Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Rais anapelekewa pool ya majina ya kuteua kutoka kwenye mamlaka za vetting, kama vetting imelalia upande mmoja basi chance ya wateuliwa wengi italalia upande huo, unless rais specifically aseme kuiambia mamlaka ya uteuzi imletee list pana ya watu wanaozingatia vigezo vya kazi lakini na demographia ya nchi ili aunde timu wakilishi!
Unajua ni vigezo gani watu wa vetting wanaangalia?

Au unalalamika tu?

Oh rais aangalie demography,sijui aangalie nini.

Hizo mamlaka ziko kisheria. lazima vetting ilalie qualifications only. na ndicho wanachofanya.

No qualifications no rights. simple as thats. dini tupa kule
 
Kwani nchi ina wakristo wangapi na waislamu wangapi?

Je, nchi ina imani mbili tu za dini zinazotambulika kikatiba?
 
Ufanunuzi pls

Kuna msuguano wa idadi ya Wakristo na WaIslam hapa Tanganyika.Upande wa Zanzibar WaIslam ni zaidi ya 90% hili halina ubishi.

Tanganyika WaIslam wanadai wao ni wengi zaidi ya WaKristo,WaKristo nao wanadai wao ni wengi kuliko WaIslam.

Senso ya mwisho kabla kipengele cha dini hakijaindolewa idadi ya WaIslam na WaKristo zilikuwa karibu sawa huku idadi ya wapagani ikiwa kubwa sana nadhani 35% kama kumbu kumbu zangu zipo sawa.

Nina uhakika leo hii idadi ya waPagani (wasio amini katika Ukristo na UIslam) imepungua sana. Hiyo 35% itakuwa sasa ipo katika UIslam na UKristo itategemea na dini ipi ilifanya kazi ya kueneza imani yao katika kipindi cha kati 1960s hadi 1980s.

Unaweza kupata picha ingawa sio sahihi sana, kwa kutazama idadi ya watu katika makabila makubwa Tanganyika eg Wasukuma, Wahaya, Wachagga, Wanyakyusa, Wamakonde na Wamaasai.
 
mada yako imejiweka kidini zaidi kuliko reality.
reality is teuzi zinaangalia qualification, zinaangalia background, work history yako.

kama nchi hii inataratibu. hakuna kutoa cheo ku balance dini.
ukianza kuendekeza udini kwenye nafasi za kazi, utaajiri watu wasio na qualifications just sababu ni wa dini fulani.

hii serikali si ya kidini. na haina dini. ni independent organ.
Kwa hiyo Waislamu wenye vigezo hivyo nchi hii ni just about only 20% ila Wakiristo wenye hivyo vigezo ulivyovitaja ni more than 80%?
 
Wengine nao watasema muangalie makabila yote mnapoteua.

Wenye degree nao watasema wanasahaulika sana kwenye teuzi.

Wenye masters pia

Diploma pia.

Wapagani nao watasema sisi ndo hamtujali kbs.

Wasiosoma nao watataka fungu lao

Wenye sura nzuri nao watasema sisi tumesahaulika kbs

Waliopo uswahilini nao watasema hamna waZiri kateuliwa kutoka tandale

Weupe nao watasema baraza zima la mawaziri wote weusi, sisi wenye rangi nyeupe mbona tupo 2%tu

Sasa mtu mwenye uwezo mdog kama wewe unapata wapi nguvu ya kuandika post humu tena maneno mengiiiiii kana kwamba unajua hata unachokiandika yaani watu waache kuangalia sifa waanze kuangalia dini, rangi na sura
 
unajua ni vigezo gani watu wa vetting wanaangalia?
au unalalamika tu?

oh rais aangalie demography,sijui aangalie nini.

hizo mamlaka ziko kisheria. lazima vetting ilalie qualifications only. na ndicho wanachofanya.

no qualifications no rights. simple as thats. dini tupa kule
Ina maana watu wa dini moja ndo wana hivyo vigezo zaidi kuliko wa dini nyingine?
 
Mamlaka ya uteuzi ni raisi wala sio taasisi ya watu hapana, unaweza mshauri rais lakini yy kikatiba peke ake ndo mwenye mamlaka. Sasa mteuaji mwenyew muislamu boss wa makatibu Muislam, waziri mkuu pia Muislam.
 
tatizo la waislamu ni kwamba kila mahala wanataka wajenge msikiti. tizama vizuri idara yeyote ya serikali yenye kuongozwa na majority muslims kuna eneo limetengwa kwa ajili ya kuswalia humohumo kwenye facilities za kazi. huku ni kuchanganya dini na kazi na majungu mengine ya kuwaita watu makafiri.

tuchukulie mfano eneo la posta baharini kuna ofisi nyingi tu za umma. muda wa ibada za wakatoliki kwa mfano ukifika hushuka kuenda st. joseph cathedral wanasali wanarudi maofisini. waislamu ibada zao zikifika wanaanza kutandika mikeka ofisini. unaona utofauti?
 
Kabla ya bandiko lako umejaribu kuja ktk jamii na kuchunguza Mambo yafuatayo kwa asilimia

  • Mazingira na malezi ya hizo jamii mbili ulizozitaja yakoje na yapi bora zaidi?
  • Shule na vyuo zinazosimamiwa na hizo jamii mbili ulizozitaja zipi bora zaidi?

Nadhani ukiangalia vizuri unaweza kuwa na hoja ya msingi ktk bandiko lako
 
Huu mjadala unachochea udini, mleta mada ni mdini na mbaguzi.

Watu tunaangalia uwezo wa mtu na si dini kama mawazo yako yalivyo.

Wachochezi wa vurugu za kidini huwa mnaanza hivi hivi kidogo kidogo na mwisho mnamwagia petrol kabisa, na kuchoma nyumba tunaomba ushindwe kabisa na hiyo agenda yako.
 
