Tunahitaji Ufunguo mwingine wa Mafaniko, Elimu haifanyi kazi tena

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Zamani wakati tunasoma tulikuwa na Kauli mbiu kuwa "Education is a Key To Success" au "Education is a key to life"

Ikiwa na maana ya Elimu ni ufunguo wa Maisha au ufunguo wa mafaniko.

Lakini cha kushangaza tena Elimu sio tena ufunguo wa mafaniko ya maisha au kitasa cha mafanikio kimebadirishwa.

Sasa hivi waliofanikiwa zaidi sio waliosoma sana, bali wenye kujua njia za kupita au wenye kuwa na connection.

Tanzania One anazidiwa Maisha na Anko T..... Mwenye Elimu na aliyekuwa anakimbiza darasani kaajiriwa na mchora katuni au muimbaji.

Sanaa zamani ndio ilikuwa inaonekana ni ya vilaza au wasikuwa na Akili, lakini sasa hivi hapa bongo wenye Maisha ni wafanya sanaa. Darasani unakomaa na Hesabu unakuwa kipanga alafu kuna mwana yeye anakomaa na content creation badae wewe mkali wa hesabu unaishia kuwa mwalimu wa Mathematics pale Kazuramimba kigoma huku content creator akikaa mjini na kula Maisha mazuri.

Steve Mweusi na utahira wake kawazidi wasomi wengi maisha
 
C7106327-1C5E-4304-92F3-C4D447F2F924.jpeg
 
Ni kweli ila hali ya elimu kwa muda mrefu sasa, inafanya kuna baadhi ya sekta ambazo zina umuhimu ila maslahi yake yapo chini zinakosa watu wenye uwezo mkubwa
Fanya kama unajivua akili mkuu utanishukuru hela nyingi zipo kwenye matendo ya uchizi na ukichaa, ingawa wale machizi na vichaa kwenye wanaoshinda makaburini, majalalani, na kwenye mitaro hawalipwi chochote ila wale wanaoigiza uchizi ndio wanaziokota tu kwa hio fanya km unajivua akili hivi jifanye fala upate maslahi mazuri
 
Mleta mada nadhani hapo ulipo Una watoto.
Haya basi Acha kuwapeleka shule wakasome kwa kisingizio cha elimu sio ufunguo wa maisha tena

Jipe miaka kadhaa mbele, nakwambia utarudi hapa upesi kutengua hizi kauli zako
 
Elimu itaendelea kuwepo at least ya kuandika na kusoma, lakini hii education model ya sasa unaenda shule miaka 20 vidudu- University ili upate degree imeanza kufikia mwisho, hata AI ili ikufanyie kazi lazima ujue kuongea nayo, na inahitaji ujue kusoma na kuandika and some reasoning skills
 
Elimu muhimu cha msingi kujiongeza

Kabla hujafikiria kukata tamaa kwenye haya maisha, Hebu angalia nywele zinazoota kwenye makwapa Licha ya mazingira magumu, bado zinaendelea kukua.
Sio hizo bana, zile za sehemu nyingine😂🏃🏽‍♀️
 
Zamani wakati tunasoma tulikuwa na Kauli mbiu kuwa "Education is a Key To Success" au "Education is a key to life"

Ikiwa na maana ya Elimu ni ufunguo wa Maisha au ufunguo wa mafaniko.

Lakini cha kushangaza tena Elimu sio tena ufunguo wa mafaniko ya maisha au kitasa cha mafanikio kimebadirishwa.

Sasa hivi waliofanikiwa zaidi sio waliosoma sana, bali wenye kujua njia za kupita au wenye kuwa na connection.

Tanzania One anazidiwa Maisha na Anko T..... Mwenye Elimu na aliyekuwa anakimbiza darasani kaajiriwa na mchora katuni au muimbaji.

Sanaa zamani ndio ilikuwa inaonekana ni ya vilaza au wasikuwa na Akili, lakini sasa hivi hapa bongo wenye Maisha ni wafanya sanaa. Darasani unakomaa na Hesabu unakuwa kipanga alafu kuna mwana yeye anakomaa na content creation badae wewe mkali wa hesabu unaishia kuwa mwalimu wa Mathematics pale Kazuramimba kigoma huku content creator akikaa mjini na kula Maisha mazuri.

Steve Mweusi na utahira wake kawazidi wasomi wengi maisha
Naunga mkono..ila vyeti uwe navyo tu. Siku vikihitajika uwe navyo. Sio utupwe kwenye mchujo..
 
Fanya kama unajivua akili mkuu utanishukuru hela nyingi zipo kwenye matendo ya uchizi na ukichaa, ingawa wale machizi na vichaa kwenye wanaoshinda makaburini, majalalani, na kwenye mitaro hawalipwi chochote ila wale wanaoigiza uchizi ndio wanaziokota tu kwa hio fanya km unajivua akili hivi jifanye fala upate maslahi mazuri
Tujikite kwenye mada ya mtoa mada mkuu 😁
 
Back
Top Bottom