Tunachokitaka na kusisitiza ni uchaguzi wa haki na si jingine

Tunachokitaka na kusisitiza ni uchaguzi wa haki na si jingine

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,181
Marehemu Raisi Magufuli ameondoka na kaiwacha nchi katika sintofahamu ya manunguniko ya matokea ya uchaguzi ,tunaweza kusema ameiwacha nchi wananchi wake wakiwa ndani ya mgawanyiko mkubwa sana unaofukuta.

Ninavyoamini hata kama uchaguzi usingekuwa na mizengwe bado CCM wangeibuka videdea kwa upande wa Tanzania bara,wakati mwengine najiuliza hivi kama ungefanywa au ukifanywa uchaguzi ulio wazi na usio na chembe chembe zinazoashiria mizengwe,wizi wa kura,ubadilisho wa matokeo na kila mgombea awe diwani,mbunge raisi ashinde kwa nguvu ya kura za uhalali kabisa ,furaha yetu itakuwaje ?

Hukuti mtu au chama kimelalamika kwa kukiukwa misingi ya uchaguzi ndani ya bunge unakuta kuna wabunge walioshinda kwa haki kabisa hawakulalamikiwa wao wala chama chao,kwa kweli watanzania wa leo wanahitaji hili jambo lifanyike kwa chaguzi zinazokuja,tupige hatua ,mhimizo kwa wazalendo hilo jambo linahitaji kufanywa ,iwepo tume inayojielewa,tume sikizi inayofanya mambo yake kwa uwazi kabisa na maridhiano kila mmoja aridhike kuwa tunaingia kwenye uchaguzi wanaochagua ni wananchi wakichagua bovu au lililoiva ni wao na hakutakuwa na senenesenene.

natumai chini ya Mheshimiwa Raisi Mpya wa Tanzania hili linawezekana kabisa ni kuamua tu ,maana hakutakuwa hata na malalamiko na vyombo vyetu vya usalama vitakuwa huru vyenye kuheshimiwa na wananchi ,Ila CCM hili naona hawaliwezi na hawajiamini ,ila mimi naona ni woga tu bado wananchi wanaiamini CCM na wataichagua japo kura zitagawika ushindi mwembamba unatosha kuirudisha imani kwa wananchi kuwa nchi yao ipo kwenye mikono salama.

CCM wabaya sana na ndio mtu muoga alivyo anakuwa hatari kwa wananchi na Taifa.
 
Tunataka urudiwe hata sasa hivi kionekane kilichomtoa kanga manyoya ccm si ya mchezo mchezo!
 
Back
Top Bottom