#COVID19 Tunaambiwa na Serikali tuchukue tahadhari ya Corona lakini matukio mengi ya chama na Serikali hayana hiyo tahadhari

#COVID19 Tunaambiwa na Serikali tuchukue tahadhari ya Corona lakini matukio mengi ya chama na Serikali hayana hiyo tahadhari

Yes, aunt kafia korogwe tanga. Babu kafia muhimbili. Yaan it means iko kila mahali. Nahofia itatunaliza aisee. Babu siyo mzururaji aisee.
... halafu kmbwembwe anakwambia Corona inakuzwa bila sababu! Pathetic! Poleni sana ndugu.
 
CCM ni ukoo wa panya, hamtakuja kuwaelewa dawa ni kuwatoa tu madarakani
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wewe endelea kuchapa kazi upate kipato cha kuendeleza maisha yako ya baadae, habari za Corona achana nazo. Tatizo mna macho lakini hamuoni, mnajifanya mnajua kumbe hamjui, achana na siasa ya dunia itakupotezea mda wa kukuza uchumi wako.
Isije ikawa unawaingiza watu chaka, wanafuata hayo maneno wakati wewe unachukua tahadhari zote, Mungu anakuona
 
Nimemuona Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na mikutano ya hadhara kule Songwe na anakusanya watu wengi tu huku viongozi wakituambia hali ya corona ni mbaya. Je, kuendeleza hii mikutano haiwezi kuwa kitisho kikubwa cha kusambaza hiyo corona?

Ni kwanini CCM isiisitishe hii mikutano ili kuonesha mfano wa kuchukua tahadhari?

Mbali na hizo ziara za CCM kuna mbio za mwenge vyuo na shule ambavyo vyote hukusanya watu wengi na viko ndani ya uwezo kuvifunga ili kuwanusuru wananchi na hilo wimbi?
Tunafanya masiahara na janga la corona.Huku Mbozi utadhani hakuna corona.Ni watu wachache wanaochukua tahadhari ya corona.Serikali ichukue hatua zaidi ya kujihadhari na corona.Kwa hali tuliyo nayo isiyozingatia tahadhari tunaweza kuingia kwenye maafa ya kutisha.Mitutano ya kisiasa na mbio za mwenge zisitishwe kwa muda.Ama sivyo tahadhari kubwa ichukuliwe.Kusiwe na mikesha ya mwenge.
 
Macho kumchuzi mkono kuubwabwa pia alikua na ziara ya kikanda pia hilo msijisahaulishe,pamoja na vikao vya chama chake vilikua vikifanyika kwa watu kujazana ndani ya kumbi na sio nje.
Wamesahau! Wanaangalia upande moja
 
Watu wanakwaza sana. Binafsi hapa napata shida ktk kupumua. Nimetoka hospitali. Hizi siku kadhaa hapa nimetoka toka. Ninatumia dawa kwa sasa.

Pole sana. Achana na wajinga chukua tahadhari unazo weza:

IMG_20210708_070119_331.jpg
 
Asante mkuu. Kidogo napata hewa ila sasa siko poa ile yenyewe. Napambana nikae sawa.

Pole sana mkuu. Kwa sasa muhimu kujipa mapumziko. Unahitaji nguvu zote kupambana. Mola atakuvusha.
 
Serikali inajua Corona ipo lakini lockdown haiwezekani. Lockdown hapa itanguusha uchumi na machafuko yatatokea. Kilichobaki sasa hivi ni kuomba misaada tupewe mikopo ya kununua chanjo za Corona na oxygen za wagonjwa.
 
Back
Top Bottom