Nguvu au ishara pekee iliyobaki wanayoitegwemea ccm ni muungano. Azimio la Arusha limesha kufa, na hata siasa za Arusha hawanaushawishi nazo tena. CDM wamejikita kwelikweli. Enzi za Nyerere Arusha ilikuwa ngome kuu ya ccm. Kwa sasa, ngome ya ccm kubwa ipo Unguja na Pwani. Hizi sehemu nyingine wanacheza patapotea tu kupata kura. Hauwezi kusema ni ngome. Tatizo ni kwamba nguvu ya CUF Pemba inawasumbua sana huko Zanzibar. Muungano umekuwa kama Jinamizi. Kila kukicha maadui wapya wanajitokeza na ushawishi wa ccm unapungua. Muungano umekuwa kama a hidden treasure in the 'lord of the rings' kwa ccm. CCM is too obsessed na Muungano kiasi kwamba hawataki hata Kuuboresha. Hawasikii, hawaonii, hawaambiliki wala hawashauriki. Sijue ndo kifo cha nyani hicho?
Tatizo kadiri wanavyozidi kuutetea muungano ndo wanavyozidi kuuuwa. Miaka michache iliyopita watanganyika ulikuwa huwasikii wakizungumzia habari ya muungano. Waziri mkuu Pinda alikuwa ajua Zanzibar ni mkoa tu. Sijue ibilisi gani akamwingina Mh Dhaifu, akaruhusu Zanzibar wabadili katiba kuwa nchi, na bendera kabang!! Katika kufurahia mafanikio hayo, Mh Dhaifu akajikuta kumbe ndo kajiongezea maadue maradufu kutoka Tanzania bara, haswa haswa kaskazini na nyanda za juu kusini. Hili jambo lilikera watz sana. Kinacho endelea sasa hivi nikutolewa kwa uhamuzi mwingine wakijinga na viongozi waccm, then utasikia maadui wengine wataibuka, sijue itakuwaje. Ule mtaji wanaoutegemea unazidi kupungua tu. Wao wenyewe kila kukicha ni minyukano tu ndani ya chama. Mwisho wa siku utasikia habari yake, itakuwa kama titanic vile ilivyo zama katikati ya bahari. Abiria chunga mzigo wako.
Sifa moja ya hii trend ni kwamba it is irreversible. CCM siku hizi inapokonyana ubunge na yama vya upinzani!!!! Haijawi kutokea hii. Mbaya zaidi CDM na CUF hawaichii mwanya ipumue hata kidogo, wanagonga mulemule. CDM na NCCR wanagonga mikoani, CUF pwani na Zanzibar kwenye ngome yoa iliyobakia. Lazima kuna kitu kitatokea. Wataalamu wanatumia neno la kitaalamu 'dynamics'. Soon after one generation, ccm itakuwa haina tofauti na vyama vingine kama CUF na CDM. A major catastrophy itakuwa muungano. Ni vigumu kutabiri what will be the outcome ya katiba mpya.