Tunaelewa kwanini Mwigulu ana hasira na Magufuli hadi leo, na hadi sasa anatoa kauli hasi dhidi yake, na kumwaga maua kwa wingi!

Ushauri wa Bure Kwa walinda Ligacy,badala ya kuhangaika na Mwigulu wajikite zaidi kwenye hoja zake za takwimu Ili wafanye ulinganisho na waseme amedanganya au hapana maana kajenga hoja ambae anabisha ajitokeze kwa hoja pia.

Samia ni next level ila sio mtu wa Majigambo
 
Hujaeleza sahihi. Chuki ya ng'wigulu ni kwamba anautaka urais na magufuli alimpiga chini kwa mbali. Kuutaka urais sio kosa ila unautaka kwa ajili gani. Ng'wigulu anautaka urais kwa sababu za ubinafsi. Kujitajirisha na kuweka himaya ya familia yake. Magufuli aliutaka urais kwa maslahi ya umma. Tangu ngwigulu awe waziri amemshauri mama kukopa ovyoovyo mikopo hadi kujenga matundu ya choo. Tunaojua tunajua ukikopa ovyo wakopeshaji wanakulipa. Si benki ya dunia wala imf wao ni vyombo vya kibiashara tu na kuchochea sera za kufaidisha nchi za maghsribi. Kuhusu ubinafsi wa ng'wigulu ona anavyompromote mwanae kwenye siasa za vidudu. Tuliona kila akikopa mabasi ya ester ya familia yake yanaongezeka. Kwa hiyo lao na wabinafsi wenzake kina januari ni moja wako kwenye mission ya kumshusha jpm kuonesha hakua rais mzuri maana wanataka kiongozi mbinafsi kama sio wao basi japo abakie samia mbinagsi aliyewaruhusu wale kwa urefu wa kamba zao za malisho.
 
Matapeli siku zote hayapendi watu makini waliobana mirija Yao ya unyonyaji. Ulitegemea amsifu Magufuli kwa namna anavyopiga pesa hivyo? Haya mengine umeandika hadithi tu lakini ukweli ni kwamba Jamaa ni tapeli na fisadi hivyo lazima amsifu yule kamuweka hapo. Hata akimbeza Magufuli leo kitu Nina uhakika nacho ni kwamba tapeli huyu atakufa na ataacha kila kitu alichowaibia Watanzania
 
Angalia bwana, anaweza kuja kuwa raisi wako ajae. Katika siasa hakuna mtu anafanya kitu bila kuwa na malengo. Nyimbo za mpeni maua yake haziimbwi bure!
Hili linajulikana alishawahi kuwa rais wa Mawe sasa anataka akakalie magogoni.

Mwigulu namfahamu nje ndani ni hatari kwa uhai wa watu hasa akiwa anataka kufanikisha jambi lake.
Najiulizaga huu ujasiri wa kumtaja Mungu huwa anautoa wapi?
 
akumbuke samia haungi mkono hoja za kijinga za kumtukana au kumlaumu magufuli
 
Umeongea mengi ila Magufuli hakupenda kufanya kazi na wanasiasa..mtu ambaye kila akikaa anawaza namna ya kuwa rais badala ya kutimiza majukumu..mtu ambaye anawaza anapigaje hela za serikali ili zimsaidie kuwapa watu wa kumuandika kwenye mawe na madaraja nchi nzima wakati wa uchaguzi.
Kina Mwigulu ni underperformers na Magu aliliona hilo..hawakuweza spidi ya Magu..kwa sasa anachofanya ni kumpaka huyu mafuta kwa mgongo wa chupa..anajua anapiga vya kutisha na mama yupo yupo tu..ukiona sifa za ovyo ovyo ujue upigaji ni mkubwa.
 
Tatizo la wafuasi wa mwendazake hamtaki kuambiwa au kusikia ukweli. Yule mwamba hakuwa mtu kabisa. Tukiongea humu tunaonekana sio wazalendo. Kati ya wewe mleta mada na Mwigulu ambae alikuwa ni waziri wake ni nani anamjua Magu vizuri? Acha upumbavu uwe huru
 
Na wewe inatosha sasa ku invent mambo Ili uonekane unajua.
Unajua maana ya invention, tuanzie hapo. Nenda kamuulize Mwigulu kama kuna invention hapo. Anzia na kumuuliza kama kama aliwahi kutolewa baraza la mawaziri na Magufuli!
 
