Tuna Tatizo la Uwezo wa Uendeshaji Uchumi Wetu?. TAZARA Asante Mchina, Vipi Mingine? Hatutafika Mahali Tukahitaji Kusaidiwa Hadi Ikulu Yetu?.

It takes a lot of courage to fight biases and oppressive regimes, but it takes even greater courage to admit ignorance and venture into the unknown. Secular education teaches us that if we don’t know something, we shouldn’t be afraid of acknowledging our ignorance and looking for new evidence. Even if we think we know something, we shouldn’t be afraid of doubting our opinions and checking ourselves again. Many people are afraid of the unknown, and want clear-cut answers for every question. Fear of the unknown can paralyse us more than any tyrant. People throughout history worried that unless we put all our faith in some set of absolute answers, human society will crumble. In fact, modern history has demonstrated that a society of courageous people willing to admit ignorance and raise difficult questions is usually not just more prosperous but also more peaceful than societies in which everyone must unquestioningly accept a single answer. People afraid of losing their truth tend to be more violent than people who are used to looking at the world from several different viewpoints. Questions you cannot answer are usually far better for you than answers you cannot question.
Yuval Noah Harari, 21 Lessons for the 21st Century
 
Mtu anaanza na basi moja, miaka kumi ana basi kumi na kampuni imekua, DART wanaanza na basi mia moja, miaka mitatu zimebaki 10 Ambazo ziko barabarani nazo sio nzima, tisini zilishakufa unategemea nini hapo
 
Haya maandiko mjomba mayala kwenye ule utawala wa kambale sikuwah yaona naona utawala huu umeyarudi kuyaaandika. Haya sie tupo ila nyie wadingi ndo mnasababisha hili taifa lisisonge kwa kutowaambia ukweli watawala kwa hofu ya kukosa fungu na unadiriki kusema eti china inatoa msada kwa masharti yasiyo magumu pesa za westerners chungu kwa sababu lazima wazifuatilie huwez omba pesa za kuanza program za wamama kupunguzq vifo vya watt kipindi wanajifungua ukanunue V8 westerners wako serious na hayo mambo hamtaki ila mchina yeye hajali hata mkitiana shaba ilimradi yake yanaenda its f*****in wanking kwa kweli ....uwe na weekend njema.
 
Gharama za kupeleka zile convoy china, wangecheza kibati wakawa wanapeana pesa wao kwa wao wangetoboa, wamepeleka china pesa kubwa sana sana Kwa ahadi ya USD 50b
 
Tatizo ni aina ya Viongozi tunaowachagua na Check and balance, wakivurunda wanajua watahamishwa au kupewa promotion kabisa. Hao hao uwapeleka Rwanda au Singapore wangeweza kuwa viongozi wazuri tu, sababu hawapewi nafasi kufanya ujinga na wakifanya ujinga adhabu ni kali na hazikwepeki.

Tatizo ni viongozi hapa Tanzania hauko serious na mali za umma.
 
Bado namkumbuka professor Lumumba wa Kenya "we elect fools to the office ". Huenda meneja wa hilo shirika aliingia kiundugu au kwa rushwa.
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Gazeti la NIPASHE la leo
View attachment 3089972

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa ambazo huwa na maswali yakifuatiwa na hoja halafu jibu utatoa wewe mwenyewe.

Hoja ya leo ni je kuna uwezekano sisi Watanzania tuna tatizo la uwezo wa uendeshaji wa baadhi ya miradi mikubwa ya kiuchumi ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu?. Tumshukuru Mchina kutushika mkono kwenye hili la reli ya TAZARA vipi miradi mingine na taasisi nyingine tegemewa zinazo sua sua?. Tuna matatizo gani ya kushindwa kuendesha miradi yetu tegemewa kwa faida?. Je huko mbele tukifanya utafiti wa uendeshaji wa Ikulu yetu, serikali yetu, Bunge letu na Mahakama zetu, tukajikuta kote ni matatizo matupu, hakuna uwezekano tukafika mahali tukajikua tukahitaji kusaidiwa hadi kuendesha Ikulu Yetu?.

