Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
MADA HII IMEJIKITA KATIKA TEUZI ZA MAKATIBU WAKUU ULIOFANYIKA TAREHE 4/4/2021

Mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye anaishi katika nchi inayoongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninayo haki ya kutoa maoni juu ya mustakbali wa nchi hii.

Katiba yetu inatambua kuwa, palipo na binadamu hapawezi kukosekana mapungufu ya kibinadamu ikiwemo ubaguzi, uonevu upendeleo n. k, ndiyo maana Katiba ikapiga marufuku vitu hivyo.

Sasa kwa muda mrefu, nimekuwa hapa JF nakemea teuzi ambazo haziakisi demografia ya nchi yetu, nilikemea teuzi zilizokaa kidini, kijinsia na kikanda. Kuna watu humu JF wako comfortable kukemea teuzi zilizokaa kikanda, au kikabila lakini wanafumba macho teuzi zilizokaa kidini, na wanakuwa wakali kwelikweli pindi ukilisemea. Kuna wengine wanakua comfortable kukemea teuzi zilizojaa ujinsia lakini wanaogopa kukemea teuzi zinazonuka udini. Na Tupo wengine tuko tayari kukemea kila viashiria vya teuzi zenye sura ya udini, Ukanda, Ujinsia, Ukabila n. k

Sasa kuna Pattern ninayoiona katika Teuzi hizi kuanzia serikali ya Magufuli na ninaona zimeanza kujitokeza katika utawala wa Samia

Kwanini overall teuzi nyingi zinakuwa na Ratio zaidi ya (75-80%) Wakiristo na only( 20%-25%) Waislamu, Hii ratio inakuwaje fixed, Hii imetokea tu kwa nasibu au imewekwa by design?

Kwanini pattern hii inajirudiarudia kila mara, pindi uteuzi unaoinvolve watu wengi unapofanyika?

Mimi kama Mwananchi, mpenda mshikamano wa Kitaifa, ninaona kuna harufu ya ubaguzi wa makusudi katika kugawa keki hii ya Taifa, na kwangu mimi binafsi naamini na naamini pia maelfu ya Watanzania wenzangu wengi wapenda haki bila kujali dini zao hawalipendi hili, kwa hiyo ninasema wazi kuwa hili halikubaliki hata kidogo.

Nimeangalia leo teuzi za makatibu wakuu, naona kuna ratio kama ya waislamu Watatu au Wanne katika timu nzima ya makatibu wakuu Ishirini walioteuliwa hii ikiwa ni ratio ile ile ya 20% Waislamu na 80% Christians. Ningependa kujua, hii ni by design au kuna mchezo mchafu?

Kuna watu wanajenga hoja kuwa, hii ishu haina maana bali uchapakazi wa mtu —Hii hoja yangu bado ni muhimu kwa sababu zifuatazo

1. Hizi teuzi ni chanzo cha kipato, ni keki ya Taifa, Unapokuwa na watu janii moja wanaenjoy keki hii kuliko wengine maana yake unawaandalia hata vizazi vyao elimu bora zaidi, huduma bora zaidi za afya, nyumba bora zaidi kwa hiyo maana yake vizazi vya hawa wanaoenjoy sehemu kubwa ya keki ya Taifa leo, wana nafasi ya vizazi vyao kuendelea kuwa tabaka la juu katika nchi wakati hawa wengine wakiendelea kuwa kama raia wa daraja la pili!. Hili hakikubaliki.

2. Lakini teuzi za hivi zinazolalia upande mmoja ni hatari kwa umoja, amani na mshikamano wa Kitaifa—Haiwezekani teuzi za hivi zilalie upande mmoja halafu udhani kuwa wale wengine ambao wako marginalized wafurahi, hilo haliwezi kutokea

Kwa hiyo natoa wito sasa Kwa mamlaka za juu za serikali.

1. Lazima uchunguzi ufanyike kwa timu nzima inayohusika na kupeleka majina ya teuzi mbalimbali kwa Rais, Je hakuna udini katika kuchuja kwao majina?, na kama hakuna udini kwa nini hii pattern ya 20% by 80% inajirudiarudia, Kwa nini kwa mfano hatujawahi kuona teuzi zenye wauslamu 80% na Wakiristo 20%?

