Tunafikiri kwa kutumia lugha gani?

Tunafikiri kwa kutumia lugha gani?

The Intelligent

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2013
Posts
2,459
Reaction score
824
Ni lugha ipi ambayo mtu huitumia wakati anafikiri? binafsi nimeshindwa kujua lugha nnayotumia wakati wa kufikiri(sio kuzungumza),
Vipi kwa wale wanaotumia lugha zaidi ya moja ktk kuzungumza, je kabla ya kuamua kuzungumza anakuwa amefikiri kwa lugha ipi? kwani anaweza kuchagua ni lugha ipi aitumie, lakini lugha ya kufikiri ni moja tu, kufikia hapo ndipo nnapotaka kujua lugha ya kufikiri ni ipi?
 
Kila jambo kwa majira yake na wakati kwa kila kusudi..

Ukiwa unawasiliana kwa lugha flani taarifa huzifikia ubongo kuputia hiyo lugha na matokeo kutafsiriwa kwa lugha ile ya taarifa iliyopokelewa...
Mfano mimi nimesoma ujumbe wako ulioandikwa kwa kiswahili ubongo wangu umetoa tafsiri ya ujumbe kwa kiswahili...so ni inategemea..
 
Ni lugha ipi ambayo mtu huitumia wakati anafikiri? binafsi nimeshindwa kujua lugha nnayotumia wakati wa kufikiri(sio kuzungumza),
Vipi kwa wale wanaotumia lugha zaidi ya moja ktk kuzungumza, je kabla ya kuamua kuzungumza anakuwa amefikiri kwa lugha ipi? kwani anaweza kuchagua ni lugha ipi aitumie, lakini lugha ya kufikiri ni moja tu, kufikia hapo ndipo nnapotaka kujua lugha ya kufikiri ni ipi?

Lugha inayotumika ktk kufikiri ni ile unayoijua na kuielewa sana!
 
Kuwaza na kufikiri hakutumii lugha yo yote.
 
Ni lugha ipi ambayo mtu huitumia wakati anafikiri? binafsi nimeshindwa kujua lugha nnayotumia wakati wa kufikiri(sio kuzungumza),
Vipi kwa wale wanaotumia lugha zaidi ya moja ktk kuzungumza, je kabla ya kuamua kuzungumza anakuwa amefikiri kwa lugha ipi? kwani anaweza kuchagua ni lugha ipi aitumie, lakini lugha ya kufikiri ni moja tu, kufikia hapo ndipo nnapotaka kujua lugha ya kufikiri ni ipi?

huwa tunafikiri kwa lugha nyingi mno tunazozijua na tusizozijua, kwa mfano 1.unamkuta mtu anaongea lugha usiyoijua lakini unakamata neno moja au mawili unajaribu kuwaza kuwa pengine kamaanisha nini, 2. unakuta mkalimani anayefahamu lugha tatu lakini anawatafsiria watu wawili wasiojua lugha ya mwingine mfano mchina na mfaransa hapo unafikiri wa lughta tatu kichina kiswahili na kifaransa 3. unampigia simu mtu yuko kijijini ambaye mmezoea kuongea kilugha hapa utakuwa unawaza cha kusema kwa lugha hiyo. tunawaza kwa lugha nyingi tu inategemea uko location gani na watu gani
 
Naweza kuongea lugha zaidi ya moja lakini wakati wakufikiria natumia kiswahili, nikiongea na mzungu wakati naanda jibu la swali aliloniuliza hua naliwaza kwa kiswahili kwanza na kujiridhisha kama ni jibu au ni hoja sahihi
 
Lugha ni mfumo km ilivyokuwa mipangilio ya vitu mbalimbali kwenye computer ambapo vyote vikikutanishwa ndipo hufanya kazi ikiwepo kimoja wapo hakipo bac co mfumo tena....
Tuje ktk swali lako lugha km mfumo inamatumizi mengi ambayo hukidhi matumizi ya mtumiaji mfano.hapa tunatumia lugha kuzungumzia lugha hii pia ni kazi ya moja wapo ya kazi ya lugha.Mtoto anapozaliwa na kukulia ktk jamii flani ambayo ni wazungumzaji wa lugha fulani yule mtoto pasipo yy kujua atajikuta anazungumza ile lugha husika lets say yule mtoto akasoma pale pale kuanzia shule ya msingi had kidato cha nne lakn baadae akahama na kuenda kwenye jamii nyingne ambayo wanazungumza lugha tofaut na ile aliyokulia atajifunza ile lugha na kuilewa vzr...lakn ss kwa vle yule mtoto alishakulia ktk jamii nyngne tofauti na ile na akaweza kuzungumza ile lugha kwa ufasaha yule mtu hatakama atakuwa kwenye hyo jamii nyingne atatumia lugha yake ya kwanza(mother tongue)kwenye kufikiria lakn kwenye mazungumzo anaweza kutumia lugha ambayo tofaut na ile anayotumia kufikiria...
Conclusion:::Mtu anatumia lugha mama au lugha yake ya kwanza kuifahamu ktk kufikiria hata km anafahamu lugha mbili na kuzitumia zote kwa ufasaha ila lugha mama ndo inadominate sana kwenye kufikiria
 
Nauliza tena, kama mtu anafikiri kwa lugha anayotumia(aliyoizoea), vp bubu na vipofu? watoto wachanga je nao wanafikiri kwa lugha ipi?
Kram Billz.
 
Last edited by a moderator:
Naweza kuongea lugha zaidi ya moja lakini wakati wakufikiria natumia kiswahili, nikiongea na mzungu wakati naanda jibu la swali aliloniuliza hua naliwaza kwa kiswahili kwanza na kujiridhisha kama ni jibu au ni hoja sahihi

Na kiziwi anatumia lugha ipi kufikiri?
 
Upo sahihi mkuu nakujibu km ifuatavyo:::kipofu na bubu wote wanamatatizo ambayo yanaweza kuwafanya kutokutumia lugha japokuwa wanaifahamu...kumbuka kipofu na bubu wote lazma watakuwa watu wa jamii ambazo wanazunguza lugha fulani kwaiyo katka kukua kwao mfno.bubu atakuwa anajifunza lugha kwa namna yake ambapo anaweza kufanyia tendo kwa anachokisikia lakn hawez kujibu kwa kutoa sauti ila kwavle amezoea kusikia labda mtu akifariki itabd uoneshe uso wa huruma bas nae atafanya ivo....
Watoto wachanga huwa wanajifunza lugha pasipo wenyewe kujijua na nivigumu kwa kawaida mtoto mchanga kutokana na umri wake mdgo ubongo unashindwa kukumbuka vzr ndomana hata leo nikikuuliza ulizaliwa hospitali gan huwez kunijbu kwasababu kpnd hcho ubongo wako ulikuwa bado haujaanza kuhifadhi kumbukumbu...
So vipofu n bubu wote wanatumia lugha ya jamii yao husika ktk kufikiria japokuwa ya mapungufu yao...kwa kesi ya watoto wachanga ambao bado wao kufikiria inakuwa ngumu kutokana na ubongo wao unakuwa bado haupo tayar kuhifadhi kumbuku
 
Kama kiziwi mzungu atafikiria kwa kizungu na kama ni mswahili atafikiria kwa kiswahili

Kiziwi wa kizungu/kiswahili atakuwa amewahi kusikia wapi hizo lugha? kumbuka kuwa kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa.
 
Back
Top Bottom