Najua hili la kusaidiwa kuendesha Ikulu yetu litawaogopesha maana Ikulu ya nchi ndio roho ya nchi, lakini kama kuna vitu sisi wenyewe tunashindwa, kuna ubaya gani kusaidiwa?. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Mfano mzuri wa Watanzania kusaidiwa kitu Ikulu yetu ni kwenye kuhamasisha utalii,
Nimebahatika kufika Africa Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda Mauritius, Seychelles, Misri, ukiangalia vivutio vyao vya utalii ukilinganisha na vyetu, hawatufikii hata nusu!, lakini ukiangalia idadi ya watalii wanatuzidi sana, sababu ni sisi tumeshindwa kuutangaza utalii wetu kikamilifu. Rais Samia alipoingia madarakani, akatokea mfadhili fulani akaifadhili ikulu yetu na Rais wetu kwa kuandaa filamu ya Royal Tour na kugharimia uzinduzi wake nchini Marekani, sasa utalii unashamiri, hivyo hakuna ajabu yoyote kusaidiwa popote hadi Ikulu!.

Wiki hii kumepatikana habari njema kwenye ziara ya Rais Samia nchini China, China imekubali kufanya ukarabati wa Reli ya TAZARA na kutusaidia kuiendesha kwa faida.

Taarifa hii ni habari njema kwa Watanzania, zinazothibitisha China sio tuu ni mshirika mzuri wa Tanzania katika ujenzi wa miundombinu, bali pia ni rafiki wa kweli, kwa kutusaidia misaada bila masharti magumu ya kuingilia uhuru wetu.

Ni China ndio aliijenga reli ya TAZARA, tena hadi vibarua wote ni kutoka China, na baada ya ujenzi, ukiondoa wale waliofia nchini na kuzikwa nchini, wengine wote waliondoka kurejea kwao.

Reli ya Kati ilijengwa na Ujerumani na kumaliziwa na Uingereza, vibarua walitoka India, na baada ya reli kukamilika vibarua hao walilowea Tanzania, na ndio hawa Wahindi waliopo ambao walijenga uhindini kwenye kila miji mikuu reli ilipopita.

Reli ya TAZARA ndio reli pekee ya Uhuru iliyojengwa baada ya Tanzania kupata uhuru, kazi ngumu kabisa katika ujenzi wa reli, sio kutandika mataruma, kazi kubwa ni kufanya upembuzi yakinifu na kuchoronga na kuchanja njia ya kutandika hayo mataruma, hata ujenzi wa SGR, upembuzi yakinifu na kuchanja au kuchoronga njia ulikuwa ni kwa mserereko tuu wa Reli ya Kati kwa kupita mule mule kama tuu kujaladia reli mpya kwenye njia ile ile ya Reli ya Kati.

Usafiri wa reli ndio usafiri wa gharama nafuu kabisa baada ya usafiri wa meli, na reli ndio usafiri wenye uwezo wa kusafirisha abiria wengi na mizigo mingi kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu.

Kati ya mipaka yote nchini Tanzania, mpaka wa Tunduma ndio mpaka unaongoza kwa kuwa bize, kutokana na malori ya mizigo inayokwenda Zambia kutokea bandari ya Dar es Salaam.

Reli ya TAZARA sio tuu ilisaidia sana kubeba mizigo ya Zambia na nchi jirani, za Kusini mwa Tanzania, bali ilisaidia kuokoa barabara zetu na kupunguza msongomano mpaka wa Tunduma.

Kitendo cha reli ya TAZARA kulega lega, kumepelekea mizigo ya Zambia na nchi za Kusini kusafirishwa kwa malori, hivyo kuharibu barabara, kuleta msongamano mpaka wa Tunduma, mizigo ya watu kuchelewa, na ngarama za usafirishaji kuwa juu, hali iliyopelekea jirani yetu Zambia kuamua kutumia bandari ya Msumbiji ambayo iko mbali zaidi, hivyo maboresho ya TAZARA ni habari njema sana kwa Tanzania.

Swali la kujiuliza, tulifikaje huko hadi TAZARA kushindwa kujiendesha kwa faida?. Na sio TAZARA tuu, hata TAZAMA, hata TIPPER, hata ATC, hata Reli ya Kati, NASACO, TCFB, UDA, KAMATA, DMT, Bandari, TANESCO, TTCL, hata POSTA ina chechemea!.