Nilipofika kwenye Dini tu nikaishia hapohapo sikutaka kuendelea kusoma uz wako.
 
Rais anapelekewa pool ya majina ya kuteua kutoka kwenye mamlaka za vetting, kama vetting imelalia upande mmoja basi chance ya wateuliwa wengi italalia upande huo, unless rais specifically aseme kuiambia mamlaka ya uteuzi imletee list pana ya watu wanaozingatia vigezo vya kazi lakini na demographia ya nchi ili aunde timu wakilishi!
Labda tujiulize ni bias za makusudi au ni za kimazingira. Maana distribution ya dini au kabila huwa hazina usawa katika kila level. Let's assume umechukua list ya watanzania wote wenye PHD, distribution yao itakuwaje? Unaweza ukakuta katika hao probably Wahaya ni 10%, lakini population ya wahaya Tanzania sio 10% ya watanzania wote, au pengine ukakuta 70% ya hao ni wa dini fulani wakati hiyo dini doesnt not represent 70% ya watanzania.

Haya mambo ni complicated sana, hakuna majibu rahisi kwa sababu hakuna data pia.
 
Huu mjadala unachochea udini, mleta mada ni mdini na mbaguzi,
Watu tunaangalia uwezo wa mtu na si dini kama mawazo yako yalivyo,
Wachochezi wa vurugu za kidini huwa mnaanza hivi hivi kidogo kidogo na mwisho mnamwagia petrol kabisa,na kuchoma nyumba tunaomba ushindwe kabisa na hiyo agenda yako
Si vizuri kumhukumu mtu anayejaribu kuondoa ubaguzi wa kidini kuwa ni mdini.

Unachokifanya wewe ni kumhukumu anayekemea wizi kuwa ni mwizi!

Hizi mada ni muhimu tuzijadili ili kujenga Taifa fair, lenye umoja na mshikamano wa Kitaifa ambapo hakuna ubaguzi wa wazi(overt) au wa siri(covert) kwenye mgawanyo wa keki ya Taifa
 
Kwa hiyo Waislamu wenye vigezo hivyo nchi hii ni just about only 20% ila Wakiristo wenye hivyo vigezo ulivyovitaja ni more than 80%?
Jina lako linapopelekwa kwa tume za vetting.. dini inakuwa sidelined.
Yanaepelekwa majina ya mtu,si dini.

kama wahusika hawana qualifications wanaondolewa regardless dini zao.

no body care about dini. dini haikuongezei ufanisi kazini.

wana qualifications or not, that is up to vetting team.
 
Sidhani kama dini ni kigezo kabisa sababu serikali haina dini bali wafanyakazi wake ndio wana dini, ila ili kuleta umoja wa kitaifa ambao umekuwa ukidumishwa tangu alivyouasisi JKN, wamekuwa wakizingatia kabila na ukanda ili kuleta uwiano wenye uwakilishi sawia kutoka kila pande za nchi ikiwa wanaokusudiwa wana vigezo sahihi tu vinavyohitajika na sio vinginevyo.

NB: usigeneralize udini wa mtu kwa kuangalia jina tu kwa nadhiri huyu ni Abdallah basi ni muislamu , na yule ni David basi atakuwa tu mkristo. sababu hata wapagani wana majina hayo hayo... na kuna wengi pamoja na dini zao wana miaka hawaujui mlango wa msikiti wala kanisa. Asante
 
kama walioonekana wanakidhi vigezo.. outcome ya kuwa wamelingana dini hiyo ni irrelevant.
after all dini haikubebi kwenye usahili wowote ule.
so yes if that the case
I wish mazingira yangethibitisha hicho unachokisema, ila hii pattern inayojirudiarudia ya 20% by 80% rule inahitaji jicho kali la kiuchunguzi

Haiwezekani nchi hii vigezo fulani vinavyomandate teuzi kuwa vipatikane kwa wingi kwa watu wa dini moja tu kuliko wengine.

Hapa huenda kuna mchezo mchafu kwenye timu nzima ya vetting
 
Kuna msuguano wa idadi ya Wakristo na WaIslam hapa Tanganyika.Upande wa Zanzibar WaIslam ni zaidi ya 90% hili halina ubishi.

Tanganyika WaIslam wanadai wao ni wengi zaidi ya WaKristo,WaKristo nao wanadai wao ni wengi kuliko WaIslam.

Senso ya mwisho kabla kipengele cha dini hakijaindolewa idadi ya WaIslam na WaKristo zilikuwa karibu sawa huku idadi ya wapagani ikiwa kubwa sana nadhani 35% kama kumbu kumbu zangu zipo sawa.

Nina uhakika leo hii idadi ya waPagani (wasio amini katika Ukristo na UIslam) imepungua sana.Hiyo 35% itakuwa sasa ipo katika UIslam na UKristo itategemea na dini ipi ilifanya kazi ya kueneza imani yao katika kipindi cha kati 1960s hadi 1980s.

Unaweza kupata picha ingawa sio sahihi sana,kwa kutazama idadi ya watu katika makabila makubwa Tanganyika eg Wasukuma,Wahaya,Wachagga,Wanyakyusa,Wamakonde na Wamaasai.
Mkuu, hii mijadala ya dini ni mibaya na haina mwisho.

Juzi tu hapa watu walikuwa namasema Askofu Shoo(KKKT) kwamba amekuwa mkali utawala uliopita kwasababu Magu ni mkatoliki. Watu wapimwe kwa uwezo wao.

Tushukuru Mungu Kikwete hakuingia kwenye mtego wa dini kwenye sensa, ingeleta shida sana.
 
Back
Top Bottom