Reli ya Kati, NASACO, TCFB, UDA, KAMATA, DMT, Bandari, TANESCO, TTCL, hata POSTA ina chechemea!.

Hivi Tanzania kama taifa, tumewahi kukaa chini na kutafakari, tunakwama wapi?, nini kinachotukwamisha?.
Siku zote kisingizio kikubwa ni mtaji!, nimesema ni kisingizio tuu kwasababu kama ni mtaji, mbona tunakopa sana na serikali inatoa fedha nyingi kuyabeba mashirika yake na mfano mzuri ni Shirika la Ndege la Tanzania, ATCL, limepewa ndege mpya za kutosha tuu, limepewa mtaji mkubwa tuu wa kutosha lakini bado linaendeshwa kwa hasara!.

Hii reli ya SGR tunayoishangilia sana hii ruti ya DAR-Dodoma kupitia Morogoro, subirieni taarifa ya ukaguzi ya CAG mwakani!. Reli ya SGR haiwezi kujiendesha kwa faida kwa kubeba abiria, ubebaji abiria kwenye SGR ni huduma tuu, services, faida ya SGR ni kubeba mzigo wa kushiba!.

Wakati awamu wa JK wakipanga kujenga SGR pia walipanga ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kuipatia SGR yetu mzigo wa kushiba, mzigo unaipitia bandari ya Dar es Salaam, hauwezi kuishibisha SGR ikajiendesha kwa faida!. Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...

Hata uendeshaji wa reli ya kati, tuna matatizo!, faida kubwa ya bandari ya Dar es Salaam ni mizigo ya jirani zetu inayopita kwetu (transit goods), tukajenga bandari kavu ya Isaka ili mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC, ikifika tuu Dar Port, inapakiwa kwenye meli na kukimbizwa Isaka, malori ya Rwanda, Burundi na DRC, wataikusanyia pale. Mara ya mwisho nimepita pale Isaka, hakuna crane ya kushusha mizigo toka kwenye treni, hivyo hakuna mzigo unashushwa Isaka, yale maghala ya TRC, yamekodishwa kwa Bakhresa.

Kwenye kikao kazi cha Ofisi ya Msajili wa Hazina na watendaji wakuu wa mashiriki ya umma, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, aliyataja mashirika 40 ya umma ambayo ni mizigo, akapendekeza yafutwe!, huu ni uthibitisho sisi Watanzania tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya taasisi, lakini zikibinafshishwa, zinashamiri. Hili tumelishuhudia kwenye TBL na Sigara, TCC.

Wakati wa kelele za ubinafsishaji wa bandari, tulishauri, kitu cha kwanza kwa sisi Watanzania, ni kujitathmini tunakwama wapi?, tukijigundua tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya miradi, kwanza tukubali makosa, kisha tutafute ufumbuzi, na ikitokea ufumbuzi wa baadhi ya matatizo yetu yatahitaji kusaidiwa, hakuna ubaya kuomba msaada kusaidiwa, kuna nchi zinasaidiwa kuendesha baadhi ya miradi yake, na sasa kwa kadri dunia inavyobadilika kidigitali, utafika wakati tunaweza hata kujikuta tukaikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji kuiendesha kwa faida!. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?

Kwenye hili la kuikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji atuendeshee, mnaweza kudhani ninatania!, mwenzenu nimebahatika kufika ikulu mbalimbalimbali za wenzetu duniani ikiwemo ikulu ya Afrika Kusini, Ikulu ya White House, St. Peters Basilika pale Roma, Buckemham Palace Uingereza, ikulu, ni eneo la kivutio cha watalii, mfano mdogo ni angalia jingo la Beit Al Ajab Zanzibar.

Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa, tulikuwa tunapita kule nyuma ya Ikulu kwenda Feri, enzi za JK, kumefungwa eti ni kiusalama!, JPM alipoingia amepapendezesha Ikulu kwa kujaza wanyama na kuzalisha tausi, yote haya ni ya nini kama Ikulu inafungwa?.

Kwa vile sasa ikulu imehamia Dodoma, hakuna ubaya ikulu ya Dar es Salaam ikafunguliwa kwa utalii, sio tuu tutazalisha mapato mengi bali ikulu ndio kitakuwa kivutio number moja cha utalii wa ndani, kila atakayetembelea ikulu, atapitishwa Makumbusho ya Taifa, na kuishia kupumzika pale Botanic Garden, hata hili linasubiri mwekezaji ajitokeze aandike andiko?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
Ramli chonganishi?
 
Back
Top Bottom