Hivi Tanzania kama taifa, tumewahi kukaa chini na kutafakari, tunakwama wapi?, nini kinachotukwamisha?.
Siku zote kisingizio kikubwa ni mtaji!, nimesema ni kisingizio tuu kwasababu kama ni mtaji, mbona tunakopa sana na serikali inatoa fedha nyingi kuyabeba mashirika yake na mfano mzuri ni Shirika la Ndege la Tanzania, ATCL, limepewa ndege mpya za kutosha tuu, limepewa mtaji mkubwa tuu wa kutosha lakini bado linaendeshwa kwa hasara!.

Hii reli ya SGR tunayoishangilia sana hii ruti ya DAR-Dodoma kupitia Morogoro, subirieni taarifa ya ukaguzi ya CAG mwakani!. Reli ya SGR haiwezi kujiendesha kwa faida kwa kubeba abiria, ubebaji abiria kwenye SGR ni huduma tuu, services, faida ya SGR ni kubeba mzigo wa kushiba!.

Wakati awamu wa JK wakipanga kujenga SGR pia walipanga ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kuipatia SGR yetu mzigo wa kushiba, mzigo unaipitia bandari ya Dar es Salaam, hauwezi kuishibisha SGR ikajiendesha kwa faida!. Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...

Hata uendeshaji wa reli ya kati, tuna matatizo!, faida kubwa ya bandari ya Dar es Salaam ni mizigo ya jirani zetu inayopita kwetu (transit goods), tukajenga bandari kavu ya Isaka ili mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC, ikifika tuu Dar Port, inapakiwa kwenye meli na kukimbizwa Isaka, malori ya Rwanda, Burundi na DRC, wataikusanyia pale. Mara ya mwisho nimepita pale Isaka, hakuna crane ya kushusha mizigo toka kwenye treni, hivyo hakuna mzigo unashushwa Isaka, yale maghala ya TRC, yamekodishwa kwa Bakhresa.

Kwenye kikao kazi cha Ofisi ya Msajili wa Hazina na watendaji wakuu wa mashiriki ya umma, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, aliyataja mashirika 40 ya umma ambayo ni mizigo, akapendekeza yafutwe!, huu ni uthibitisho sisi Watanzania tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya taasisi, lakini zikibinafshishwa, zinashamiri. Hili tumelishuhudia kwenye TBL na Sigara, TCC.

Wakati wa kelele za ubinafsishaji wa bandari, tulishauri, kitu cha kwanza kwa sisi Watanzania, ni kujitathmini tunakwama wapi?, tukijigundua tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya miradi, kwanza tukubali makosa, kisha tutafute ufumbuzi, na ikitokea ufumbuzi wa baadhi ya matatizo yetu yatahitaji kusaidiwa, hakuna ubaya kuomba msaada kusaidiwa, kuna nchi zinasaidiwa kuendesha baadhi ya miradi yake, na sasa kwa kadri dunia inavyobadilika kidigitali, utafika wakati tunaweza hata kujikuta tukaikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji kuiendesha kwa faida!. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?

Kwenye hili la kuikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji atuendeshee, mnaweza kudhani ninatania!, mwenzenu nimebahatika kufika ikulu mbalimbalimbali za wenzetu duniani ikiwemo ikulu ya Afrika Kusini, Ikulu ya White House, St. Peters Basilika pale Roma, Buckemham Palace Uingereza, ikulu, ni eneo la kivutio cha watalii, mfano mdogo ni angalia jingo la Beit Al Ajab Zanzibar.

Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa, tulikuwa tunapita kule nyuma ya Ikulu kwenda Feri, enzi za JK, kumefungwa eti ni kiusalama!, JPM alipoingia amepapendezesha Ikulu kwa kujaza wanyama na kuzalisha tausi, yote haya ni ya nini kama Ikulu inafungwa?.

Kwa vile sasa ikulu imehamia Dodoma, hakuna ubaya ikulu ya Dar es Salaam ikafunguliwa kwa utalii, sio tuu tutazalisha mapato mengi bali ikulu ndio kitakuwa kivutio number moja cha utalii wa ndani, kila atakayetembelea ikulu, atapitishwa Makumbusho ya Taifa, na kuishia kupumzika pale Botanic Garden, hata hili linasubiri mwekezaji ajitokeze aandike andiko?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
Asante kwa mchango wako mzuri mimi naandika kitabu cha ujasiriamali ambacho ni fikirishi ni mjasiriamali pia, darasani tulijifunza kwamba asilimia 80 ya mafanikio kwenye biashara yanategemea mjasiriamali na asilimia 20 ni mjasiriamali na yanayomzunguka, hii asilimia 20 kwa wakati ule, 1986, ilihusika na liseni za biashara, mabango, ushuru wa mazao kama vile ngozi za wanyama tunao wafuga, nitaje kwa ufupi, mwaka 1986-1990, nchi nyingi Afrika zilikuwa zinakusanya mapato toka kwenye biashara kupitia wafanyakazi kwa mfumo unaoitwa pay as you earn kwasasa wafanya biashara wanalipa kodi inayotokana na mauzo ya jumla kwa mfumo wa kodi wa mamlaka husika inayo kusanya kodi.

