Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 7,875
- 12,665
Ndio! Pamoja na mapungufu yote ya uongozi na uendeshaji wa mwendokasi kuna tatizo kubwa sana la WATANZANIA
Watanzania kwa maana ya watumiaji wa mwendokasi na madereva hawa watu sio wastaarabu kabisa katika utumiaji wa vyombo hivi vya usafiri. Mtu unaona gari limejaa mpaka mlango haufunguki badala ya kusubiri lingine unalazimisha kuingia hadi milango inang'oka na vile hamna konda wanajibana watakavyo
Madereva walioajiriwa sio wastaarabu kabisa katika uendeshaji wa haya magari, hawajali muda kwanza wao ndio maboss abiria kwao ni kama ombaomba.
Gari linapelekwa kama halina mwenyewe dereva hata aone gari imejaa hafanyi jitihada yoyote kuhamasisha watu wasubiri lingine kwani yeye ndio dereva pia ndio konakta lakini pia kuna migambo kwenye vituo vya mwendokasi kwanini wasifanye kazi kusimamia ujazo wa magari haya kuliko kuyaover load mwisho wa siku yanawahi kuchakaa
Tutaendelea kuilaumu mwendokasi lakini bila ustaarabu na matumizi sahihi ya magari haya hamna kitakachofanyika kwanza watanzania tustaarabike katika kutumia vyombo vya umma
Ahsanteni