tunaelekea 2027 ila hali ya vyoo vya maeneo ya umma vinakupa ujumbe gani

tunaelekea 2027 ila hali ya vyoo vya maeneo ya umma vinakupa ujumbe gani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Jamani, tunaishi mwaka 2026, dunia inazungumzia AI, robots na safari za kwenda Mars, lakini ukiingia kwenye baadhi ya vyoo vya maeneo ya umma unajiuliza kama bado tuko kwenye zama za mawe tena nahisi hata zama za mawe vyoo vyao vilikuwa sio vichafu kama sasa huenda walikuwa wanakwenda porini wanachimba shimo na kufukia..

Nani amewahi kuingia kwenye choo cha hospitali ya serikali akatoka akiwa na maswali mengi kuliko aliyokuwa nayo kabla ya kuingia?

Tuache kwanza vyoo vya shule za msingi, ambako tunaweza kusema watoto bado wanajifunza nidhamu. Lakini hospitalini, mahali ambapo watu wanakwenda kutafuta afya, unakuta choo chenyewe kinaumwa.

Maji hakuna, usafi hakuna, vifaa vimeharibika, na wakati mwingine unakuta mazingira ambayo hata kuyaelezea ni changamoto. Aisee, mtu anaingia chooni na kutoka akiwa na hitaji jipya la kunawa moyo

mambo kama haya lawama tuwape kina nani je ni raia kukosa ustaraabu,je ni viongozi wa hizo ofisi ,je ni wafanyakazi wa usafi,je ni mifumo ya ujenzi sio rafiki ilitakiwa ujenzi ufanyike kwa namna hata kuchafua haiwezekani,je ni serikali,,kuna nani hapa anazingua zaidi...
 
Mambo ya vyoo vya umma....shulen, offcn , hospital n.k ni changamoto sana kwa Tz ....

Kila mtu kakulia kwenye utamaduni wake.... kuna mtu anayaona maji hapo lakini hamwagi, anaweka mzigo anaondoka zake.... hivi hapo tutalaumu mamlaka ?

Ustaarabu ni ishu binafsi yani, tumia nawa safisha/flash na mwenzio aje atumie

Enzi nasoma chuo, niliwahi kupanga mahali mtaani, kuna jamaa anachukua kopo la maji lipo nusu anaingia nalo chooni.... unawaza hapo atanawa ? Make hayatoshi.... Ama ataflash ? Uchafu ni jadi kwa baadhi ya jamii zetu
 
Tech za AI, robots nk ni kwa nchi za watu huko! Kwa Tanzania bado tupo ujima...
 
Uwakute sasa vingozi wa ngazi za wilaya wakifika ngazi za vijiji na taasisi zao za umma. Wanalaumu kama kule kwenye ofisi zao kuko safi.
 
Back
Top Bottom