Baadae nimekuwa nikifuatilia kwa ujumla kwanini biashara zinachangamka na kuto changamka na kwanini zinakufa kumbe kwenye hii asilimia 20 kuna, (factors), kuna vijambo vilivyo jificha, (major environmental factors), ambazo mfanyabiashara ama mtu mmoja mmoja hana mamlaka navyo 1. Maamuzi ya kisiasa political decisions, maamuzi haya huwa na matokeo chanya na hasi kulingana na biashara husika
2. Serikali iliyoko madarakani jinsi ilivyo jipange kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja, ( national economy and social development strategies of an existing government)
3.Aina ya watu, elimu yao na shughuli zao katika jamii, wanao izinguka biashara husika, (social democratic variables)
4. Teknolojia, maandalizi ya kuwezesha kuipokea teknolojia kuna wengine hadi sasa hawezi kufanya muamala kwenye simu, (adaptbility skills and technology changes)

Chanzo kikuu kinasababishwa na jamii zetu kuto kuhoji, kwasababu tumeandaliwa kuto kuhoji, na tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukivihoji utaambiwa kama umekua uondoke matokeo ya zuio la kuhoji kwenye ngazi mbalimbali za maisha kumejenga tabia ya kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani, yaani kuahirisha kufikiri kizalendo
Hitimisho jamii iwe huru kuhoji, kuhoji kunachagiza jamii kuweza kubuni mbinu za kukabiliana na changamoto zilizopo na zitakazo kuja ama kutumia mbinu ambazo tayari zina matokeo chanya

Angalizo changamoto husababishwa na majanga, (natural disasters) lakini chanzo kikuu cha changamoto nyingi kwenye jamii zetu ni binadamu, anaweza kujisababishia changamoto kwa uzembe uvivu ujinga na ushamba ama kuwasababishia wengi kwa kutokujua ama kwa makusudi, inamaana endapo jamii itakaa kimya kuto kubuni mbinu za kukabiliana na changamoto anazo sabisha binadamu basi hii asilimia 20 itaendelea kuwa na nguvu hata ya kuziua biashara
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Gazeti la NIPASHE la leo
View attachment 3089972

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa ambazo huwa na maswali yakifuatiwa na hoja halafu jibu utatoa wewe mwenyewe.

Hoja ya leo ni je kuna uwezekano sisi Watanzania tuna tatizo la uwezo wa uendeshaji wa baadhi ya miradi mikubwa ya kiuchumi ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu?. Tumshukuru Mchina kutushika mkono kwenye hili la reli ya TAZARA vipi miradi mingine na taasisi nyingine tegemewa zinazo sua sua?. Tuna matatizo gani ya kushindwa kuendesha miradi yetu tegemewa kwa faida?. Je huko mbele tukifanya utafiti wa uendeshaji wa Ikulu yetu, serikali yetu, Bunge letu na Mahakama zetu, tukajikuta kote ni matatizo matupu, hakuna uwezekano tukafika mahali tukajikua tukahitaji kusaidiwa hadi kuendesha Ikulu Yetu?.

Najua hili la kusaidiwa kuendesha Ikulu yetu litawaogopesha maana Ikulu ya nchi ndio roho ya nchi, lakini kama kuna vitu sisi wenyewe tunashindwa, kuna ubaya gani kusaidiwa?. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Mfano mzuri wa Watanzania kusaidiwa kitu Ikulu yetu ni kwenye kuhamasisha utalii,
Nimebahatika kufika Africa Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda Mauritius, Seychelles, Misri, ukiangalia vivutio vyao vya utalii ukilinganisha na vyetu, hawatufikii hata nusu!, lakini ukiangalia idadi ya watalii wanatuzidi sana, sababu ni sisi tumeshindwa kuutangaza utalii wetu kikamilifu. Rais Samia alipoingia madarakani, akatokea mfadhili fulani akaifadhili ikulu yetu na Rais wetu kwa kuandaa filamu ya Royal Tour na kugharimia uzinduzi wake nchini Marekani, sasa utalii unashamiri, hivyo hakuna ajabu yoyote kusaidiwa popote hadi Ikulu!.

