Tunaenda kumaliza kazi Misri, Al Ahly ni wa kawaida mno

Sio billioni 2 ni wastani wa billioni moja coz ni dola laki nne

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Ni dola milioni 1 (Shilingi bilioni 2 na nusu), chanzo ni caf wenyewe

 
Sasa huyo El shahat kafanya nn? Mbna hakna cha ajabu kwake hata km angeanza.
 
Jamaa wana spidi na Yule manywele aliyeingia ni moto
 
Shida ni mashabiki wengi kuweka ushabiki mbele kuliko uhalisia, wale jamaa hawabutui kubahatisha goli, ni timu kubwa wametuzidi vingi, tuna vingi vya kujifunza kwao
 
Shida ni mashabiki wengi kuweka ushabiki mbele kuliko uhalisia, wale jamaa hawabutui kubahatisha goli, ni timu kubwa wametuzidi vingi, tuna vingi vya kujifunza kwao
Hata katika uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ni habari nyingine, control na maamuzi wakiwa na mpira ni ya kiwango cha juu.
Ila, Simba wamejitahidi.
 
Wakati unawaza hivyo, jaribu kutathmini ni lini Al Ahly alipata sare Dar es salaam? Huenda wao wakakuona wewe ndio wakawaida sana tena kakukosa mengi mno ukiwa kwako.
Mpira hauchezwi sebuleni kwako.

Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Hata katika uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ni habari nyingine, control na maamuzi wakiwa na mpira ni ya kiwango cha juu.
Ila, Simba wamejitahidi.
Simba tumejitahidi sana, wale jamaa wanasajili mchezaji Bilion 12 kutoka ulaya, kuna striker wamemsajili msimu uliopita kutoka Borussia Dortmund Anaitwa Anthony Modeste mcheki you tube, kwa investment hawa sio wenzetu na soka ni uwekezaji, sisi Bilioni 3 mfadhili kuweka ni Mvutano balaa.
 
Yaani Simba akapate ushindi au sare ya zaidi ya goli moja Cairo, Misri? Mkuu, punguza kuotaota. Simba imeshafika mwisho...
Huujui mpira ndiyo maana unaona haiwezekani.

Halafu nyie ndio wale mnaokariri. Mpira hauchezwi chumbani.

Nb: wewe ndiyo umefika mwisho wa kufikiri bila shaka!

Simba itajipanga vilivyo na itavuka! Hakuna lisilowezekana ktk mpira.
 
Mnahesabu mlivyokuwa mnatishia tishia kipindi cha pili wakati ahly zile nafas tatu za kipindi cha kwanza mmezisahau kabisa.
Kwa kigezo lipi Simba atashinda huko misri
Ni kipi hakiwezekani ktk mpira ?
 
Huujui mpira ndiyo maana unaona haiwezekani.

Halafu nyie ndio wale mnaokariri. Mpira hauchezwi chumbani.

Nb: wewe ndiyo umefika mwisho wa kufikiri bila shaka!

Simba itajipanga vilivyo na itavuka! Hakuna lisilowezekana ktk mpira.
Mkuu, inawezekana kwa kufuatilia mpira huniwezi. Nimeanza kufuatilia na kuupenda tangu miaka ya 80. Nayajua mengi sana.

Kama ambavyo ilikuwa ngumu kwa Power Dynamos kupenya baada ya sare ya 2-2 kwao ndivyo itakavyokuwa kwa Simba pale Misri.

Al Ahly wamecheza kibingwa sana leo. Kumbuka hii ni mtoano, si suala la alama. Sare ya Dar, kwa mabingwa kama wale, ni kisu kikali shingoni mwa Simba.

Hata mimi najua kwenye mpira lolote linaweza kutokea. Ila, ugumu huonekana zaidi kwenye matokeo kama ya leo na historia ya timu hizi zinapocheza Cairo, Misri.
 
Mnauhakika hayo mapungufu waliyoyaonesha hapa Dar watayaonesha na huko Misri?? Na mnauhakika pia mapungufu yenu mliyoyaonesha hapa dar hamtayaonesha misri?
 
Kazi inaenda kumalizika Misri, Tukitumia mapungufu waliyoonyesha hapa kwa Mkapa tunatoboa

Al Ahly ni wepesi tu, tunawaweza
ni jambo bora kuishi kwa matumaini,, nakukumbusha al ahly hajawahi kupata sare kwa mkapa huu ni kama ushindi kwao.

ukicheza na al ahly kwao wanakulazimisha wewe ufanye makosa ili wakufunge na hayo mapungufu uliyoyaona kwao hayakusababishwa na simba ni wao wenyewe na hawatayafanya kwao.
 
As long as wanapigiwa boli mpaka goli zinaingia al ahly amna kitu..
 
Hakuna team yenye figisu na inayobebwa duniani kama al ahly yaani mechi zao nyingi wanashinda kwa fiksi tu leo refa kawabeba sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…