Hovyo kweli ulitaka Magufuli ampe Mwigulu wadhifa gani kuwaridhisha wenye chama chao huko CCM.

Elewa Mwigulu sio wa mzaha-mzaha au mtu wa kuunga unga-unga kama hakina mwana FA.

Mwigulu ni mtoto wa CCM allelewa kushika madaraka makubwa siku moja (better still mwalimu wake wa siasa ndio mshauri wa raisi wa siasa leo na ndio wenye chama chao ukisikia).

Future ya Mwigulu hata raisi angekuwa nani mradi ni mtoto wa CCM walisha mtengeneza kushika madaraka kwa succession planning yao ndani ya CCM. Shida yake ni baada ya kufika juu amekuwa mtu hovyo.

Ndio maana hata Magufuli alimpa madaraka makubwa kwa kuelewa mpango wa CCM juu yake, waziri wa mambo ya ndani sio mtu mdogo,

Ukitoa waziri mkuu na makamu kwa kipindi hiki. Vinginevyo ni waziri wa mambo ya ndani pekee ndio mwenye escort huyo sio mtu mdogo kabisa.

Shida ilikuwa Mwigulu mwenyewe sasa alipopewa mambo ya ndani na Magufuli, kutwa yupo kwenye ndondo cup; hizo ndio sababu za Magufuli kumtumbua na kuona to hell na plan za watoto wa CCM..

Shida yenu amuelewi how CCM works.
 
rais samia ni bora kiliko ibilisi mwendazake.

over
Nakubali. Pamoja na uzuri woooote wa Magufuli, huwezi kuwa na kiongozi mbovu zaidi yake ikiwa kiongozi huyo hawanyimi watu haki ya kuishi.

Tuseme ukweli, Magufuli aliona ni halali kuwaondoa watu kwa maslahi ya taifa, na alitamka hayo waziwazi. Sasa hata uwe mzalendo kiasi gani, hilo linakuweka doa ambalo ndilo watu wataona siku zote. Wale wanaomsifia Magufuli lazima wafikirie wale walioptozewa ndugu zao. Unawezaje kuwashawishi ndugu ya Bensaanane kwamba Magufuli alikuwa kiongozi mzuri kwa sababu alizuia ufisadi, alijenga flyovers? Atakuelewa? Unawezaje kumshawishi huyo ndugu ya Bensaanane kwamba Raisi Magufuli ni bora zaidi ya Samia kwa sababu Raisi Samia kosa lake ni kuruhusu mawaziri na viongozi kufanya ufisadi, japo anataka haki sawa kwa Watanzania na hapotezei watu?
 
We hauko sawa, miradi ya ujenzi hata asingekuwa yeye raisi ingefanyika tu. Miradi mingi anamalizia ya mAgufuli na bila aibu kuna vichwa panzi wanamshukuru yeye. Hata ungekuwa wewe rais ungejenga barabara.
 
We hauko sawa, miradi ya ujenzi hata asingekuwa yeye raisi ingefanyika tu. Miradi mingi anamalizia ya mAgufuli na bila aibu kuna vichwa panzi wanamshukuru yeye. Hata ungekuwa wewe rais ungejenga barabara.
Pole sana Bado hujasema Hadi useme 🤣 🤣

Sijaweka mradi hata mmja wa kumaliza ,yote ni miradi mipya.Ya kumalizia haipo hapo na sijamaliza yaani.

Mwisho kwani huyo mwingine mnamsifia Kwa lipi zaidi ya mamiradi ya hasara?
 
Anaupga mwingi na ana mbususu tamu au sio Mwii GURU...
 
Hakuna uongozi bora duniani unao justify kuwapotezea watu kwa sababu tu wanapingana na kauli zako. Hili kwa Magufuli halikuwa doa, lilimuondolea sifa zote za kuwa kiongozi.
 
Yule jamaa alitaka kuwa raisi wakati alishindwa kutaja maana ya TRAB na TRAT yaani akiongea dakika mbili humsikilizi kwasababu anaongea pumba tu.
 
Mkuu jitahidi sana kwenye matumizi ya ubongo wako.
 
Upenyo wa dili ulifungwa sasa umefunguliwa
 
Mwigulu huyu huyu aliyeiba pesa akiwa wazir wa, Mambo ya ndani na kuanzisha Singida United. Na alipofukuzwa, uwaziri timu ikafa. Huyu huyu mwenye timu nyingi huku pesa ikitoka serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…