Wiki hii kumepatikana habari njema kwenye ziara ya Rais Samia nchini China, China imekubali kufanya ukarabati wa Reli ya TAZARA na kutusaidia kuiendesha kwa faida.

Taarifa hii ni habari njema kwa Watanzania, zinazothibitisha China sio tuu ni mshirika mzuri wa Tanzania katika ujenzi wa miundombinu, bali pia ni rafiki wa kweli, kwa kutusaidia misaada bila masharti magumu ya kuingilia uhuru wetu.

Ni China ndio aliijenga reli ya TAZARA, tena hadi vibarua wote ni kutoka China, na baada ya ujenzi, ukiondoa wale waliofia nchini na kuzikwa nchini, wengine wote waliondoka kurejea kwao.

Reli ya Kati ilijengwa na Ujerumani na kumaliziwa na Uingereza, vibarua walitoka India, na baada ya reli kukamilika vibarua hao walilowea Tanzania, na ndio hawa Wahindi waliopo ambao walijenga uhindini kwenye kila miji mikuu reli ilipopita.

Reli ya TAZARA ndio reli pekee ya Uhuru iliyojengwa baada ya Tanzania kupata uhuru, kazi ngumu kabisa katika ujenzi wa reli, sio kutandika mataruma, kazi kubwa ni kufanya upembuzi yakinifu na kuchoronga na kuchanja njia ya kutandika hayo mataruma, hata ujenzi wa SGR, upembuzi yakinifu na kuchanja au kuchoronga njia ulikuwa ni kwa mserereko tuu wa Reli ya Kati kwa kupita mule mule kama tuu kujaladia reli mpya kwenye njia ile ile ya Reli ya Kati.

Usafiri wa reli ndio usafiri wa gharama nafuu kabisa baada ya usafiri wa meli, na reli ndio usafiri wenye uwezo wa kusafirisha abiria wengi na mizigo mingi kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu.

Kati ya mipaka yote nchini Tanzania, mpaka wa Tunduma ndio mpaka unaongoza kwa kuwa bize, kutokana na malori ya mizigo inayokwenda Zambia kutokea bandari ya Dar es Salaam.

Reli ya TAZARA sio tuu ilisaidia sana kubeba mizigo ya Zambia na nchi jirani, za Kusini mwa Tanzania, bali ilisaidia kuokoa barabara zetu na kupunguza msongomano mpaka wa Tunduma.

Kitendo cha reli ya TAZARA kulega lega, kumepelekea mizigo ya Zambia na nchi za Kusini kusafirishwa kwa malori, hivyo kuharibu barabara, kuleta msongamano mpaka wa Tunduma, mizigo ya watu kuchelewa, na ngarama za usafirishaji kuwa juu, hali iliyopelekea jirani yetu Zambia kuamua kutumia bandari ya Msumbiji ambayo iko mbali zaidi, hivyo maboresho ya TAZARA ni habari njema sana kwa Tanzania.

Swali la kujiuliza, tulifikaje huko hadi TAZARA kushindwa kujiendesha kwa faida?. Na sio TAZARA tuu, hata TAZAMA, hata TIPPER, hata ATC, hata Reli ya Kati, NASACO, TCFB, UDA, KAMATA, DMT, Bandari, TANESCO, TTCL, hata POSTA ina chechemea!.

Hivi Tanzania kama taifa, tumewahi kukaa chini na kutafakari, tunakwama wapi?, nini kinachotukwamisha?.
Siku zote kisingizio kikubwa ni mtaji!, nimesema ni kisingizio tuu kwasababu kama ni mtaji, mbona tunakopa sana na serikali inatoa fedha nyingi kuyabeba mashirika yake na mfano mzuri ni Shirika la Ndege la Tanzania, ATCL, limepewa ndege mpya za kutosha tuu, limepewa mtaji mkubwa tuu wa kutosha lakini bado linaendeshwa kwa hasara!.

