Tunailaumu mwendokasi lakini na hili pia ni tatizo

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Ndio! Pamoja na mapungufu yote ya uongozi na uendeshaji wa mwendokasi kuna tatizo kubwa sana la WATANZANIA

Watanzania kwa maana ya watumiaji wa mwendokasi na madereva hawa watu sio wastaarabu kabisa katika utumiaji wa vyombo hivi vya usafiri. Mtu unaona gari limejaa mpaka mlango haufunguki badala ya kusubiri lingine unalazimisha kuingia hadi milango inang'oka na vile hamna konda wanajibana watakavyo

Madereva walioajiriwa sio wastaarabu kabisa katika uendeshaji wa haya magari, hawajali muda kwanza wao ndio maboss abiria kwao ni kama ombaomba.

Gari linapelekwa kama halina mwenyewe dereva hata aone gari imejaa hafanyi jitihada yoyote kuhamasisha watu wasubiri lingine kwani yeye ndio dereva pia ndio konakta lakini pia kuna migambo kwenye vituo vya mwendokasi kwanini wasifanye kazi kusimamia ujazo wa magari haya kuliko kuyaover load mwisho wa siku yanawahi kuchakaa

Tutaendelea kuilaumu mwendokasi lakini bila ustaarabu na matumizi sahihi ya magari haya hamna kitakachofanyika kwanza watanzania tustaarabike katika kutumia vyombo vya umma

Ahsanteni
 
Kila mtu anataka kuwahi mjomba, mtu kasubiri gari saa zima, limekuja eti asubiri saa jingine na kanafasi ka kujibanza huku akifaidi udungadunga ipo.

Waoneze mabasi, mbona daladala zikijaa mtu anaacha ipite tu maana anajua zipo kibao, achilia mbali ikijaa wengine hata kusimama tu hawataki, anaacha ipite anasubiri yenye siti.

Hizo mwendokasi ukiiacha iende, nyingine ni baada ya masaa kadhaa.
 
Mkuu, magari yangekua mengi hayo mambo ya kujazana yasingekuepo.

We shahidi, unasubiria gari pale Kkoo 2 hrs hivihivi hafu chuna zinapita tu kama haziwaoni.
Kabisa mkuu, hamna anaependa kubanana. Mpaka dereva anaacha mjae vile nae anajua fika wapo wachache na sia ajabu yeye ndo inabidi aende na arudi kuja kuwachukua tena.
 
Mkuu, magari yangekua mengi hayo mambo ya kujazana yasingekuepo.

We shahidi, unasubiria gari pale Kkoo 2 hrs hivihivi hafu chuna zinapita tu kama haziwaoni.
Tatizo ni madereva ni mabwenyenye sana akipaki gari hapo anaenda lodge akirudi ndio aangalie route magari mengi yapo tu yamepaki na wala hayana tatizo lolote na madereva nao wanachangia wamezidi uboss
 
Ustaarabu ni mdogo sana kwa watumiaji wa mwendokasi.
Kabisa watu hawazingatii matumizi sahihi ya haya mabasi unakuta nafasi zimejaa mtu anakaa mlangoni dereva akifungua mlango unakwama hadi umpush ndio ufunguke
 
Kwa hiyo Mwendokasi haina amanagement?
 
Usha wahi kupanda mwendo kasi kweli..? Hao watu huwa wana panga kabisa abiria na wanasimamisha gari hata likiwa limejaa wanafungua milango abiria waingie. Na madereva tutawalaumu tu inaonekana ni maagizo kutoka juu mkuu. Zile gari zinajaza mpaka kama una afya ya mgogoro pole yako
 
Hayo yote ni Kwa sababu ya Muda
Je mabas yangekuwa mengi sana na nafasi zingekuwa za kutosha
Wangefanya hivyo?

Ustarab uzingatiwe na pia Mabasi yaongezwe
 
Ndio maana nasema hawajui matumizi sahihi ya haya mabasi wanayaoverload ndio maana yanachakaa haraka
 
Kaa vituoni mfano Gerezani Alafu subiri gari kama ya Route ya Kimara utaelewa vzr hoja za Watu kulalamika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…