Tunaelekea “Kuishi Kwenye Mtaji” Baada ya Matukio ya Oktona 29. Tujitafute na tujue tunatokaje hapa

Tunaelekea “Kuishi Kwenye Mtaji” Baada ya Matukio ya Oktona 29. Tujitafute na tujue tunatokaje hapa

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Kuna kauli maarufu inayosema: “Nchi inapoanza kutumia nguvu nyingi sana kujilinda na kulinda utawala wake, ndipo inapoanza kuishi kwenye mtaji wake.”
Bado hakuna takwimu rasmi za kuthibitisha hilo, lakini dalili zote zinaonesha tunaelekea huko au tumeshafika.
Tangu tarehe 29 Oktoba 2025, siku ya uchaguzi mkuu, Tanzania imekuwa kwenye hali ya taharuki ya kiusalama. Hadi leo, wiki sita baadaye, bado kuna vikwazo vya usafiri, polisi na askari barabarani kila baada ya kilomita chache, na hisia kuwa kila kitu kinaweza kutokea muda wowote.

Wakati halii inaendela, inaweza tukawa tunaishi kwenye mtaji bila ya kujua. Ni wazi uchumi wetu kwa miaka mingi, umekuwa wa “subsistence”, yanii unachopata leo unatumia leo, na kesho unatafuta tena cha kesho. Uchumi huu si kwa wananchi tu, hata serikali ndio uchumi wake huo. Unakusanya leo unatumia leo, au unaanza kutumia kabla hata ya kukusanya tena kwa serikali, ni ule uchumi wa Mali kauli. Uchumi wa aina hii hauwezi kumudu mtikisiko wa aina hii kwa muda mrefu.
Kwanini nimeanza kuwa na dhana kuwa tunaishi kwenye mtaji?, hebutufikiriie mambo haya:
  • Bajeti iliyoegemea kwenye mishahara na posho, Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 (Sh trilioni 55.6), karibu 70% ni matumizi ya kawaida, na zaidi ya Sh trilioni 20 ni mishahara na posho pekee. Hiyo inamaanisha kwamba maendeleo yanategemea asilimia 30 tu ya bajeti. Uchumi ukishuka hata kwa 20–30%, tayari tunakuwa kwenye hali ya “kuishi kwenye mtaji”.
  • Ongezeko kubwa la bajeti za ulinzi na usalama, Bajeti ya Ulinzi iliongezeka kwa 20% hadi Sh trilioni 3.8, na ile ya Mambo ya Ndani kwa 20.5% hadi Sh trilioni 2.06. Hizo zilikuwa kabla ya machafuko. Sasa, pamoja na posho za ziada, petroli, risasi, na gharama za kurusha helikopta (zaidi ya Sh milioni 6 kwa saa moja kwa kila Cougar H215M), matumizi haya bila shaka yameongezeka zaidi.
  • Uharibifu wa miundombinu, Nilimsikia Waziri akisema Vituo 672 ya mafuta vilichomwa moto, kama aliiona hiyo kauri nyepesi basi anapaswa kujua , hiyo ni 26% ya vituo vyote vya mafuta Tanzania Bara (kwa mujibu wa takwimu za EWURA 2024). Hiyo ni hasara ya mabilioni ya shilingi ambayo italazimika kuyalipa kwa kampuni za bima au kwa wamiliki. Kama ni kweli, na kama ilikuwa siasa ya “kushift burden” ni sawa na kuwaambia wageni kwenye msimu huu wa sikukuu kuwa 26% ya miundombinu ya kununua mafuta haifanyikazi kwasasa ukitaka kuja basi ujifikirie vizuri.
  • Bima na usafirishaji wa mizigo, Kampuni zote za bima duniani zimeshaona kilichotokea. Mizigo inayokuja Tanzania sasa inalipiwa premium kubwa sana, na wengi wanaweza kugoma kabisa kuleta mizigo. Bei za bidhaa zitaongezeka moja kwa moja.
  • Biashara za mwisho wa mwaka imekufa, Watu wengi wamekimbia mjini na kurudi vijijini kabla ya sikukuu. Hakuna shopping za Krismasi wala mwaka mpya. Wafanyabiashara wanaufunga mwaka bila faida wanategemea Januari ili wapumue, lakini hali bado ikiendelea kuwa ya wasisi basi ni ukosefu wa mapato kwa muda mrefu.
  • Utalii umepigwa chini kabisa, Kipindi hiki ndicho msimu wa watalii. Lakini ni nani anayetaka kuja nchini ambapo kila kilomita mbili unakutana na askari mwenye bunduki au helikopta inayozunguka juu? Yani mtu pesa yake na aje kuitumia akiwa chini ya ulinzi, Anakichaa? Kiufipi “maokoto” ya kila mwaka yamekatika.