Hii reli ya SGR tunayoishangilia sana hii ruti ya DAR-Dodoma kupitia Morogoro, subirieni taarifa ya ukaguzi ya CAG mwakani!. Reli ya SGR haiwezi kujiendesha kwa faida kwa kubeba abiria, ubebaji abiria kwenye SGR ni huduma tuu, services, faida ya SGR ni kubeba mzigo wa kushiba!.

Wakati awamu wa JK wakipanga kujenga SGR pia walipanga ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kuipatia SGR yetu mzigo wa kushiba, mzigo unaipitia bandari ya Dar es Salaam, hauwezi kuishibisha SGR ikajiendesha kwa faida!. Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...

Hata uendeshaji wa reli ya kati, tuna matatizo!, faida kubwa ya bandari ya Dar es Salaam ni mizigo ya jirani zetu inayopita kwetu (transit goods), tukajenga bandari kavu ya Isaka ili mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC, ikifika tuu Dar Port, inapakiwa kwenye meli na kukimbizwa Isaka, malori ya Rwanda, Burundi na DRC, wataikusanyia pale. Mara ya mwisho nimepita pale Isaka, hakuna crane ya kushusha mizigo toka kwenye treni, hivyo hakuna mzigo unashushwa Isaka, yale maghala ya TRC, yamekodishwa kwa Bakhresa.

Kwenye kikao kazi cha Ofisi ya Msajili wa Hazina na watendaji wakuu wa mashiriki ya umma, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, aliyataja mashirika 40 ya umma ambayo ni mizigo, akapendekeza yafutwe!, huu ni uthibitisho sisi Watanzania tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya taasisi, lakini zikibinafshishwa, zinashamiri. Hili tumelishuhudia kwenye TBL na Sigara, TCC.

Wakati wa kelele za ubinafsishaji wa bandari, tulishauri, kitu cha kwanza kwa sisi Watanzania, ni kujitathmini tunakwama wapi?, tukijigundua tuna matatizo ya uendeshaji wa baadhi ya miradi, kwanza tukubali makosa, kisha tutafute ufumbuzi, na ikitokea ufumbuzi wa baadhi ya matatizo yetu yatahitaji kusaidiwa, hakuna ubaya kuomba msaada kusaidiwa, kuna nchi zinasaidiwa kuendesha baadhi ya miradi yake, na sasa kwa kadri dunia inavyobadilika kidigitali, utafika wakati tunaweza hata kujikuta tukaikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji kuiendesha kwa faida!. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?

Kwenye hili la kuikodisha Ikulu yetu kwa mwekezaji atuendeshee, mnaweza kudhani ninatania!, mwenzenu nimebahatika kufika ikulu mbalimbalimbali za wenzetu duniani ikiwemo ikulu ya Afrika Kusini, Ikulu ya White House, St. Peters Basilika pale Roma, Buckemham Palace Uingereza, ikulu, ni eneo la kivutio cha watalii, mfano mdogo ni angalia jingo la Beit Al Ajab Zanzibar.

Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa, tulikuwa tunapita kule nyuma ya Ikulu kwenda Feri, enzi za JK, kumefungwa eti ni kiusalama!, JPM alipoingia amepapendezesha Ikulu kwa kujaza wanyama na kuzalisha tausi, yote haya ni ya nini kama Ikulu inafungwa?.

Kwa vile sasa ikulu imehamia Dodoma, hakuna ubaya ikulu ya Dar es Salaam ikafunguliwa kwa utalii, sio tuu tutazalisha mapato mengi bali ikulu ndio kitakuwa kivutio number moja cha utalii wa ndani, kila atakayetembelea ikulu, atapitishwa Makumbusho ya Taifa, na kuishia kupumzika pale Botanic Garden, hata hili linasubiri mwekezaji ajitokeze aandike andiko?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
 
Issue sio CCM issue ni watu walio na Maamunzi ndani ya CCM na nchi kwa ujumla.CCM kama CCM Wala Haina shida.Jiulize kati ya Watu wa CCM na CCM kipi kinaunda nyenzie!?.
Hivyo socially mtu wa pwani swala la kujituma kuvuja Jasho kwaajili ya maendeleo hata yake Binafsi ni Dogo.

Usitegemee Mtu wa pwani au Zanzibar akose usingizii ATI kisa Barabara za Kateshi,Mlowo zimekosa pesa za kujengwa Lami never.
Issue siyo kanda issue ni CCM ni ya hovyo sn
 
Back
Top Bottom