The Intelligent
JF-Expert Member
- Dec 27, 2013
- 2,459
- 824
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
badilisha heading iwe kiziwi na bubu wanatumia lugha gani kufikiri naona maswali yako mengi yameegemea huko.
Mm naongea lugha tano, pamoja kwamba inategemea na kitu unachofanya japokuwa kunakuwa kama kuna in-situ translation kutoka lugha moja kwenda nyingine lakini mother tongue ndo inayotawala. Na usishangae wakati mwingine uko kwenye mazungumzo kwa mfano ya kiingereza ukajikuta umetumia neno la kifaransa bila kujua.
Watu hufikir kwa.Lugha ya picha
Nilikuwa nasubiri jibu kama lako. Mara nyingi tunatumia picha
Hoja ni lugha ya kufikiri sio kuzungumza.
Hujaelewa context kwa ujumla, suala suala la kuwa unafikiri kwa lugha gani linaanza kama unazungumza lugha zaidi ya moja. Na nikasema pamoja na hizo lugha ninazozungumza ila mara nyingi nafikiri kwa kutumia lugha mama. Lakini wakati mwingine inategemea na kitu unachofikiri na ukiwa unafikiri kunaweza kukawa na in-situ translation. Au neno lugha tano ndo limekukwaza!!!?
Ni lugha ipi ambayo mtu huitumia wakati anafikiri? binafsi nimeshindwa kujua lugha nnayotumia wakati wa kufikiri(sio kuzungumza),
Vipi kwa wale wanaotumia lugha zaidi ya moja ktk kuzungumza, je kabla ya kuamua kuzungumza anakuwa amefikiri kwa lugha ipi? kwani anaweza kuchagua ni lugha ipi aitumie, lakini lugha ya kufikiri ni moja tu, kufikia hapo ndipo nnapotaka kujua lugha ya kufikiri ni ipi?
Kama ni hivyo viziwi je hutumia lugha gani kufikiri?
Ni lugha ipi ambayo mtu huitumia wakati anafikiri? binafsi nimeshindwa kujua lugha nnayotumia wakati wa kufikiri(sio kuzungumza),
Vipi kwa wale wanaotumia lugha zaidi ya moja ktk kuzungumza, je kabla ya kuamua kuzungumza anakuwa amefikiri kwa lugha ipi? kwani anaweza kuchagua ni lugha ipi aitumie, lakini lugha ya kufikiri ni moja tu, kufikia hapo ndipo nnapotaka kujua lugha ya kufikiri ni ipi?
Lugha uliyozoea
Kwa mfano, kiziwi asiyewahi kusikia sauti yoyote ya mtu au kitu, halafu pia ni kipofu kwa maana ya kwamba hajawahi kuona taswira ya kitu chochote, je huyo anafikiri kutumia lugha ipi?
Lugha inamaana pana, yeye kwa jinsi anavyowasiliana hata kama ni kwa hisia kwa mfano harufu ndivyo atakavyofikiria, ndio lugha aliyozoea hiyo. Bubu anayeona atawaza kwa lugha yake, kiziwi na bubu ila anaona analugha yake, kipofu anayesikia na kunusa analugha yake atafikiri na kuwaza kwa kutumia lugha hiyo aliyozoea.
Unajua maana ya lugha?
Ni utaratibu rasmi wa kuwasiliana kati ya binaadamu na binaadamu au wanyama wowote mwenye akili.