2. Tunataka kujua, je ni kweli hakuna waislamu wa kutosha kushika nafasi za juu kwa ratio nzuri? —Kama hawapo kwa nini? Na kama wapo kwa nini ratio inaendelea kuwa katika mtindo huo wa ALWAYS WAISLAMU NAMBA ZAO ZIWE Chini?

Suala la pili ni suala la Jinsia
Nimeona pia idadi ya wanawake walioteuliwa katika nafasi za makatibu wakuu ni almost negligible. Je, kwa utaratibu tuliokuwa tumeanza kukubaliana wa kufanya women empowerment, teuzi za namna hii zinasaidiaje katika ajenda hii?

Mada hii nataka iwafikie wafuatao

1. Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3. Mkurugenzi Mkuu wa TISS
 
Lengo lako kubwa ni kuyaongelea udini kwa kiasi kikubwa na sio angles zote kama ulivyojipambanua udini, ukanda na jinsia.

Kaparagraph kamoja ndo umeongelea gender ili ku dilute udini ulouandika, anyways you made sense ngoja wateuzi waje watujibu.
 
Rais - muislam

Waziri mkuu - muisilam

Katibu mkuu kiongozi - muisilam.

Sasa wewe mleta mda unataka Viongozi gani wa ngazi za juu tofauti na hao watatu?

Kwanza waislamu wengi tuko busy na Mambo ya Allah, kwanini unataka kutuingiza kwenye Mambo ya duniaa?

"Au nakosea ndugu zangu" R.I.P jiwe[emoji122]
 
Rais - muislam

Waziri mkuu - muisilam

Katibu mkuu kiongozi - muisilam.

Sasa wewe mleta mda unataka Viongozi gani wa ngazi za juu tofauti na hao watatu?

Kwanza waislamu wengi tuko busy na Mambo ya Allah, kwanini unataka kutuingiza kwenye Mambo ya duniaa?

"Au nakosea ndugu zangu" R.I.P jiwe[emoji122]
Serikali ina maelfu ya watu, hao ni sehemu tu, japo ni influential
 
Naunga mkono hoja, kwa maoni yangu rais kwenye uteuzi Kuna hatari ya kuzungukwa Kwa mfano uteuzi wa Sasa wa mama Sio Siri hauko balanced hasa ukiangalia jinsia. Hivi kweli kwenye utumishi wa umma katika idara zake zote hatuna kina mama wenye uwezo wa kuongoza taasisi au wizara? Mfumo wetu wa vetting umejaa who know you badala ya wenye sifa stahiki.

Ushauri wangu ni kwamba utumishi wa umma na menejiment zake zitengeneze database strong za watumishi wote wa umma na utendaji wao. Inapotokea uteuzi asiangaliwe mtu kwa jina Bali kwa sifa. Pia vyombo vya usalama vitumike kuchunguza na sio vyenyewe kutumia sifa hiyo kujiteua.
 
"Au nakosea ndugu zangu" R.I.P jiwe
emoji122.png
Swaga za mwendazake hakika hazitasahaulika mapema.
 
Mamlaka ya uteuzi ni rais, hata kukiwa na timu ni kushauri tu. Tujikite kwenye sifa za watu, tukianza kuchambua dini, kanda na makabila hatutamaliza. Kila mtu ana manung'uniko yake
Rais anapelekewa pool ya majina ya kuteua kutoka kwenye mamlaka za vetting, kama vetting imelalia upande mmoja basi chance ya wateuliwa wengi italalia upande huo, unless rais specifically aseme kuiambia mamlaka ya uteuzi imletee list pana ya watu wanaozingatia vigezo vya kazi lakini na demographia ya nchi ili aunde timu wakilishi!
 
Mada yako imejiweka kidini zaidi kuliko reality.

Reality is teuzi zinaangalia qualification, zinaangalia background, work history yako.

Kama nchi hii ina taratibu. hakuna kutoa cheo ku balance dini.

Ukianza kuendekeza udini kwenye nafasi za kazi, utaajiri watu wasio na qualifications just sababu ni wa dini fulani.

hii serikali si ya kidini. na haina dini. ni independent organ.
 
Back
Top Bottom