Hali hii haiimuzi serikali pekee, inamgusa hadi mtu mmoja mmoja nayeye ameingia kwenye “kuishi kwenye mtaji”:
  • Anatumia akiba yake ya dharura kwa sababu shughuri za kiuchumi zimedorora au biashara zimesimama.
  • Anauza mali ili alipie chakula na kodi.
  • Anakopa ili aendelee kuishi.
Cha kushangaza badala ya serikali kufikiria namna kutoka hapa, yenyewe iko busy kumtafuta mchawi.
Hakuna mchawi aliyeleta hali hii. Kuna uchawi tu na uchawi ni siasa za chuki, uchu, ubinafsi na kutumia nguvu badala ya mazungumzo. Uchawi ni siasa za CCM zilionza baada ya Uchaguzi wa 2015.
Acheni kutafuta mchwai kwa kutubua mahusiano yetu ya kidiplomasia, Nyie mtapita au mtakufa hii nchi itabaki, Kinachotakiwa hapa ni kutafuta muarobaini wa muda mrefu na si janja janja za muda mfupi.
  • Ufanyike uponyaji wa kweli, si ujanja-ujanja. Watu waambiwe kweli kuendelea kuzungunga mbuyu ni sawa kabisa kutokuwa na nia ya kuponya watu.
  • Ufanyike uchunguzi wa haki kuhusu vifo na mauaji na walioathrika waponywe. Hili sio jiwe kwa unaweza kulifukia tu na usahau, Hii ni mbegu mti wenye Miba na utaota tena, kama hakujafanyika uponyaji.
  • Serikali iache siasa za kutangaza ajira, iwawekee vijana mazaingira wezeshi ya kiuchumi, ni wazi serikali haiwezi kuajiri watu wote, kwanza uchumi wetu hauwezi hata kuhudumia watunishi wa umma milioni moja, hivyo tusiwaongepee hawavijana kwa matangazo ya kazi, mtarudisha mzigo tena kwa wananchi na litaandamana kundi lingine.
  • Urejeshe uhuru wa kujieleza na wa kukusanyika bila hofu, wote Tumeona vitu vilivyo haribiwa na kuchomwa moto ila cha kushangaza bado tunadhani sababu watu wametumwa na watu kutoka nje ya nchi kufanya vile. Sikweli, uhalisia ni kwamba uharibifu ni haiba ya binadamu mwenye makasiriko, tuache hii tabia ya kutokusikilizana, kuna mtu akiachwa atoe povu lake anakuwa amemaliza hasira zake hapo… huu mchezo wa kuwafanya watu wawe mabubu kuna siku mtu atavaa bomu.

Amani ya kweli haipatikani kwa risasi wala kwa kufunga midomo.
Inapatikani pale ambapo kila mwananchi anahisi yeye ni sehemu ya taifa, si adui wa taifa. Tuchague amani ya haki ili tujitoe hapa kwenye kuishi kwenye mtaji. Wala hatuna uthubutu wakutunishiana misuli na wahisani, tutakuwa Zimbabwe.
Tanzania yetu sote ila inayokuja ni vijana na wanastahili mustakabali bora kuliko huu, wengiwenu mnaominya haki hamuwezi hata kuwa na wiki 3,000 za kuishi mbeleni. Haya sio makazi yenu, fanyeni mjiandae na maisha yenu ya milele huko, yaliyobaki hapa duniani ni ya vijana.
 
Back
Top Bottom